Wana JF natamani Sitta angegombea urais kupitia Chadema 2015 awe Rais halafu Dr Slaa akagombee ubunge ateuliwe kuwa PM. Mawaziri akina mwakyembe, Ole Sndeka, Kilango, Mnyika, Mdee, Lissu nk. Nadhani hiyo timu ingefanikiwa sana.
Sitta na Dr ni watu wakali, wanaichukia rushwa, wana busara na ni waadilifu.
Ukimwangalia Sitta na ukirudi ukimwangalia Dr Slaa, unauona unyerere ndani yao. Pamoja na hawa mabwana kuwa na maadui wengi, ulishawahi kusikia wanatuhumiwa au kuzushiwa rushwa? Hawa maadui wangekuwa hata na chembe ya ushahidi wa rushwa wangeutumia.
Waulizeni watu wanaotokea Hanang au Urambo na pia chunguza mwenyewe utagundua hawa mabwana ni kati ya rare breeds zilizobaki Tz.