Sitta: Kuna Wabunge mizigo CCM

Sitta: Kuna Wabunge mizigo CCM

...huyu jamaa kwa kunyea kambi..? sijui atalala wapi,walichomfanya mpaka anahasira na chama chake anakijua mwenyewe...
 
Busega. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo kwani hata wakienda bungeni, hawachangii na wanabebwa na chama.

Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alisema hayo juzi jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama.

"Ukweli ni kwamba, baadhi ya wabunge wa jinsi hii hawatufai. Wanakwenda bungeni hawachangii, wanakwenda bungeni hawana hata hoja za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo," alisema Sitta.

Sitta alisema licha ya aina hiyo ya wabunge, pia wapo wale ambao hawafiki majimboni kwao kukagua shughuli za maendeleo.

"Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... inawezekana hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa wakiomba tena kura," alisema na kuongeza:

"Haiwezekani mbunge akakaa mjini na kushindwa kwenda kuwatembelea watu wake jimboni. Mbunge anakwenda jimboni kwa kuchungulia halafu wananchi wanamshabikia na kumpa kura?

"Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana hawayajui lakini watu hawaendi majimboni, wananchi watayafahamu vipi haya maendeleo?"

Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya, Sitta alisema: "Kwanza kuna viashiria vya baadhi ya watu kuanza kuipinga Katiba mahakamani. Watu hao wasiungwe mkono kwani ndio wanaoanza chokochoko.

"Katiba tunayoitaka ni kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na Watanzania na si ya wengine. Hivyo hatuna budi kila mmoja kutumia nafasi hiyo kuwasilisha mchango wake wa kuboresha kwenye Mabaraza ya Katiba."

Aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba watumie nafasi kuwasilisha hoja zinazojenga na wasiwe mamluki wa kuharibu mchakato mzima.

Awali, Sitta alishiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Kiloleli, Wilaya ya Busega na kuchangia Sh3 milioni.

Akizungumza katika harambee hiyo, iliyotarajiwa kukusanya Sh217,538,000, Sitta aliwataka wazazi kuwalea watoto wao katika misingi ya dini ambayo baadaye hutoa viongozi bora na wenye maadili... "Huwezi kuchukua tu mtu awe kiongozi, lazima wafunzwe misingi ya maisha na uongozi."


Naona anajikweza ki- raisiraisi huyu mzee. Kwani yeye amewachachafya vipi wapinzani?
 
Kuna yule jamaa mda wote ni usingizi akiamuka anaenda kuburudisha sisim ni nambari one!
 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta , amesema, " baadhi ya wabunge wa CCM Wakienda bungeni hawachangii lolote, hawaonekani Majimboni mwao, Wanabebwa na Chama, hawa ni mzigo"

"Wabunge wa jinsi hii hawatufai' hawana Hoja za kuchachafya upinzani" alisema Sitta.

Chanzo: Mwananchi, Jumanne, Julai 30, 2013
mbona yeye ndo mzigo namba moja kwani hajijui? awaulize mwigulu na nnape .
na pia ajiulize na kujitathmini kwanini alimzuia dr. mwakyemebe "asiseme mambo yote ambayo alitaka kusema ila akavunga ili kulinda heshima ya serikali ya magamba" huyu sita si ndiye aliyekuwa spika au sita mwingine, mnapopewa nafasi za kuongoza mnavunga , mkitolewa mnajidai ndo mnaona vibanzi kwenye macho ya wengine wakati maboriti yenu bado hamjayatoa vibanzi . luku vere vere bwana sita kwa sita.
 
Ikifika March-April,2015 kabla ya hamjampitisha mgombea wenu wa Urais,mtakuwa mmeshatoana roho kabisa ninyi majambazi CCM!
 
Kama chadema ilivyo mzigo kwa watanzania.
Dada Deograsia mbona unajidhalilisha na kuonesha ulivyo mweupe kichwani?? Sijawahi kubahatika kukusoma ukiwa umetoa hoja wewe mtu akisema Usiku mwema, wewe unajibu Nawewe usiku mwema, huna mawazo binafsi?? Wewe huku baaaado sana nenda facebook kule kunamchanganyiko mpaka watoto, vichaa, nao wapo, ukitaka kuwepo huku jifunze kwanza kwa kusoma post za wenzako ukishajua ndio uandike,
Na hizi ajira za Lumumba zitawafanya muwe vichaa ingawa mngeweza kuja kuwa potentials baadae maana unaambiwa kawaambie nyeupe ni nyeusi nawe kama dodoki unakuja mbio, hiyo ni nyeusi, unawaambia wenye akili zao. Shauri yako ajira hizo zitaisha tena sio mbali shida ni kuwa muda huo utakuwa umeachiwa uchizi sijui utaishije. Ila jitume bwana watoto waende choo
 
Big up mzee Sitta... Wabunge wengi hovyoo sana,Kama kwetu sumbawanga tuna mbunge bogus kabisaa anaitwa aeshi...atakusoma hajui dunia hiiiii...... Pesa zitatutoa roho
 
Acha hizo Muraa!!

CCM hakuna mizigo, ndo maana nimempiga kijembe Mzee Six.
Wabunge wa CCM ni slow but sure, smart operators behind the curtain!!

Siyo kama Halima Mdee a.k.a Boxer, au Mnyika mastatement mengi vitendo zero, Sugu ndo kabisa hasara bin hakuna rizki.

Wabunge wengi wa upinzani tontorillo nyingi na wengi hawatarudi 2015, tunawasubiri mitaani DSM.

We mzee wacha kabisa kujidanganya, hili bunge la sasahivi bila wabunge wa Chadema kila kitu kinakuwa cha hovyo na bunge linakosa mvuto. Ilipotokea milipuko ya Arusha na wabunge wetu kuondoka bungeni bunge lilipwaya sana hadi kufikia hatua kupitishwa kwa kodi ya kijinga kabisa ya simcard ambayo baade mabunge mizigo hayo hayo ya ccm yakiongozwa na January yanataka sheria ya fedha ya mwaka 2013 irudishwe bungeni kufanyiwa marekebisho.

Huwezi kumfananisha kamanda Halima Mdee na mbunge yeyote kijana ndani ya ccm, she is far better than anyone, huwezi kumfananisha kamanda Mnyika au Sugu na hiyo mizigo yenu. Kamanda Mnyika anasema na kutenda, Kamanda Sugu anasema na kutenda na hilo unalifahamu lakini kwakuwa mizigo huko ccm ni mingi angalia na wewe usijekuwa ni mzigo basi tu hujatambulika.
 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta , amesema, “ baadhi ya wabunge wa CCM Wakienda bungeni hawachangii lolote, hawaonekani Majimboni mwao, Wanabebwa na Chama, hawa ni mzigo”

“Wabunge wa jinsi hii hawatufai’ hawana Hoja za kuchachafya upinzani” alisema Sitta.

Chanzo: Mwananchi, Jumanne, Julai 30, 2013


bungeni ni kuchachafyana na wapinzani tu? lini watafikiria kujenga hoja za kuwaletea wananchi maendeleo?
kwa umri huo kama bado anadhani kulumbana ndo tija, hata lini basi atafikiria watu waje na hoja za kuboresha maisha ya watanzani bila kujali hoj imetolewa na upande gani yaani upinzani au chama tawala kwa maana ya serikali!
nawashauri wabadilike kufikiria hoja za upinzani zinahitaji kuchachafya tu na mwishowe zipingwe kwa njia yoyote! yaani kwa kutumia kura ya wingi wa wabunge, spika,na hata mwanasheria mkuu wa serikali au hata vyombo vya usalama.
 
kila ntu ni mzigo kwa mwenzake. inategemea unaongelea katika context ipi.
 
Naona mzee Sitta amekuwa Katibu Mwenezi wa mambo ya reja reja ya Chama!!!

Umeona mkuu mzeze sitta imebid aanze kufanya kazi ya chama maana wizara aliyopewa inamfanya asisikike katika vyombo vya habari na ukizingati mawazir wetu wanapenda kuonekana katika vyombo vya habari wakati siku zote wanasema hawafanyi kazi na Magazeti. Maana leo sita utamsikia anataka Lowasa amtajie rafiki zake wanaomchangia kesho utamsikia kuhusu wabunge wa CCM daah! Sijui Nape na kinana watafanya kazi gan?
 
Uzuri maneno yake huzungumzia kanisani!Hazungumzi kwenye vikao rasmi vya chama
 
Kwa Pesa na Posho wanazotia ndani, na upuuzi unaopita Bungeni; Wabunge wote ni Mzigo kwa Taifa...., Maybe Apart from Five or Four of them
 
Wabunge mizigo ni pamoja na lema,msigwa na sugu.

Uncle Deo,
hivi ukiacha kuchafua mada utaugua kichaa? Hao uliowaleta hapo wana nini na ccm ya Sita??? Vichaa wengine hawafai hata Mirembe. We unaonesha una kichaa cha miguuni, nenda pale Muhumbili.
 
Back
Top Bottom