Sitta: Kuna Wabunge mizigo CCM

Sitta: Kuna Wabunge mizigo CCM

Wabunge mizigo ni pamoja na lema,msigwa na sugu.

Hivi kumbe Godbless Lema,mchungaji Peter Msigwa na Rais wa Mbeya Joseph
Mbilinyi a.k.a Sugu,nao ni wabunge wa chama cha mapinduzi..!? Maana
nimeona mzee 6 ametaja wabunge wa ccm,ww umetaja majina.
 
Sitta ni wale wale hana cha kujivunia kokote hapa Tanzania, hivi amekaa miaka mingapi bungeni yeye na mke wake? Urambo ukifika utashangaa sana maendeleo yako nyuma sana, yaani wanyamwezi kama wamerogwa vile kwa kuchagua waroho wa madaraka na ndio bwana.......Mkumba, Rage, Sitta, Dalali, Kigwangalla....
 
Hata hapo yuko chama kingine. We unataka aende physically? Hapo anafanya kazi ya chama kingine ndani ya ukoo wa panya. Sitta husihame chama, bomoa nyumba ukiwa nao ndani.
Hahahahahaaa........kama vipi alipue baruti kabisa.
 
Mke wa Samwel Sitta alihonga ili apite kwenye viti maalum, akabambwa na TAKUKURU, Mzee akaingilia kati ili waende wote Bungeni kwa maana hiyo naye ni Mzigo. Pia huyu Sitta haaminiki anayosema yanatokana na eneo alilosimama ni MNAFIKI SANA.
 
CCM wasivyompenda huyu mzee..sidhani kama watampitisha tena 2015
 
Kuwachachafya wapinzani!!?, nilifikiri kuleta hoja za kulipeleka mbele taifa.
 
Sitta nae anaanza kuzeeka na kupata kifafa cha siasa alikua wapi siku zote kusema hayo, na kwa nini asiwe na ujasiri wa kuwataja kwa majina badala ya kuweka average disposition.
 
Mzee Six anafanya hivyo kujaribu kuokoa jahazi la ccm baada ya vuvuzela nape kushindwa kuhimili vishindo. Badala ya kumlaumu ulitakiwa umshukuru kwa kuwakumbusha wabunge wenu wa ndiyo wafanye kazi zao kikamilifu.

Ni ukweli kwamba wabunge wengi wa ccm takribani asilimia 95 ni mizigo kwa wananchi waliowachagua, ni mizigo kwa chama chenu ccm lakini pia ni mizigo kwa majimbo wanayoyawakilisha.
Acha hizo Muraa!!

CCM hakuna mizigo, ndo maana nimempiga kijembe Mzee Six.
Wabunge wa CCM ni slow but sure, smart operators behind the curtain!!

Siyo kama Halima Mdee a.k.a Boxer, au Mnyika mastatement mengi vitendo zero, Sugu ndo kabisa hasara bin hakuna rizki.

Wabunge wengi wa upinzani tontorillo nyingi na wengi hawatarudi 2015, tunawasubiri mitaani DSM.
 
Busega. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo kwani hata wakienda bungeni, hawachangii na wanabebwa na chama.

Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alisema hayo juzi jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama.

“Ukweli ni kwamba, baadhi ya wabunge wa jinsi hii hawatufai. Wanakwenda bungeni hawachangii, wanakwenda bungeni hawana hata hoja za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo,” alisema Sitta.

Sitta alisema licha ya aina hiyo ya wabunge, pia wapo wale ambao hawafiki majimboni kwao kukagua shughuli za maendeleo.

“Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... inawezekana hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa wakiomba tena kura,” alisema na kuongeza:

“Haiwezekani mbunge akakaa mjini na kushindwa kwenda kuwatembelea watu wake jimboni. Mbunge anakwenda jimboni kwa kuchungulia halafu wananchi wanamshabikia na kumpa kura?

“Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana hawayajui lakini watu hawaendi majimboni, wananchi watayafahamu vipi haya maendeleo?”

Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya, Sitta alisema: “Kwanza kuna viashiria vya baadhi ya watu kuanza kuipinga Katiba mahakamani. Watu hao wasiungwe mkono kwani ndio wanaoanza chokochoko.

“Katiba tunayoitaka ni kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na Watanzania na si ya wengine. Hivyo hatuna budi kila mmoja kutumia nafasi hiyo kuwasilisha mchango wake wa kuboresha kwenye Mabaraza ya Katiba.”

Aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba watumie nafasi kuwasilisha hoja zinazojenga na wasiwe mamluki wa kuharibu mchakato mzima.

Awali, Sitta alishiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Kiloleli, Wilaya ya Busega na kuchangia Sh3 milioni.

Akizungumza katika harambee hiyo, iliyotarajiwa kukusanya Sh217,538,000, Sitta aliwataka wazazi kuwalea watoto wao katika misingi ya dini ambayo baadaye hutoa viongozi bora na wenye maadili... “Huwezi kuchukua tu mtu awe kiongozi, lazima wafunzwe misingi ya maisha na uongozi.”
 
Yeye mwenyewe ni mzigo

hahahahahaha tena mzingo wa mavi kafanya nn tabora ndo wazir toka miaka ya 60 huko kashindwa unganisha lami toka tbr mjin mpk urambo kwake ...ata hy urambo yenyewe kafanya nn cha maana labda kwa kujenga hiyo ofic ya kufikia spika,...hahahahaha mzee anachekesha sana kashindwa tbr(mkoa) et anataka nchi mweee!!
 
:wave::wave::wave::wave:...........WITH PLEASURE

images
hashima kwako mkuu Safari_ni_Safari haya jamani huyu hapa ni mzigo zaidi ya kiroba cha kokoto,akishtuka hapa anagonga meza kwa nguvu na kuunga mkono hoja mia kwa mia,shame on you 6 na masisiem yako!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom