Walisema "Mfa maji haachi kutapatapa" Hilo ndio Bunge la Katiba.Spika wa BMK ameishauri serikali kupitia kwa waziri wa habari Mh Fenela kuwashughulikia ITV kwa kuendesha mijadala na makongamano.
Spika sitta amekereka kwa watu kutoa maoni yao kuhusu mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba ambayo ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Je akiwa Rais ataruhusu demokrasia nchini kweli?
Spika wa BMK ameishauri serikali kupitia kwa waziri wa habari Mh Fenela kuwashughulikia ITV kwa kuendesha mijadala na makongamano.
Spika sitta amekereka kwa watu kutoa maoni yao kuhusu mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba ambayo ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Je akiwa Rais ataruhusu demokrasia nchini kweli?
Kwani umelemaa mpaka uitaji kunyooshwa?(jisemee nafsi yako).Labda rais mbabe, dictator ndo wa kutunyoosha.
kwani hata asingelikuwa ameitoa, wewe ulitegemea anaweza kuwa rais 2015!??
hapo ndio utaujuwa uzuri wa kikwete kuhusu demokrasia.
Hata sitta demokrasia hiyo hiyo inampa uhuru wa kuongea na kutoa maoni yake, au demokrasia ni kwako tu?
Marahaba.
Simshangai Mh Sitta
kwani hiyo ndiyo tabia yake. Wengi wetu hawajui historia yake. Alikuwa
mmoja wa viongozi waliogoma chuo kikuu cha DSM enzi hizo wakidai posho
kubwa wakati huo na kupinga kwenda JKT miaka ya 1974 kama kumbukumbu za
watu waliokuwa naye wako sahihi, Na mmoja wa waliomwendea Mwalimu JK
Nyerere kuomba msamaha walipofukuzwa wote chuoni. Alitumika vile vile
kuwataja waliokuwa vinara wa mgomo ambao hawakusamehewa kabisa kurudi
chuoni kuendelea na masomo Hivyo tangu zamani ni ndumila kuwili
anayeangalia upepo unavyovuma na kujitupa kwenye mkondo ili apate
umaarufu. Mnakumbuka akiwa spika ailvyokalia kesi ya Mh Lowassa? Ni mtu
hatari zaidi ya tunavyomdhania.
kulikuwa na haraka gani kupost habari isiyokamilika?
Mkuu kwani kuna ubaya gani? Nimeweka habari niliyopata kwa ufupi radioni nikaweka gazeti lenye habari hiyo ili ufuatilie zaidi!
subiri usingizi uishe ndo upost acha kukurupuka
Vyama vinavyounda UKAWA CHADEMA, CUF na NCCR vimempunguzia Makali ya mbio za Urais mwaka 2015 mwenyekiti wa bunge maaulum la katiba Samuel Sitta. Hii ni kwa mujibu wa habari kwa ufupi magazetini ya radio magic fm kwa habari zaidi
Source : RAI nguvu ya hoja.