Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Unajuwa mungu anapokuwa anataka kuuwa au kuupunguza nguvu utawala filani anautia upofu nakuto kusikia ccm nawakina sitta makonda mtoto asiye riziki huyu laana ijuu yao naniwaambie wafanye wafanyavyo kwauchachuwaji huu ndio mwisho wamaccm navibaraka vyao mungu mpeujasili mzee walioba na wenzake wote
 
hila za ccm zinaanza kufika mwisho,kama sita anasema wanaosema hapana wapigwe wakati huo huo je itakuwaje kwa wale watakaokuja kusema ndio kama Kikwete alivyowatuma wabunge wa katiba wakawaelimishe wananchi uzuri wa katiba inayopendekezwa na kuipigia ndio?
 
Bora hiki chama kiitwe Chama Cha Majambazi!
Nafikiri jina hilo litakuwa linasadifu vilivyo matendo yake!!!
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.

Tatizo kubwa linalowasumbua viongozi wetu wa CCM ni kwamba wanajisahau Tanzania ya sasa sio ya jana wala juzi na watu tayari walishapona ule upofu CCM waliowapiga kwa zaidi ya miaka hamsini. ila wasichokijua ni kwamba kwa vitendo wanavyovifanya sasa wanazidi kufupisha zaidi siku zao za kuendelea kuwepo....Kile kitendo kilichofanyika ubungo plaza jana ndicho hicho hicho kilifanyika Ukumbi wa Nkuruma UDSM siku chache zilizopita na kwenye midahalo hii hii na waandaaji wa vurugu zile walivyo na akili ndogo wanashindwa hata kutengeneza mazingira angalau yawe tofauti kidogo!!!! Mi naamini kwa mipango na mikakati ya namna hii basi CCM hatunayo tena!!!!CCM now is DEAD!!!!!!Mi hapa namuaonea huruma tu Prof wetu Kikwete kwa kukubali chama kufia mikononi mwake....na hili lilishaonekana tangu day one 2005 wakati anaingia madarakani maana hajawahi kuwa na mipango endelevu ya kuimarisha chama zaidi ya kutumia ujanja ujanja tu of which haya ndio matokeo yake lichama linajifia natural death
 
Huyu Sitta anaitetea katiba aliyotunga mwenyewe, akaipigia kura mwenyewe, akahesabu kura mwenyewe, akajipongeza mwenyewe, akajitekenya mwenyewe, akacheka mwenyewe na akaserebuka mwenyewe kwenye ukumbi wa bunge kwa hiyo hana hekima.
 
samwel sitta amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa kuaminiwa na umma kwa nafasi yoyote na huu ndo mwaka wake wa mwisho kuwa kiongozi wa umma. Nina uhakika hata akigombea ubunge Paul Andrew Maganga atamshinda mapema asubuhi na akigombea uraisi kura za maoni hazitafika hata 30.
Ile laana ya watumishi wa Mungu imemmaliza ameungana na wahuni kina paul makonda na kuanzia sasa ntakuwa naandika jina lake kwa herufi ndogo


Muacheni wa mtumie Alafu watamuacha tu.... Hajajifunza Kwanini walimtoa usipika wa bunge? Amesahau haraka hivyo na wakati alikua anakuja ktk Vyombo vya Habari na kulia lia kutokana na mtandao wa Rostam na Mzee mamvi ulivyokua Unamdhibiti?
 
Sitta apangiwe Zanzibar aende kuipigia kampeni rasimu ya katiba kabla ya kupigiwa kura.
 
Mimi huyu mzee nilimfuta akilini mwangu alipojenga ofisi ya spika kwa sh 400 milioni jimboni kwake huku zahanati zilizokaribu na ofisi yake hazina dawa na shule hazina madawati. Madaraka hulevya, akina Sitta wameshalewa, ipo siku pombe itawaisha na siyo mbali.
 
warioba na watanzania wengine wanayo haki ya kujadili katiba mpya inayopendekezwa, ili kuwapa watu fursa ya kuielewa vizuri kabla ya kuipigia kura ya ndio au hapana. katika nchi ya kidemokrasia kama Tanzania kuvumiliana ni jambo muhimu na si la kupuuzwa kama ilivyo tokea hapo jana. tujitafakari na tujikosoe, na tuache ushabiki maana huo utatufikisha pabaya. wasomi tunayonafasi ya kuliweka sawa swala hili la katiba kwa kutoa hoja zenye mashiko na si mangumi na kurushiana viti.
 
huyo konda wenu asije huku kanda ziwa siku akitia mguu lazima tumchape bakola sana kisha tumule kiboga hana adabu hata mzee wake anaweza kumzalilisha
 
Hana hata aibu huyu Sitta ya kumkana Warioba??? Kwa kwetu tunakoelekea ni kwamba tutarajie wafungwa wengi sana!
 
"ccm bila vyombo vya dola ni
weupe kama karatasi",Dr Slaa
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.

Kuna watu wanatia hasira sana. Sitta ni mzee kama baba angu mambo anayoyafanya hayaendani na umri wake. Uthibitisho wa kundi kutumwa upo na pia mimi nimetoa ushahidi wenye ukweli ndani yake 100%. Sasa huyu anachokisema ni kweli anajiua kilichotokea na mipango yote au anajitoa ufahamu tu
 
Kilichomkuta jana Warioba ni msiba wa kujitakia

Warioba kufanyiwa fujo na CCM amejitakia? Naomba nikuulize kitu kimoja? Kama katiba ni haki yetu wote, Mjadala wakatiba una hathari gani? Kama mwisho wa siku kura zitahitajika, na waliokuwa bungeni wameridhika kuwa ni katiba nzuri kuna tatizo lolote kuijadili?
 
Kuna siri gani hawataki midahalo. Wananchi wananataka kujua

Kaka hawana hoja ndo maana hawataki ksbisa kusikia kitu mdaharo kumbuka 2010 tiddo muhando pale TBC alianzisha midahoro majimboni mbona walijitoa nakumuondoa kabisa tiddo muhando TBC wanaumbuka vibaya mno sasa ndo hayo katiba bila midaharo ni katiba gani hiyo? Hii kura ya maoni tuungane tunaotakia mema nchi hii isipigwe kabisa hakuna katiba inayoandikwa bila maridhiano
 
Hiyo ni kauli ya msaka urais. Kauli isiyokuwa na akili wala mantiki. Sitta ana mtindio wa akili
 
Back
Top Bottom