Kukiwa na songombingo la kujiuliza kuwa hawa madaktari wetu , watagoma au hawatagoma?
Huku mitaani wananchi wameanza kukosa imani na hawa wataalam wetu wa utabibu kwa kutoa takwimu zifuatazo:
- Waliomba Mganga Mkuu aondolewe-Dr Deo Mtasiwa, akaondolewa
- waliomba Katibu Mkuu aondolewe-Mama Blandina Nyoni-ameondolewa
- wakaomba Waziri wa Afya aondolewe-Dr Mponda-ameodolewa
- wakaomba Naibu Waziri wa Afya aondolewe Dr Nkya-ameondolewa
Sasa serikali inavuliwa nguo, kulingana na maoni ya watu mitaani.Madaktari hawa ni kama mtoto anyedeka na hasikii la mtu.
Serikali imewachezea kete moja, imwapeleka mahakamani, mahakama ya kazi. Na mahakama imeamua kuwa kwa vile uwanja wa mazungumzo uko wazi,si ruhusa kugoma.
Mpaka naenda mitamboni nasikia madaktari wamewazungukia zaidi ya MaAdvocate saba ambao wote wamekataa kuwatetea mahakamani.
Yet macho, ukiugua leo please kimbilia kwa Toboa Tobo.