Sitti Mtemvu kuzindua Kitabu cha 'Chozi la Sitti'

Sitti Mtemvu kuzindua Kitabu cha 'Chozi la Sitti'

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Taarifa ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, kwa vyombo vya habari leo imeeleza kuwa, Sitti atazindua kitabu kinachoelezea faida na hasara ya mitandao ya kijamii.

Amesema pamoja na kwamba mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri, huleta mapinduzi ya kimaendeleo ya kihabari kwa haraka.

Amesema maudhui yaliyopo katika kitabu hicho ni yanamlenga yeye moja kwa moja kama mhusika na kwamba pamoja na maumivu na athari azipatazo mhusika kitaelezea ni kwa jinsi gani ataweza kujifunza na kunyanyuka upya.

Mei 2, 2015 mwaka huu pia uzinduzi wa kitabu hicho utaenda sambamba na uzinduzi wa 'Taasisi ya Sitti Tanzania' yenye lengo la kusaidia watu wenye shida na kuweza kuendeleza gurudumu la maendeleo Tanzania.

Itakumbukwa sakata la Sitti kudaiwa kuwa ameghushi cheti cha kuzaliwa liliibuka kwenye kwa kasi mwaka jana kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyozifanya mamlaka husika kuanza kufuatilia uhalali wa cheti chake cha kuzaliwa....hadi pale alipojivua taji alilokuwa amevishwa baada ya kushinikizwa na watu mbalimbali kuwa aachie taji hilo kwa kile kilichoitwa ni kukosa uaminifu na kukosa sifa ya kushikilia nafasi hiyo.

=========

Sitti Mtemvu kuzindua Taasisi, Kitabu na Kipindi chake cha TV May 2

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2014 na baadaye kulivua taji lake, Sitti Mtemvu, anatarajia kuzindua taasisi yake ya ‘Sitti Tanzania', kitabu chake na kipindi cha TV kiitwacho ‘Chozi la Sitti.'

11084851_847979435267838_654524946_n.jpg


Uzinduzi huo utafanyika May 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City na utapambwa na burudani kutoka kwa Yamoto Band.

Chanzo
: Bongo5
 
Aliyekuwa miss Tanzania na kuvuliwa taji sitti mtemvu ametoa kitabu kinachoitwa "chozi la sitti" kinachohusu matumizi mabaya ya mitandao
Source Chanel ten
 
Aliyekuwa miss Tanzania na kuvuliwa taji sitti mtemvu ametoa kitabu kinachoitwa "chozi la sitti" kinachohusu matumizi mabaya ya mitandao
Source Chanel ten

Huyo mpuuzi na mwongo hatusomi maana atatudanganya tu
 
hao mamiss wazee kama vip mwaka kesho namleta bibi yangu agombee
 
Kitakuwa na maana kama hukudanganya umri. Kwa ufupi we mwizi
 
hao mamiss wazee kama vip mwaka kesho namleta bibi yangu agombee

Si heri bibi yako tutakuwa tunajua umri wake kuliko yeye aliyeamua kudanganya umri wake eti kisa tu aupaishe ule mfuko wa baba yake wa kuwapeleka mahouse girl uarabuni wa MTEMVU FOUNDATION
 
Atakinunua na kukisoma yeye na familia yake...habari ndio hiyo!
 
anataka kupiga mpunga tu kupitia mauzo ya kitabu na hiyo entrance collection...
 
Back
Top Bottom