Madaktari kuchati kazini: Ongezeko la machekibobu

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
4,690
10,194
Japo madaktari wote ni makasuku wanaomeza madesa ya shule na kuyakariri jinsi yalivyo, lakini mnyonge mnyongeni, nchi hii walikuwepo madaktari bwana!

Kuna madaktari ukiwaambia naumwa kichwa anakimbilia kukudunga chanjo ya FANSIDA, sijui ni kukariri ama ndivyo walivyofundishwa huko mashuleni?

Mimi mzee wangu alikuwa daktari, tena daktari nguli aliyeheshimika haswa kutokana na huduma zake. Hawa ni wale madaktari wa zamani ambao akikuhudumia unasema kweli hapa nimehudumiwa na DOKTA HASWA!

Madaktari wa enzi hizo ukiwafuata hadi unahisi raha kuhudumiwa. Utakaguliwa, utabonyezwa bonyezwa vimashavu vyako, unaachama mdomo unamulikwa koromelo na kitochi, yaani hadi raha!!!

Baadaye unawekewa la kupimia moyo, huku daktari anakuhoji kitaalamu na kwa ufanisi.

Lakini siku hizi kumezuka wimbi la MACHEKIBOBU wanaojiita madaktari. Hawawezi kukuhudumia wana mapepe na mawenge muda wote.

Unashtukia daktari amerukia kipima moyo, mara amekitupa mezani, anakurupuka nduki anawahi kuchungulia meseji ya Instagram. Akikuhurumia sana anakudunga chanjo la KOVIDI.

Akikuhoji wala hakuangalii usoni, kaweka EARPHONES anasikiliza singeli ati! Ni mwendo wa Unasemaaaa!!!??? Eeeeh, unasemajeee!!??? Eeeeeeeh?? sijasikia umesemaaa??? Eeeh nasemajeeee!

MY TAKE: Hili nalo mkalitizame.
 
Wanachonikera mimi ni tabia yao mpya ya kupenda kupima watu ukimwi

Kuna siku nimeumwa kichwa nikaenda kupima Malaria, baada ya kipimo akasema malaria yangu ni ndogo kiasi kwamba sihitaji kutumia dawa bali nitumie muda mwingi kupumzika na kunywa maji

Cha ajabu akashauri eti unaonaje tukupime na ukimwi? Nikamwambia acha ufala, mimi nimekuja kupima malaria siyo ukimwi, nikaondoka
 
nimechekaa.
 
Katika Watu Wanaopenda Wanachokifanya Ni Hawa Madaktari.

Daktari Karibia Wote Wanakutibu Na Wanapenda Kufanya Hivyo Sababu Wajajifunza Na Kupata Case Mpya Ambayo Inawaongezea Experience.

Madaktari Wanafanya Kazi Kwa Passion Kubwa Mnyonge Mnyongeni Ila Haki Yake Mpeni.

Wewe Itakuwa Unaenda Zahanati Na Kwenye Vituo Vidogo Vya Afya Ambavyo Unakutana Na Waliovaa Makoti Meupe Ukadhani Ni Daktari.

Jitahidi Kwenda Vituo Vya Afya Vikubwa Vyenye Kutambulika Kuepuka Kukutana Na Hao Wahuni.
 
Wanachonikera mimi ni tabia yao mpya ya kupenda kupima watu ukimwi

Kuna siku nimeumwa kichwa nikaenda kupima Malaria, baada ya kipimo akasema malaria yangu ni ndogo kiasi kwamba sihitaji kutumia dawa bali nitumie muda mwingi kupumzika na kunywa maji

Cha ajabu akashauri eti unaonaje tukupime na ukimwi? Nikamwambia acha ufala, mimi nimekuja kupima malaria siyo ukimwi, nikaondoka
... bajameniii!!! ...sasa kutaka kukupima ukimwi si alikuwa anakutakia KHERI lakini!!!?
😅
 
Wanachonikera mimi ni tabia yao mpya ya kupenda kupima watu ukimwi

Kuna siku nimeumwa kichwa nikaenda kupima Malaria, baada ya kipimo akasema malaria yangu ni ndogo kiasi kwamba sihitaji kutumia dawa bali nitumie muda mwingi kupumzika na kunywa maji

Cha ajabu akashauri eti unaonaje tukupime na ukimwi? Nikamwambia acha ufala, mimi nimekuja kupima malaria siyo ukimwi, nikaondoka
Mim nimeenda kupima U.T.I ila vipimo na Cha ukimwi wakaweka ila mi nikajikausha kimya ,nikamuuliza sasa hicho kingine Cha nin akasema malaria sasa wakati hapo ashanichoma kwenye kidole na akaweka damu kwenye ki glass ili apeleke ,alafu damu nyingine akaweka kwenye kile kidude Cha kupimia ukimwi ....majibu hata hakunipa kama yakoje ndo nashindwa kuwaelewa kwanini anakupima alafu majibu hatoi

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom