Mwanangu, Sita siyo stable tena kwa sababu nyingi tu. Lakini kubwa ni dhamira yake (nadhani iliyo nzuri) na matendo yake ambayo ni kinyume, na dhamira yake. Na anafanya hivyo kwa sababu ya chama chake. Wote tunajua ukiwa ndani ya sisiem inabidi uwe mnafiki kubwa uweze kulinda maovu ya kifisadi ambayo ni itikadi ya chama hicho. Hili linamsumbua sana Sitta, ndio maana alitaka kuanza ccj. Sasa hili la kutaka kuanza ccj kuwekwa hadharani kuwa alihusika linamtesa sana, anashindwa kupima ni kwa namna gani hasa wanafiki wenzake ndani ya chama wanamfikiria. Angekuwa na pa kukimbilia angeondoka lakini kwa sasa hana, inambidi anganganie ndani ya ccm kwa unafiki unaomdhalilisha sana akiomba kuwa muda utapita na yote yatakwisha (time is a great healer). Uspika walimnyima kwa kuwaumbua mafisadi, sasa anataka kuwabambeleza mafisadi walewale wasimtoe roho, kwa uhakika anajua urais hawezi kuupata akiwa ndani ya hiki chama kinachoelekea ambako siko.
Mungu msaidie Sitta aweze kufikiria tena kama msomi. Amen.