Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Mama soma na utafakari acha kukurupuka....

Mtu kama wewe kweli hata ukileta habari za kweli JF watu si wanakupuuza tu...wewe niite upendevyo mie sijali chochote hayo ni matunda ya makuzi yako.
 
Ungetafuta nafasi kwenye gazeti la Tanzania Daima nadhani ungesomeka vizuri.

Asante kwa kutambua kuwa gazeti la Tanzania Daima ndiyo inayoandika habari za ukweli, za wanaodai na kutetea haki na usawa!

Inashangaza tbc mpaka sasa hawajatangaza kilichomtokea Dr. Ulimboka
 
Sisi wananchi tunawajibika kwa kuiweka madarakani serikali dhaifu,mateso tunayoyapata siyo kwa sababu madaktari hawatupendi bali kwa sababu serikali tuliyoikabidhi mamlaka ya kutetea afya zetu,wanatetea afya zao. Hata kama watawadhuru madaktari wote ili wajisikie maumivu kama watanzania wengine,bado halitakuwa suluhisho. Mkuu Gimmy,nimekuita DHAIFU kwa sababu unadhani Ulimbuka vile amepigwa na kujisikia maumivu basi litakuwa funzo.Watu waliomdhuru Ulimboka wametumia NGUVU NYINGI-AKILI KIDOGO.Sisi wananchi tunatakiwa tumjue adui yetu ni nani? We unaona adui no.1 ni Madaktari.I think you have applied illogical premises to the problem as you got imaginary truth and not an absolute truth.Try to think beyond the box then,you will recognise your true enemy unless wewe ndo umekurupuka!
 
Ni wakati wa Ulimboka kutafakari u nyeti wahuduma mahospitalini,
si furahishwi na alicho tendewa ulimboka ila pia sifurahishwi na maamuzi ya madkari akiwemo na Ulimboka kama kinara wa mgomo,
naamini dr ulimboka akipata nafuu anaweza hisi watanzania wanateseka kwa kiwango gani na migomo yenu,je kama wewe ungeachwa bila huduma nini ingekua hatma ya maisha yako?
lazma tuache ushabiki kwani watu wanaangamia kwa mgomo huu,
ni ajabu watu kuonesha huruma kwa ulimboka pekee ambae kimsingi hakuwahurumia wagonjwa wenye hali kama yake au mbaya zaidi ya hali alionayo sasa.
Madkatari tafuteni njia mbadala kuwabana serikali kwani mnatuua watanzania wenzenu bila hatia

Madakatari hawawatesi walalahoi, bali wanateswa na wanasiasa wao kwa vile wanasiasa hao wanatibiwa nje tu; hata mafua !!. Ningekuwa daktari wa tiba, nadhani wanasiasa wote wangeigopa kabisa taaluma ya udakari hasa kwa vile tuna huduma mbovu sana za afya, na madaktariwamekuwa wanafanya kazi ya ziada kutibu magonjwa ambayo hayangetakiwa kuwapo kabisa.
 
mkipasuliwa vichwa badala ya miguu msije kulalamika, hakuna kitu kibaya kama kufanya kazi kwa manung'unguniko.
 
Igunga, Arusha, Arumeru anayejua na pengine aongeze kote huko Srilaki ya CCM imeua, kwa hili la Ulimboka ni Mungu tu ndiyo amemnusuru ili ukweli ujulikane, hakika Mungu ni mwema AMPONYE HARAKA Dr. Ulimboka.
Piiiiiiiiiinda mnafiki mkubwa na kujiita mtoto wa mkulima, liwalo na liwe sasa ndiyo hilo limekuwa damu ya huyo kiumbe itakuwa juu yako na kizazi chako
 
Nacho amini HAKUNA UKOMBOZI BILA SADAKA. hapa haikwepeki both gvt and drs they have to resolve the crisis. coz cont delaying tha isue mahafa ni makubwa. MUNGU WANGU TUONYESHE NJIA.
 
watu wengi wanasashau 'mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu' kupata kwake matatizo ni njia moja wapo ya kumwonyesha maumivu wanayoyapata wagonjwa wengine wanapokosa huduma ya daktari, naomba kuuliza mgomo huu wa madaktari anayathirika ni nani kama siyo mwananchi wa hali ya chini jamani? Wakuu wote katka serikali wanatibiwa nje ie India South afrika, Ujerumani nk, hivyo madaktari tunayakubali madai yen lkn kumbukeni na afya zetu

lakini pia inabidi ujiulize,ni kitu gani ambacho waheshimiwa wanakifuata mahospitali ya huko India na Ujerumani!
Kama hicho kitu hapa Tanzania hawakioni,basi Madaktari ndo wanachokitaka.
Kikipatikana hapa basi hata waheshimiwa watakwenda Mwananyamala kama mimi na wewe na hvyo kuokoa mabilioni yanayopelekwa India na kwengineko.
 
Baada ya kutafakari nasema, Ulimboka ni turufu iliyotumiwa na wasiyoitakia mema Serikali iliyopo madarakani:

Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.


Mlio tumia hii turufu mmelamba jike.

Nakubaliana na mleta mada kwa kilichomkuta Ulimboka.

Mi nilidhani ukilaza nilio nao ndo ulonifanya kudhani kuwa hawa waliofanya kituko hiki nao ni mageneous...!!! kumbe lengo lao wamuonjeshe na yeye ladha ya kutotibiwa kidogo...
Sisemi kwa ushabiki bali waTZ tuache kukurupuka kufuata mkumbo... Uli ni sehemu ndogo sana ya kufanya threat kwa serikali, ingewezekana kabisa kupuliziwa hata sumu akafa kimyakimya kama angekuwa ni kikwazo. wapo watu wanaosubiri opportunity ndogo tu na wao watumie mwanya huo kuzidi kuibomo serikali...
As a GT nasubiri upande wa pili wa shilingi, subirini tamko la polisi halafu mpime uzito wa hoja yangu. Naamini si polisi wala usalama wa Taifa waliohusika.
 
kufanya mizaha na madactari ni kufanya mzaha na afya ya wa tz. Nimeamini serikali imeshindwa kazi hiv jk, pinda, waziri wa afya na naibu wako, katibu mkuu wizara ya afya wote mmekaa chini mkatafakari na kufikia conclusion la kumpiga Dr. Ulimboka? Nilikuwa siwaamini lakini sasa mmeniongezea lingine nina wasisi na shule zenu na uwezo wenu wa kufanya maamuz hasa ktk mambo nyeti kama hili la mgomo wa madactari! Poor tanzania! Mlichokifanya mmemwagia petroli moto. Subirini matokeo yake. Kila la kheri!
 
MIMI NASHANGAA WATU WANAVYONYOOSHEA VIDOLE SERIKALI.

1. Huyu Ulimboka kama Serikali ingekuwa inataka kumshughulikia wangefanya kwa muda muafaka.
2. Kuna wanaosumbua serikali wengi, mbona hawaja Ulimbokwa?

Nadhani tuwe balanced

Nadhani tusifanye incitement

Nadhani Mgomo ulikuwa batili

Nadhani anayeumia na Mgomo huo sio JK wala Pinda

Nadhani hata akiondoka JK au Pinda; sio suluhisho la Mgomo huo

Nadhani LHRC wanatumiwa kama vehicle ya uchochezi

nadhani kuna siasa mbaya ya kuihujumu serikali kwenye hili

we unadhani wahusika ni kina nani zaidi ya serikali dhaifu iliyoona njia rahisi ya kuzuia mgomo ni kumuua kiongozi wa mgomo,
 
Ndugu yangu unaonekana una upungufu wa ufahamu wa kujua chanzo cha matatizo kama ambavyo viongozi wengi wa taifa hili walivyo.

Kuwalaumu madaktari na zaidi Dr. ulimboka uanaonekana ni namna gani ulivyomfinyu wa ku analyse sources of problems. Na kwa taarifa yako chanzo cha matatizo yote haya ni wewe mwenyewe, tena wewe, kwa sababu umeshindwa kuchagua serikali makini au hata kuiadabisha pale inapokosea na kuitaka ifanye kile unachotaka ikufanyie.

Labda kama ulikuwa hujui ni kwamba, haki haiji kwa lele mama kama unavyofikiri, hata uhuru wa nchi hii kuna watu walipoteza maisha. Big up kwa dr Ulimboka (get well soon), na madaktari wote waliogoma kwa ujumla na naziomba taasisi zingine nyeti zigome tafadhali.

Udhalimu lazima ufike mwisho wake, tumechoka kuonekana wajinga mara zote
 
lakini pia inabidi ujiulize,ni kitu gani ambacho waheshimiwa wanakifuata mahospitali ya huko India na Ujerumani!
Kama hicho kitu hapa Tanzania hawakioni,basi Madaktari ndo wanachokitaka.
Kikipatikana hapa basi hata waheshimiwa watakwenda Mwananyamala kama mimi na wewe na hvyo kuokoa mabilioni yanayopelekwa India na kwengineko.

HATE.... ningekupiga bonge la hate lingekuwepo...
Ishu ya kudai wanatetea maslahi ya wagonjwa ni uongo tu, wanajaribu kuvuta hisia za watu wawaone wana maana na kuwasupport.

Embu fikiria... jamaa wanasomeshwa bure elimu ya chuo kikuu... ambapo wengine wanasota kuomba mkopo ambao baadae wataurudisha ili kusoma fani wanazopenda lakini wanatoswa, wanapewa madaktari. Udaktari ndo miongoni mwa fani zinzaoongoza kwa mshahara mkubwa mara wanapoajiriwa serikalini achilia mbali marupurupu ya lukuki. wametuacha mbali sana tu sisi walimu, maafisa utumishi, wahasibu na wengineo.

Hawastahili kutia pamba masikioni, wakagoma kwa kigezo cha kututetea. Watusaidie kwa kinachopatikana hicho hicho kuliko kutuadhibu kwa ujuzi walioupata ambao kwa hakika, KATU hawataweza kuzilipa fadhila za elimu waliyopata kwa kodi zetu hizi hizi za kuuza maandazi sisi walala hoi.
 
Back
Top Bottom