Sitta: Tuheshimu maamuzi ya Mahakama (Igunga) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Tuheshimu maamuzi ya Mahakama (Igunga)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Aug 23, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Akizungumza jana mjini Tabora, Sitta alisema kuwa mahakama ina mamlaka yake kisheria, hivyo wana CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani imefanya kazi yake inavyotakiwa.

  chanzo;pamoja dot com
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikitangaza kusudio lake la kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, iliyotengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalali Kafumu, wadau mbalimbali wameipongeza hukumu hiyo wakiita ni darasa tosha kwa demokrasia ya mfumo wa vyama vingi.


  Miongoni mwa waliosifu hukumu hiyo ni pamoja na Spika mstaafu, ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema kuwa maamuzi hayo inafaa yaheshimiwe. Akizungumza jana mjini Tabora, Sitta alisema kuwa mahakama ina mamlaka yake kisheria, hivyo wana CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani imefanya kazi yake inavyotakiwa.


  "Kama kuna mtu anaona hukumu hiyo haikutenda haki, anaweza kwenda mahakamani kukata rufaa, lakini mimi nashauri ni vema tujipange upya tuingie ulingoni. "Hapa mimi sina maoni juu ya jambo hilo, bali cha msingi ni vema tukakaa na kutafakari yaliyotokea huko Igunga, ili basi tukiona inafaa kukata rufaa sawa, na kama tuingie ulingoni, yote ni sawa," alisisitiza Sitta.


  Katika hukumu yake juzi, Jaji Mary Nsimbo Shangali, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA, Joseph Kashindye, alisema kuwa alipokea malalamiko 15 ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili, lakini yakaongezwa madai mengine mawili na kufikia 17.


  Mbali na Dk. Kafumu, washitakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Msimamizi wa uchaguzi jimboni humo, Protace Magayane na kwamba mahakama hiyo ilithibitisha madai saba ya kutengua matokeo hayo. Hata hivyo, wakati Sitta akiwa na mtazamo huo, CCM kupitia kwa Katibu wake wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilieleza kutoridhishwa na hukumu hiyo, hivyo kuamua kukata rufaa.


  Pamoja na CCM kuchukua hatua hiyo, wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa na wanaharakati waliliambia Tanzania Daima kuwa, hukumu hiyo ni darasa tosha la demokrasia linaloonesha jinsi sheria za uchaguzi zinavyovunjwa. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashir Ali, alisema hukumu hizo za uchaguzi ikiwamo hiyo ya Igunga, zina maana sana kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa, wanasiasa na wananchi.


  "Tatizo letu huwa hatusomi hukumu hizi kwa undani, kwani tungekwishajua kuwa ni darasa tosha la demokrasia. Suala la takrima lilikuwa halieleweki kama ni rushwa, ushindani wetu wa kisiasa si wa kuvumiliana, una matumizi makubwa ya fedha, mali za serikali na madaraka kwenye kampeni," alisema. Ali alifafanua kuwa hukumu hiyo imetoa mwanga kuwa, kama hakuna chombo huru cha kusimamia sheria zinazokiukwa ni sawa na bure, akitolea mfano Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa licha ya kuwapo wakati wa mchakato huo, vilishindwa kuchukua hatua.


  "Kuna mjadala kuhusu uwepo wa sheria ya Tume ya Uchaguzi, maana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hakuna sheria ya Tume ya Uchaguzi, badala yake chombo hiki kinatambuliwa na sheria za uchaguzi, jambo linalotoa mwanya kwa mapungufu yanayojitokeza sasa," alisema. Kuhusu uwajibikaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa uchaguzi huo mdogo, Ali alisema kuwa mpaka sasa umuhimu wa ofisi hiyo hauonekani maana kama hoja ni kusajili vyama, kazi hiyo inaweza kufanywa hata mahakamani.


  Alibainisha kuwa, kwa sasa ofisi ya msajili na Tume ya Uchaguzi ni kama idara tu ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo wananchi wanapaswa kutumia hukumu ya Igunga kama tathmini wakati huu wa mchakato wa katiba mpya kusahihisha makosa ya kuvifanya vyombo hivyo huru. Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Mtatiro Julius, alisema hukumu hiyo itawafungua wananchi kuona umuhimu wa kubadilisha mfumo wa uchaguzi ili kuepusha taifa kuingia gharama zisizokuwa za lazima pale kiongozi anapokufa ama kuenguliwa.


  "Hii naiona kama hatufikirii sawa sawa, maana matumizi ya mabilioni ya fedha kwenye uchaguzi yalikuwa kwa vyama vyote kule Igunga hasa CCM, CHADEMA na CUF. Lakini hili linaweza kuepukwa mana kama upuuzi unafanywa na watu wawili, hatuna sababu ya kulisababishia taifa hasara," alisema. Kwa mujibu wa Mtatiro, inapotokea hali kama hiyo ya mbunge kuenguliwa au kupoteza maisha, mshindi wa pili kutoka chama kingine ndiye achukue nafasi badala ya kurudia uchaguzi. "Igunga tuliona Dk. Kafumu walipishana kidogo na Kashindye wa CHADEMA, hivyo kwa vile huyu alikiuka taratibu, basi mshindi wa pili apewe nafasi kuliko kurudia uchaguzi, kwani kufanya hivyo kunaweza kukipa chama kilichoenguliwa ushindi tena wa mtu asiyefaa," alisema Mtatiro.


  Mwanasiasa huyo pia hakusita kuinyoshea kidole Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema kuwa, John Tendwa (msajili) ameonesha wazi ni wakala wa CCM anayefanya mbinu za kukisaidia chama hicho kishinde badala ya kusimamia kanuni na sheria. Mtatiro aliweka bayana kuwa makosa yaliyoainishwa kwenye hukumu iliyomtia hatiani Dk. Kafumu na kumnyang'anya ubunge wake, yalilalamikiwa mapema na wapinzani kwa Msajili wa Vyama wakati wa kampeni, lakini hakuchukua hatua yoyote. "Msajili wa vyama hana meno, na huyu amekuwa na kashfa ya kusajili hata vyama visivyo na sifa ilimradi tu aweze kuvidhoofisha vyama makini vya upinzani. Hata kwenye uchaguzi ameonesha wazi anataka CCM ishinde," alisema.


  Mtatiro aliongeza kuwa, umefika wakati nafasi hizo nyeti za vyombo kama Tume ya Uchaguzi, Msajili na nyinginezo zitangazwe ili watu wenye taaluma zao washindanishwe na kuchujwa na chombo maalumu badala ya kuteuliwa na rais.


  Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya, alizungumzia hukumu hiyo ya Igunga akisema imetoa tafsiri mpya kwa wananchi kuelewa demokrasia ya vyama vingi na namna ya kumpata mwakilishi makini bila rushwa na vitisho. "Hili litakuwa fundisho kwa wanasiasa wanaochezea fedha nyingi kwenye uchaguzi kununua watu, maana watatambua sasa kuwa kufanya hivyo kutawapotezea viti vyao. Lakini na wagombea wanapaswa kuwa makini na wapiga debe na vyama vyao, kwani wanaweza kuingizwa mtegoni kama alivyoponzwa Dk. Kafumu," alisema.


  Akisoma hoja zilizothibitishwa na mahakama hiyo juzi, Jaji Shangali alisema ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kutumia nafasi yake ya uwaziri kutoa ahadi ya ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni moja ya kero kubwa kwa wananchi wa Igunga.Waziri Magufuli akiwa katika uchaguzi mdogo huo katika moja ya kampeni, alitumia nafasi ya uwaziri kuwatisha wapiga kura wa jimbo hilo kuwa kama hawatamchagua mgombea wa CCM watawekwa ndani.


  Jaji Shangali pia alisema kuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage, alipita mitaani akitangazia wananchi kuwa mgombea wa CHADEMA amejitoa. Katika hoja nyingine ni kwamba Imamu Swalekh Mohamed wa Mskiti wa Ijumaa Igunga, aliwatangazia waumini wa Kiislamu kuwa wasiichague CHADEMA kwa kuwa baadhi ya viongozi wake walimdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario.


  Nayo matamshi ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kudai kuwa CHADEMA imeleta makomandoo kuuvuruga uchaguzi huo ni mojawapo ya hoja ambazo mahakama hiyo ilizikubali. Katika hoja kuu ya mahindi, Jaji Shangali alihoji kama wananchi wa Igunga walikuwa na njaa sana. Na kwamba, kama jibu ni ndiyo, ni kwanini uchaguzi usifanyike wakati hawana njaa.

  Source: ***************
   
 3. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  hicho kinyundo na kijembe chenu hatutaki kuvisikia tena!
   
 4. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  imekaa vyema mno...wakome!
   
 5. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,933
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Huyu Jaji mhhhhhhhhhh, sijui kama atachukua round tusubiri tuone mana Dalali wa Madini (Kamishina wa MADINI) KAFUMUA migodi ya MADINI yetu na sa naye KAFUMULIWA na Mahakama, Je wadau wake wa wizi wa madini (madalali wenzie) watakubali?
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  sitta yumo kwenye hilo chama mda mrefu,anajua wapi wameiba kura wapi wameshinda kihalali..wamsikilize huyo comrade wao
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Six six six .....anaangali vizuri upepo wa m4c. Tumkaribishe cdm tumwahidi uspika...tehe tehe te teeeee
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Demokrasia ina gharama zake. Wacha chaguzi zirudiwe ili vyama vipate nafasi ya kujijenga. Nafahamu kuna vyama ambavyo havina tena uwezo wa kusimama majukwaani kwani hawana cha kuwaambia wananchi. Kama ni kuepuka gharama, zipo sehemu nyingi za kuangalia. Tunayalipa makampuni yanayoiuzia umeme TANESCO billions of shillings unnecessarily. Tuanzie huko.
   
 9. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Hukumu hii ni fundisho tosha kwa demokrasia
   
 10. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  CDM ikianza kukaribisha mafisadi hawa kina Sitta itakuwa inajichimbia kaburi. Muulize Dr Slaa akueleze Sitta alivyofuja fedha ya serikali kujenga ofisi yake Urambo. Tofauti yao huko CCM ni nani kachukua kiasi gani, lakini kimsingi wote ni majambazi ndiyo maana wanavumiliana. Subiri tuwang'oe ndiyo utawafahamu vema.
   
 11. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SITTA ni miongoni mwa watu wachache sana siku hizi wanao waza na kutumia elimu zao kwa faida ya NCHI HII.Wengine hat penye ukweli watang'ang'ania kukata rufaa hata bila kutafakari wapi walikosea.HONGERA MHESHIMIWA WA KIUKWELI.
   
 12. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Katika jambo ambalo CCM wanapaswa kuwa makini sana, ni kukata rufaa. Wao kama chama tawala wanapaswa wawe wa kwanza kuamini utendaji kazi wa mahakama zao. Sasa kama wao watasema hawana imani na mahakama, je sisi wengine tutaziamini hizo mahakama?
   
 13. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tuwekeeni basi hiyo hukumu hapa!
   
 14. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapana! Hukumu hiyo ingekuwa ya haki tu kama ccm wangeshinda! Sasa kwenda mahakamani ni muhali kwa kukata rufaa ili kama kuadhirika zaidi iwe mbele kwa mbele. Pesa ipo wala sio issue hapa. CCM kiboko yao. Atawekwa Jaji anayejua fadhila za CCM kama wa Arusha na Ukonga. Sio lazima 6 iwe 6 siku zote, inaweza kuwa 9 ikifanyiwa utaratibu mzuri. Songa mbele CCM kata rufaa, hakuna kukubali kirahisi hapa, huo ndio udume.
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani ccm wanatapatapa tu hakuna jipya hapo
   
 16. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu sitta anaelewa kilichotokea. Lakini Nape ameona aibu na sasa ameshinikiza kukata rufaaa. Acha wapoteze muda wao mkuu.
   
 17. j

  jossam paul Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  court ipewe mamlaka kikatiba kusajili vyama vya siasa kwan ofis ya msajil ni idara ya ofis ya wazir mkuu so pocbl kuna bias kwan wazir mkuu ni member wa one of the political parties,tendwa is not impartial.again namuunga mkono mtatiro kuwa katiba ijayo iondoe by election kuepusha unneccessary election cost kwa upuuz wa wa2 wachache wenye uchoyo wa madaraka na ku2mia kod za wananch vbaya.katba mpya itoe majb kwa haya mapungfu regardless gharama za democracy!
   
 18. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkuu umefikiria mbali sana ya Nape, Serikali imeundwa na wanaCCM, na wao ndo wanaiwezesha mahakama kufanya kazi zao, iweje mtu umuwezeshe asikutendee haki? Mnyime ugali tu ndo atakuwa upande wako
   
 19. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sidhani ka sitta ni ccm maana ni yeye peke yake serikalini akiwa kama waziri kwenye serikali ya JK amekubaliana na maamuzi ya mahakama wakati mbeshu wa ccm nnauye amesema watakata rufaa so tusikilize maoni ya ccm au serikali?
   
 20. hendeboy

  hendeboy JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hivi huyu mnauye yeye kila kitu ni kupinga tu, kama wao wanaona mahakama haijawatendea haki na wengine wasemeje
   
Loading...