Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

si kweli kila mtumishi anastahili better pay.Madkt wakigoma wanaongezwa mshahara haraka kulingana nature ya kazi yao.Lakin je,ni sahihi serikali kuwasikiliza madaktari tu.Mwalimu mwenye Degree alipwe sawa na nesi mwenye cheti??ni sahihi

Hao waalimu wenye degree pia wanatakiwa kuwa na strategies za kudai better pay. Tatizo wanalalamika tu badala ya kutenda. Wenzao madaktari wanafanikiwa maana wanajua namna ya kuibana serikali hivyo msiwalaumu. Sihitaji kuwafindisha education degree holders namna ya kuibana serikali.
 
Ni rahisi madki kogoma kwann ni rahisi kushawishiana.hii ni sawasawa na na waathirika wa mafuriko wa Dar na Waathirika wa Moto Mbeya,wa Dar anasaidiwa haraka kutokana na media coverage kuliko wa mbeya lakin je ni sahihi???
 
Kwanini Madoctor wanakubali kazi ya kuwa madoctor? Ni upendo wao kwa binadamu wenzao ndiyo maana wamechagua hii kazi. Madoctors hawatakiwi kuwa na fikra za pesa kwanza. Madoctors wanatakiwa kuwa na Integrity ya kazi yao kwanza baadaye ndiyo maslahi yao.

Madoctors hawatakiwi kuwa na mgomo. Kwa sababu wao kama Madoctors wana jukumu kubwa la kujenga Taifa. Taifa bora linatakiwa kuwa na Raia wenye afya bora. Mchango wa Madoctor ni mkubwa- kwanini mnagoma? je mmesahahu objective yenu ya kazi hii? kama mnataka maslahi yenu, vyombo husika vipo. Kwa nini mmeamua kuwatesa binadamu wenzenu kwa kuwaacha bila ya matibabu?

Kazi ya Udoctor ni kubwa sana- hapa mmecross the line. Hii actions mlioichukua ni UNETHICAL na ni ANTI TZ. Tunakuembeni mrudi kazini, na kama kuna actions yoyote ya kisheria ya kufunguliwa kesi yoyote dhidi yenu na wagonjwa, nina issupport 100% kwa sababu mmekiuka maadili yenu.
 
uko right.... labda tujiulize, ni kwanini binadamu wengine hukiuka viapo vyao wenyewe???

Inakuaje mtoto mwema siku zote anabadilika ghafla na kuwa kitu cha ajabu??

do you see social injustice, as the cause for the "unethica" and "unpatriotic" move by doctors???
 
Mshahara wa madaktari milioni 3; polisi na intelijensia yao ya mabomu ya machozi.... laki moja! ha! ha! ha!!!!
 
Nimeamua kutounga mkono mgomo wa madaktari wa safari hii baada ya kuona ATHARI ya mgomo uliopita,pia SABABU za mgomo wa safari hii HAZINISHAWISHI mm kuunga mkono mgomo huu na NIMEGUNDUA MGOMO HUU HAUWAATHIRI HAO KINA MPONDA BALI SISI WATANZANIA WA KAWAIDA AMBAO HATUNA UWEZO WA KWENDA INDIA
Sababu ya mgomo wa mara ya kwanza ni maslahi ambayo serikali imeanza kuwaboreshea pamoja na mazingira mazuri na vitendea kazi(niliunga mkono)
LKn sababu hii ya kutaka mtu 1 ambae hana maslahi kwangu kuwepo kwake au kutokuwepo mambo yanakwenda hakunishawishi nikubali jamii iteketee mm nafurahia si kiimani wala kijamii HAIKUBALIKI.
 
Nimeamua kutounga mkono mgomo wa madaktari wa safari hii baada ya kuona ATHARI ya mgomo uliopita,pia SABABU za mgomo wa safari hii HAZINISHAWISHI mm kuunga mkono mgomo huu na NIMEGUNDUA MGOMO HUU HAUWAATHIRI HAO KINA MPONDA BALI SISI WATANZANIA WA KAWAIDA AMBAO HATUNA UWEZO WA KWENDA INDIA
Sababu ya mgomo wa mara ya kwanza ni maslahi ambayo serikali imeanza kuwaboreshea pamoja na mazingira mazuri na vitendea kazi(niliunga mkono)
LKn sababu hii ya kutaka mtu 1 ambae hana maslahi kwangu kuwepo kwake au kutokuwepo mambo yanakwenda hakunishawishi nikubali jamii iteketee mm nafurahia si kiimani wala kijamii HAIKUBALIKI.

Ndo maana wanaogoma sio wewe, wenyewe wanaogoma, hao ambao hawawataki kuwepo kwao ama kutokuwepo kuwepo kwao kwenye hizo nafasi kunawaathiri moja kwa moja; wanatetea maslahi yao, sio yako uliyevimbiwa!
 
niko pamoja na mtoa mada sidhani kama kuwafukuza mawaziri linaweza kuwa dai la msingi. walitaka maslai wamepata wafanye kazi sio kukomoana
 
Kwanini Madoctor wanakubali kazi ya kuwa madoctor? Ni upendo wao kwa binadamu wenzao ndiyo maana wamechagua hii kazi. Madoctors hawatakiwi kuwa na fikra za pesa kwanza. Madoctors wanatakiwa kuwa na Integrity ya kazi yao kwanza baadaye ndiyo maslahi yao.

Madoctors hawatakiwi kuwa na mgomo. Kwa sababu wao kama Madoctors wana jukumu kubwa la kujenga Taifa. Taifa bora linatakiwa kuwa na Raia wenye afya bora. Mchango wa Madoctor ni mkubwa- kwanini mnagoma? je mmesahahu objective yenu ya kazi hii? kama mnataka maslahi yenu, vyombo husika vipo. Kwa nini mmeamua kuwatesa binadamu wenzenu kwa kuwaacha bila ya matibabu?

Kazi ya Udoctor ni kubwa sana- hapa mmecross the line. Hii actions mlioichukua ni UNETHICAL na ni ANTI TZ. Tunakuembeni mrudi kazini, na kama kuna actions yoyote ya kisheria ya kufunguliwa kesi yoyote dhidi yenu na wagonjwa, nina issupport 100% kwa sababu mmekiuka maadili yenu.

No point at all! Usirudie kupost u.sh.u.zi kama huu in public. Daktari anapata wapi mahtaji yake? Au unafurahia sana wanapoishi in frustrated life? Unawaona wanalewa unafkiri wanapenda? They have lost hope, and now its their high time to demand change. Mliwafanya kondoo wasadaka eeeh! Eti wasitangulize hela! Kodi ya nyumba una walipia wewe? Ada za watoto wao shule unawalipia wewe? Shiiiti!
 
Mleta hoja hajui sababu za mgomo huu! Kama ningekua mwalimu nimeuliza swali,ningempatia sufuri,maana anaongelea jambo tofauti na sababu za mgomo wa sasa. Ni kielelezo cha uvivu wetu wa kutopenda kutafiti kabla ya kuandika ama kutoa majibu.
 
Mengi ya madai ya madaktari ni illusion hayawezi kutekelezeka kwa uchumi uliopo...

So kwa madai hayo na kutaka yafanyiwe kazi immediately...inabidi watafute kazi sehemu nyingine..this is free market

Kama unaona muajir wako hawezi kukutimizia maslahi yako kama upendavyo unaweza kwenda kufanya kazi kwa wahindi...au private sector au waanzishe hospitali zao walipane wenyewe kama watakavyoona inafaa..

Mapato ya madaktari ni sawa na ya mwalimu, ni sawa na ya Askari, ni sawa na ya Mkulima????

Natoa hoja.
Umefikiri kwa mafupi sana mkuu, quiters never win and winner never quit. Ila sio mbaya kuwa na mtazamo kama wako, watu wa jinsi yako wapo wengi sana mtaani, wengine wamekimbia kimbia kila wanapoona changamoto hatimaye wakakimbia hata waume zao au wake zao na kuacha familia matesoni. If u r really Great thnker you need to change ur attitude. Otherwise u will always look S.T.U.P.I.D AS UR POST.
 
Nimejaribu kukaa kimya lakini nafsi yangu inanisuta. Siwezi kuendelea kukaa kimya. My opinion is unpopular, lakini nitasema.

Nitagusa hoja moja baada ya nyingine kama zilivyotolewa na "jumuiya ya madaktari".

Kuongezwa mshahara: Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia. Ulipotokea mgogoro wa interns wa muhimbili kuhamishwa vituo, basi madaktari wakaibuka na kutaka mshahara wa 3.5 mil na kugoma. Mambo hayafanyiki hivi! Tukiwaambia madaktari waonyeshe barua waliyokwishawahi kuiandikia serikalli kuomba mshahara huo, hakuna atakayetoa barua au ushahidi wowote kwa sababu madaktari wameanza na mgomo moja kwa moja. Siungi mkono mgomo wa namna hii.

Madaktari kupewa nyumba: Mara nyingi adui wa daktari huwa daktari mwenzake. Hili swala la nyumba lilishajadiliwa huko nyuma. Nini kilitokea? Baada ya madaktari wa muhimbili kuthibitishiwwa kuwa wao watalipwa sh laki 4 kila mwezi basi chama cha madaktari ambacho viongozi wake wengi ni madaktari wa muhimbili wakapoteza interest ya kubargain na serikali ili posho hiyo wapate madaktari wa nchi nzima. Chama hicho kilikataa kabisa mara kadhaa kuitisha vikao vya kujadili posho za nyumba huku wakitoa sababu za kuepusha migomo. Sasa hivi inakuja "jumuiya ya madaktari" na kuilazimisha serikali kutoa posho hizo with immediate effect. Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba? Standing orders za mwaka 1994 zinaeleza kinaga ubaga kuwa daktari anastahili kupewa nyumba, standing orders za mwaka 2009 hazimtaji daktari katika watumishi wanaostahili kupewa nyumba. Maafisa utumishi wote wanatafsiri kuwa standing orders za mwaka 2009 zimemtoa daktari kwenye kundi la watakaopewa nyumba. Ni lini madaktari walienda kujadili hili na wizara ya utumishi? je ni sahihi kuanza na mgomo? Ili madaktari warudishiwe stahili hiyo ni LAZIMA kifungu kwenye standing orders za mwaka 2009 kifanyiwe marekebisho. Je, hilo linaweza kufanyika with immediate effect? Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.

Call allowance: "Jumuiya ya madaktari" inataka call allowance ilipwe kwa half per diem. This is very simple! Kwa nini mnagoma kwenda kazini during working hours? Ni kweli kuwa daktari anastahili kulipwa angalau sh. elfu 40 kwa call lakini solution yake ni rahisi kuliko zote. Madaktari waingie kazini, muda wa kazi ukiisha madaktari warudi nyumbani kama watumishi wengine. Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense. lakini again, jitihada gani zimefanyika awali kuhakikisha call inaongezwa? Can doctors provide evidence of their effeorts? HAKUNA.

Mazingira duni ya kazi: Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari. Hili swala waachieni wananchi wenyewe. Daktari unachotakiwa kujua ni capacity ya hospitali yako, beyond that usipokee mgonjwa. Ukishampokea basi unalea ubovu. MV Bukoba, MV spice zilizama kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake. MV Muhimbili nayo inaingia kwenye hili kundi. Nani alaumiwe? Nahodha lazima awe miongoni mwa watu wa kulaumiwa. Kama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini. hata Ulaya wangekubali kupokea wagonjwa wengi kulikoi uwezo kungekuwa na wagonjwa wanaolala chini. Ila Ulaya swala hilo halipo. Nafasi zikijaa zimejaa, mgonjwa apelekwe wapi, sio swala la daktari. Hata hiyo hospitali unayofanya kazi hujaijenga wewe daktari, ilijengwa kwa sababu mahitaji yalikuwepo. Ukiendelea kupokea wagonjwa wengi kuliko uwezo unaonyesha kuwa mahitaji sio urgent. Wagonjwa wakikosa pa kulazwa ndipo wananchi watashinikiza viongozi wao wawahakikshie facilities za kutosha.

Interns kuhamishiwa hospitali nyingine: Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern. Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.

Huduma huuzwa na kununuliwa. Bei ya huduma uamuliwa na nguvu za mahitaji na upatikanaji wa huduma. Hakuna daktari aliyelazimishwa kufanya kazi serikali. Kwanini madaktari wanakimbilia kufanya kazi serikalini? Madaktari wawe wakweli na watuambie faida zilizopo serikalini. kwanini madaktari wasitoe notice ya kuacha kazi serikali na kwenda kufanya kazi sehemu bora zaidi. Tanzania kuna soko huria. Kama watu walitumia mamilioni kwenda Loliondo basi hata daktari wanayeamini huduma zake watamfuata popote alipo. Madaktari mnangoja nini kutambua hili?

Mwisho: Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa. Ewe daktari, jiulize ni mara ngapi umeingia kazini kwa muda unaostahili na ukafanya kazi mpaka muda wa kazi kuisha? Je, tabia yako ya kila siku kazini inachangia kuondoa umasikini wa nchi yetu? Kila mtu aweke jibu lake moyoni na kujiuliza tena, je mgomo unaoendelea hivi sasa unapaswa kuungwa mkono? Je, kwa siku hizi mlizogoma mshahara mnauchukua wote bila aibu?

Also: Am just curious, nani analipia gharama za kukodi ukumbi wa mikutano wa Starlight Hotel ambao madaktari wamekuwa wakikutania kwa siku kadhaa?!

Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Big up mdau, in simple terms Madaktari ni Terrorists mimi binafsi nawalaani sanaa, wanaokufa sio PM wala waziri wao wala katibu mkuu, kwanini wawaadhibu wasio na hatia??? Wananchi wamewakosea nn madaktari?? In other words maslahi yao ni bora kuliko uhai wa mtanzania, shame on them!!
 
1. Madai ya madaktari yote kuanzia la mshahara, posho za nyumba pamoja na posho za overtime/call allowance yanatakiwa kutatuliwa na wizara ya utumishi. Hayo ni maswala ya kiutumishi zaidi na yanafafanuliwa kwenye standng orders za public servants.

2. Madaktari wengi mwajiri wao siyo wizara ya afya. Wengi wamejiriwa na halmashauri, mikoa - chini ya TAMISEMI, wizara nyingine pamoja na mashirika ya umma. Kuna wachache walioajiriwa na wizara ya afya hawafiki asilimia 20 ya madaktari wote walioajiriwa na serikali.

Swali. Je, swala la madaktari kuconcentrate zaidi na wizara ya afya badala ya wizara husika ya utumishi wakati wanapodai maslahi yao kunaonyesha jinsi wataalam hawa wasivyo na ujuzi wa nini wanastahili kufanya juu ya swala hili?

Swali. Je, waziri wa afya anaweza kubadili waraka wa utumishi?

Swali. Je, waziri wa afya anaweza kuongeza mshahara wa daktari?

Swali. Madai ya madaktari yalikuwa nane (8) sasa wameanza kufragment madai yao into pieces. Je, tujiandae na migomo nane mwaka huu iwapo madai hayo hayatatimizwa kama wataalam hawa wa tiba wanavyotaka.
 
Ze Marcopolo,

Nakuunga mkono kabisa na kuna jamaa mmoja nilikuwa nakunywa nae pale Sea cliff nikamchanganulia madai yao na kwanini sioni sense yeyote na wao kugoma. Aliishia kudai eti anagoma kwa kuwa hawaheshimiki sasa kama sio uchizi huo ni nini??? This is schizophrenic illusion kujiona wewe ni muhimu sana sehemu kuliko wenzio. Siwaungi mkono maana ni sawa tu mafisadi wengine nchini. Wakaombe kazi nchi nyengine au kwengine waje wenye kuridhia hiyo mishahara it is a freemarket bwana!!!!
 
Zemarcopolo & co, nyie ni watumish wa idara ya propaganda ya ccm? Tunajua nape ana vijana wake kwenye mitandao ya kijamii, tatizo ni kwamba propaganda zenu ni za uongo hivyo zitashindwa daima!
 
Naunga mkono juhudi za mtu yoyote yule kudai haki zake. Madaktari wamenyimwa haki zao kwa muda mrefu na wamekuwa wakionewa, wakinyanyaswa na kudhalilishwa na serikali kila mara wanapojaribu kudai haki hizo. Suala la wagonjwa kufa halipendezi wala halikubaliki. Lakini je ni kweli kwamba ni madaktari pekee ndio wenye wajibu wa kuhakikisha kuwa wagonjwa hawafi wanapofika hospitalini? Kila mtu akitimiza wajibu wake hakuna mgonjwa atakayekufa kwa magonjwa yanayotibika nchi hii.

Unaunga mkono madaktari kumnyang'anya mwananchi wa kawaida haki yake ya kuishi?
 
Mimi sikuunga mkono mgomo wa kwanza wa madaktari na de facto na huu wa pili sikuunga mkono. Ila kuna kitu kimenishangaza zaidi kwenye huu mgomo wa pili: hivi nani aliwashauri madaktari wampe ultimatum mtu ambaye hawajawahi kukaa naye mezani kwenye majadiliano (Rais)? Logically ilitegemewa madaktari kwanza wangeomba kukutana na Rais wamweleza kumkataa kwao waziri na naibu wake face to face, then kutokana na responce yake ndio wangekuja na reaction. Sasa wao wamereact mahali ambapo hakukuwa na action! Utampaje Rais taarifa ya kutaka atengue uteuzi wake kwa kupitia vyombo vya habari? Je, viongozi wa mgomo walimuandikia Rais barua ya kumtaka awafukuze kazi mawaziri? Rais hafanyi kazi kwa kutumia vyombo vya habari. Mimi nadhani madaktari wakubali tu kuwa hawakupata ushauri unaotosheleza kujenga hoja madhubuti na kwamba utatuzi wa kweli utapatikana iwapo watajikaza "kiume" na kufuatilia madai yao hatua kwa hatua, haya mambo ya ultimatum no no no...
 
Back
Top Bottom