Siwachongei TFDA lakini ni kweli Mchele wa Plastic upo na unauzwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,720
2,000
Hii hatari sana,lakini Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA)wanasema hawana taarifa yoyote rasmi ya kuwepo kwa mchele aina hiyo wa plastiki hapa nchini.

Lakini pia taasisi hiyo ya TFDA inawaasa wananchi watoe ushirikiano wa taarifa za mchele huo ili hatua za haraka zichukuliwe.

Kila siku TFDA wanasema huo mchele haupo. Mimi nmeshindwa kuelewa. Kama sio wa Plastic, ni mchele gani huu? Kama vipi tuwatumbue tuwaweke watakaoweza kutuambia ni mchele gani.

UPDATES:

TFDA imeunda kikosi maalum ili kupata ukweli juu ya mchele unaodaiwa kutengenezwa kwa kutumia plastiki baada ya picha kusambaa mitandaoni.
=>TFDA imeunda kikosi Maalum kuchunguza Mchele wa Plastiki

======

UPDATE:

Shirika la viwango Tanzania TBS limetoa maelekezo kwa wananchi kufuatia taarifa za hivi karibuni kuwa kuna bidhaa ya mchele ambayo inaodhaniwa kutengenezwa kwa plastiki.

Hivi karibuni zimezuka taarifa kupitia video na picha kupitia mitandao ya kijamii (Istagram na whatsap) zinazoelezea hofu ya uwepo wa bidhaa ya mchele inayosadikika kutengenezwa kutokana na plastiki.

Baadhi ya video hizo zinaonesha mtambo unaosadikika kutengeneza mchele kutokana na mifuko ya plastiki, huku nyengine zinaonesha wali ukifinyangwa kisha kudundisha kwenye sakafu kama mpira.

Shirika la Viwango Tanzania TBS limesema kuwa sheria ya viwango namba 2 ya mwaka 2009 baada ya kupata taarifa hizo lilifanya utafiti katika soko (surveillance) ambapo jumla ya sample 21 za aina mbali mbali za mchele zilichukuliwa katika maeneo mbali mbali ya masoko na kupimwa ubora wake na kupimwa katika vipimo vya TBS.

Majibu ya uchunguzi wa maabara yanaonesha mchele uliopo katika soko la Tanzania ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Kutokana na majibu hayo ya kisayansi shirika linafahamisha umma kwamba taarifa zinazosambaa kuhusiana na kadhia hiyo ni kwamba hazina ukweli wowote na shirika linawataka wanajamii kuondoa hofu juu ya suala hilo.
FB_IMG_1500156218403.jpg
 

mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,564
2,000
Hii hatari sana,lakini Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA)wanasema hawana taarifa yoyote rasmi ya kuwepo kwa mchele aina hiyo wa plastiki hapa nchini.

Lakini pia taasisi hiyo ya TFDA inawaasa wananchi watoe ushirikiano wa taarifa za mchele huo ili hatua za haraka zichukuliwe.

Naomba msinichukue kusaidia upepelezi. Ntaweka Video sasa hivi.
Kupitia huu uzi naomba kujua course gani zinapelekea watu kupata kazi katika taasisi hii pamoja na TBS.
 

Silasy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
732
1,000
Hakuna digestion ya plastic kwenye tumbo la binadamu ebu tuache uzushi na sayansi ichukue mkondo wake,kama binadamu angeweza kula plastic na akaishi bila tatizo Basi pia angeweza kula cellulose (majani) kama ngombe na akaishi katika hali ya kawaida ili plastic ichemke inahitaji joto linalozidi boiling point ya maji na hata ikichemka ikapoa kwa joto ambalo binadamu anaweza sasa kula au kutia mdomoni plastic inakuwa tayari imeshaganda,kwa hiyo ukiona huo mchele unaodai wa plastic umeweza kuufinyanga mkononi bila kuungua na kisha ukaula na next day ukapata Choo that isn't Plastic ni something else!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom