Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

hapo pigia msitari, Makonda katumwa na Sitta na Membe kwa jeuri ya kikwete waliokuwa ukumbini jana walitakiwa kumrestisha Makonda iwe fundisho kwa kibaka mwingine kujaribu...

Mtu ambae ni muina mishwa anaweza kumrestisha mtu ?
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
Unajua zamani nilikuwa nadhani Mzee Sitta ana busara sana na mpaka nilisikitika sana alipotemwa kwenye uspika asigombee mara ya pili. Lakini tangu alivyovurunda kwenye Bunge Maalum la Katiba na KAMA NI KWELI katamka hayo, basi uzee unamwijia vibaya. Na maneno hayo ni kukosa hekima na busara na kuhamasisha vurugu maana kesho na kesho kutwa upande unaoshabikia Katiba Iliyopendekezwa ikiwa na mkutano, watu wasioitaka waanzishe vurugu. Huu ni upumbavu uliopitiliza!!!!!
 
Sitta anajidanganya,anadhani wananchi ni mambumbu kama yeye alivyombumbu,waliofanya vurugu si wananchi,ni wanachama wa ccm wachumia tumbo wakiongozwa na Makonda,anaposema eti wananchi wengi wanaunga mikono hiyo katiba haram ni uongo,hajui tu,aingie mtaani ajionee,siyo akae tu ofisini.Na kwakuwa ameunga mkono hizo vurugu,basi yeye ndiye mfadhili.

Subiri, hii ndio kauli utakayosikia kutoka kwa mwenyekiti wa ccm, katibu, katibu mwenezi na magambaz yote. Hawana aibu, wameishajitoa ufahamu tokea walipochakachua maoni ya wananchi na kulazimisha kura ya kupitisha hiyo ilani yao ya uchaguzi kwa kuivika koti la katibainayopendekezwa. Inatisha sana wanakotupeleka. Yaani mzee kama Sitta badala ya kulaani kitendo kama hicho, bila aibu anasema Warioba amejitakia mwenyewe!!!!!????
 
Kama Sita anaona katiba pendekezwa inaungwa mkono, kwa nini hataki watu waijadili? Hii ni uthibitisho tosha kwamba katiba pendekezwa ina masuala mengi maovu ambayo yakijulikana basi katiba hii haitapita.

Kwa mtazamo huu, hapa tunajiridhisha juu ya nia ovu ya sita et al kwa watanzania na nia ya kuhakikisha wananchi wanabaki wajinga ili wauziwe mbuzi kwenye gunia.

Sita kama ana akili timamu, hawezi kusema wananchi wapige kura bila kuelewa wanapigia kura vitu gani. Sita na team yake ni wendawazimu tena wapelekwe mirembe haraka iwezekanavyo.

Kwa statement hii sita amethibitisha ushiriki wake ama wa moja kwa moja ama kupitia chama chake katika maandalizi na utekelezaji wa mbinu za uvunjifu wa amani pale wananchi wanapoelekea kufunguliwa macho.

Sasa sita, kwa kuwa anaamini kwamba watanzania wa sasa hawadanganywi na kwamba wakidanganywa watamvamia palepale, naona ni endorsement nyingine ya kuondoa utawala wa sheria katika nchi hii.

Na kama ndivyo, Sita atoke nje afanye mkutano wa hadhara ama aitishe mdahalo kunena mazuri ya takataka lao wanaoliita katiba. Hapo ndipo atajua chanzo cha dead sea.

P.baffu sana.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
 
Laana gani ya viongozi wa dini hivi viongozi wa dini wakizungumzia suala la kisiasa linatokana na maandiko matakatifu? Wewe ndio uliochanganyikiwa kwa maana hujui yapi ya mungu na yapi ya kidunia.tena unatisha kwa sababu kiongozi wa dini anaweza kutembea na mkeo ukaogopa kumkemea kwa sababu unaogopa laana hahahahaha

Nitajie Nabii ambaye hakukemea maovu ya watawala.
Hivi viongozi wa dini kukemea udhalimu, rushwa, ufisadi na wizi unaofanywa na wanasiasa na watawala ni kujiingiza ktk siasa? Jitafakari!!
 
Sitta,ndo tukupe uraisi wa nchi hii? Angekuwa ni mtu mwenye busara angekemea vikari kitendo hicho. Mzee Warioba ni ni mwananchi wa Tanzania na anao uhuru wa kuongelea katiba sawa na makada wengine wa CCM wanavyoipigia debe katiba yao oendekezwa! Wasira, JK na makada wote wanaipigia debe,mbona hawahafanyiwa fujo!? Anajidanganya upuuzi wao wa katiba unakubarika kwa wananchi!? Hivi ni nchi gani waliingia mchakato wa katiba na viongozi wakasaini katiba hiyo huku wakikata mauno km hapa kwetu!? Walikata mauno vile walijua katiba imewapendelea wao! Ingelalia upande wa mwananchi wasingekata mauno.
Sitta uache ulaghai,waacheni waliokusanya maoni yetu watuambie walichokusanya na kisha tupime!
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.

Samuel Sitta ni mwanasiasa wa maji taka. Hana moral authority ya kumshauri hata mwendawazimu
Siku zote nimempinga EL lakini kwa sasa kati ya wawili hao the lesser evil ni EL
 
Sitta mnafiki sana. Ni lazima watanzania wamwogope kama Ukoma. Huyi ni mzee mlevi kifikra.
 
Samuel Sitta ni mwanasiasa wa maji taka. Hana moral authority ya kumshauri hata mwendawazimu
Siku zote nimempinga EL lakini kwa sasa kati ya wawili hao the lesser evil ni EL
Umenikumbusha mawazo ya Mwampembwa (GADO) akilinganisha Al-Assad na ISIS ambapo USA inalazimika kuungana na Irani kumuondoa a greater evil!

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.

Sitta hawezi kujibu hilo swali tumezoea mtu akinyamaza kimya anapoulizwa maana yake ni YES, Hakuna shaka yeye ndiye amegaramia lile vurugu la jana na sasa atakuwa anajisumbua Wananchi tupo tayari kwa mapambano.
 
Sita amekiu CCM wamemteka ili wananchi tuendelee kuwa madikini hatufai kazarau misingi yote ya kusimamia haki za umma.Katukana ukristo na maaskofu asikanyage uraiani
 
sijamwelewa Sitta, ina maana tukimpiga yeye ndiyo atajua kuwa hatutaki ushenzi wake wa kuiua Tanganyika?
 
Nlkuwa namweshimu sana Sitta lkn kwa sasa duuuuuu,sidhan kama ametumia akili kujibu hili. Ameshavurugwa huyu c bure
 
"Mwenye kilanga haliliwi wala halaliwi tanga" Amejitakia mwenyewe
 
Kwa hiyo amebariki ule uhuni uliofanyika pale ubungo! Ngoja yeye atandikwe siku yake, sijui atakimbilia wapi!!
 
sita anaona ni vizuri mtu kuvamiwa jukwaani kwa kuwa anapendekeza kura ya hapana je?itakuwaje pale watakaokuja kupendekeza kura ya ndio kama Kikwete alivoagiza wajumbe wa katiba kuwaeleza wananchi uzuri wa katiba pendekezwa na wapige kura ya ndio?
 
Hapo kuna mambo haya nikichambua.

Kwanza ni vijana wanahusika katika tuhuma.

Pili ni wasomi tena wa chuo kikuu.

Tatu wanapinga mawazo ya mtu ambaye kimuonekana na umri ni mzee ila anafikiri na kuwajibika kama kijana.

Nne hata kwenye jambo la msingi kama katiba unakubali kununuliwa na kujazwa ujinga.

Tano wameamua vurugu kwanza badala ya kujenga hoja na kuweka vurugu ya fikra ili kusumbua akili.

Sita wamepinga katiba na kuzuia mawazo ya watu wengine kusikika na kujadiliwa.

Mwisho ni muda uliotumika vibaya hauwezi kurudishwa tena maana wakati ni mali.

Mwisho kabisa, hili tulitazame katika uwezo wetu wa kujadili mambo, kuvumilia wengine, kushindwa kuwa na ustarabu katika mambo muhimu na mwisho tufikiri kuhusu vijana wetu.

Historia imeandikwa.
📝📝📝📝
 
Back
Top Bottom