wise-comedian
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 3,290
- 3,946
Kwani hadhi yako ni sawa na rais kikatiba?Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.
Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?
Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Umedandia treni kwa mbele!kwani sheria inayotumika kutoa hukumu ni moja au ziko mbili kwa minajili ya asiye na cheo na mwenye cheo?
Mhesh. Lema unafahamu suala hili limekuwa mjadala kutokana na mambo mawili; 1. Kwa bahati nzuri wakati kijana yule anatiwa hatiani kwa kosa la "kumwita Rais kuwa ni bwege" kule Arusha, kule Dodoma naibu spika wa Bunge alikuwa ametoka kumdhalilisha mbunge wa upinzani kwa kumwambia kuwa "aache ubwege wake". 2. Sheria ya mtandao imeibua maswali mengi mno mno!"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.
Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"
Godbless Lema (Mp)
Watu tunachokiongelea hapa ni double standards.. Matusi si mazuri kwa pande zote sio upande mmoja tu.. Kwahiyo na sisi tulioitwa malofa na wapumbavu tukiamua kujikusanya kupeleka shauri mahakamani Mr. Clean ataadhibiwa??
Wewe kama Mwanasheria naomba unijibu hilo..
Jamani juzi nkatika kipindi cha dakika 45, nilimsikia G Lema wa CDM akisema kuwa hana ID yoyote katika mtandao wa kijamii wowote. Sasa hii imetoka wapi?"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.
Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"
Godbless Lema (Mp)
Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Nimeweka hoja ya ulinzi wa Rais kukuonyesha mantiki ya tofauti kati ya Rais wa nchi na wananchi mwingine.
Kusema wewe hauna tofauti na Rais wa nchi ni kuongea kwa kinadharia lakini kiuhalisia Rais wa nchi na wananchi wa kawaida wako tofauti.
Hapana. Wewe unaongelea dhana ya kinadharia inayosema binadamu wote ni sawa lakini kiuhalisia binadamu wote siyo sawa.
Rais kutokea miongoni mwa wananchi hakumfanyi awe ni sawa na wananchi wengine katika matendo na majukumu yake kama Rais.
Matendo na majumu ya Rais ndiyo yanamfanya awe ni tofauti na wananchi wengine ndiyo maana hata Katiba ya Tanzania 1977 katika Sura ya Pili, Ibara ya 33(1-2) imebainisha ukweli kuhusu umuhimu wa Rais wa nchi.
Lazima uelewe kuwa kujiheshimu ni kuheshimiwa.
Ninapoongelea Rais nina maana taasisi kwa ujumla wake.
Rais Magufuli amevaa taasisi ya Urais na kutokana na taasisi hiyo, anatakiwa kisheria ajiheshimu.
Wewe mwananchi unaweza kuchagua kutojiheshimu na hakuna mtu au sheria inayokutaka kujiheshimu.
Rais hawezi kuchagua kutojiheshimu na kama atataka kufanya hivyo basi inabidi aachie madaraka.
Hii ndiyo tofauti ya msingi kati ya Rais wa nchi na mwananchi wingine.
The truth will always set you free. Your words are as informative, educative and liberating tool as a real politician"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.
Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"
Godbless Lema (Mp)
Khee kilichovunjwa ni heshima ya mtu... na si uraisi wake... BINADAMU ANASTAHILI HESHIMA NA KUTHAMINIWA UTU WAKE.... nyie mnaodhani raisi nibmtu zaidi yako mnakosea... na ndo mnaoleta dhana ya umalaika..Kwa hiyo unataka kujilinganisha na Rais wa nchi?
Gharama za kukutunza unataka kuzilinganisha na gharama za kumtunza Rais?
KWA sababu rais ni ndogo wa Mungu???Ukitukanwa mahakama ipo...
Ni jukumu lako kwenda mahakamani...
Akitukanwa Rais wapo wa kumwendea mahakamani sababu ni Rais...
Vyeo vinaenda na privileges ...huwezi kujilinganisha na mwenye cheo...ni kutafuta BP tu...
Mila, taratibu, kaninu za Marekeni tofauti na zetu na walipofikia wanatamani kubadikikakakini ni too late. NAdhani tujadili kwa context ya Tanzania na utamaduni wake!Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Yaani we ndio huja muelewa kabisa keywords ya Lema ni haya hapa "LAKI KUMWAMBIA HUYU KIJANA AMEKOSEA NI JAMBO LA BUSARA ZAIDI" Ana maanisha adhabu yote aliopewa haina maaana mpaka anaangaika kwenda kuchangisha watu na badala yake wangewezwa kumuonya kwa busara na akaelewa na kuwa balozi mzuri wa maadili.Mkuu, kama umemsoma vema Lema amewakemea na hao wanaomchangia. Soma vizuri utaelewa
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.
Bwege sio sahihi hata kidogo Lakini kwa mtoto unamkanya sirudie tena. vile vile sio sahihi kuwaita watoto kama mzazi uliyezaa na una watoto V ,LAZA9. Mzazi hapo ameteleza vile vile- najua alikuwa labda kama anatania, lakini utani mwingine unaumiza roho! Ni sawasawa kumwambia mtu anayeanguka kifafa kuwa "ondoa kifafa chako hapa" ataumia sana hata kama ulilenga utani.,Kwani kukosoa lazima utukane au kutoa maneno ya kudhalilisha?? Kosoa kwa kutoa hoja sio VIOJA.
Na kama unaona hilo neno bwege ni sahihi basi jaribu kumuita mzazi wako hivyo ndiyo utaelewa uzito wake.
Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....