Sitta atoboa siri ya CCJ

Ewe Bwana mwema ! umewaumba wanadamu wote kutokana na wazazi wamoja. umekusudia kuwa wote wawe jamii ya nyumba moja. mbele ya utakatifu wako wote ni watumishi wako, naikabizi jf mikononi mwako na wanadamu wote uwalinde chini ya hema lako,wote uwakusanye pamoja kwenye meza yako ya ukarim, wote wang'ae kwa mwanga wa neema yako

Ee Baba mwema furahisha roho zetu kwa manukato ya upendo wako. Angaza macho yetu kwa mwangaza wa uongozi wako. Furahisha masikio yetu kwa sauti tamu ya Neno lako, na utulinde sote katika NGOME ya neema yako.

wewe u mwenye uwezo na mwenye nguvu, wewe u msamehevu na wewe u yule asiyeangalia makosa ya wanadamu sisi ni wenye zambi hatusitahili hata kusimama mbele za uso wako
 
Hii inakuwaje siri jamani ? Mbona ukweli uko wazi au kuna mtu alimtegemea huyu fisadi mnafiki kukiri uhusika wake CCJ. Amesahau aliyoyasema wakati akiulilia Uspika ? Naona baada ya kuhakikishiwa kuwa ataendelea kukaa kwenye ile nyumba ya mamilioni na zile furniture za bei mbaya, sasa anaweza akaropoka anavyotaka. Anachosahau ni kuwa kama kuna wakati angetakiwa kutulia na kupima kwanza kina cha maji kabla ya kuyajavulia nguo ni huu ! Mbona Sitta hakukanusha madai ya huyu kada wa CCM ? Tukumbushane yaliyotokea mapema mwaka huu

Kaka ukisha kuwa CCM ama kiongozi au mwanachama unakoma mambo mengi tu kasoro kupumua lakini mengine yote unakoma kuwa na akili safi , utu unakutoka , aibu hakuna , unakuwa fyatu, kwapuakwapua ni wewe .Na upuuzi mwingine mwingi.Sitta watu walimuoma shujaa lakini wapi .Mie nilimkataa zamani sana .Now here we are .
 
sita

ameereza nijinsi gani wenye pesa ndani ya ccm walivo kuwa wamepania kumtowa ikashindikana kwamaelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea uraisi bado alibaki imala anashanga kusakamwa

mimi sihusiki na ccj hao walionifata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama yvao leo wananipaka matopo kajifananisha na chuma chapuwa hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama 6 kayaeleza hayo mbeya

chanzo live G fm mbeya

alikuwa na ushahidi wowote?
 
Wewe Mufiyakicheko aliyekuambia humu JF wote ni wagalatia nani? Mbona unajaza nyaraka tuu? kuwa na adabu ebo!
 
sita (ameereza) nijinsi gani wenye pesa ndani ya ccm (walivo) kuwa wamepania (kumtowa) ikashindikana kwamaelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea (urais)i bado alibaki( imala) anashanga kusakamwa mimi sihusiki na ccj hao walionifata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama( yvao) leo wananipaka (matopo) kajifananisha na chuma chapuwa hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama 6 (kayaeleza) hayo mbeya chanzo live G fm mbeya
Kamwenee!!
 
Anawahi kuanzisha thread, asije kuta imeanzishwa humu.
Ingawa umenichekesha, lakini naamini Mufiyakicheko alikuwa na haraka tu, mbona kaandika kiswahili safi kabisa post nyingine humu. Hata hivyo ujumbe unaeleweka vizuri tu.
 
sita ameereza nijinsi gani wenye pesa ndani ya ccm walivo kuwa wamepania kumtowa ikashindikana kwamaelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea uraisi bado alibaki imala anashanga kusakamwa mimi sihusiki na ccj hao walionifata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama yvao leo wananipaka matopo kajifananisha na chuma chapuwa hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama 6 kayaeleza hayo mbeya chanzo live G fm mbeya
Huyu mbaba(sita) ni mnafiki sana
 
Kaka ukisha kuwa CCM ama kiongozi au mwanachama unakoma mambo mengi tu kasoro kupumua lakini mengine yote unakoma kuwa na akili safi , utu unakutoka , aibu hakuna , unakuwa fyatu, kwapuakwapua ni wewe .Na upuuzi mwingine mwingi.Sitta watu walimuoma shujaa lakini wapi .Mie nilimkataa zamani sana .Now here we are .
Sure yaani amekuwa kituko kama mr bean.Mizee mingine ovyo kabisa lingekuwa zee langu ningelikata vibao linanikera sana.
 
jamani huyu jamaa yuko mbeya anatujuza yanayotokea kwenye mkutano wa magamba. Please be in context when reading.

I agree with you sir....being a great thinker means you think ahead of others/things! if you are a great thinker, mbona inaeleweka ingawa kuna makosa tunayoyaona.
 
Kweli nimeamini Siasa ni Upepo kama wenyewe wanavosemaga "UPEPO wa KISIASA" hasa za CCM Chama Tawala!
Mwanzoni mapacha 3 wa kujivua Gamba Mahiri na kuonekena nguzo ya chama,sasa hivi ni Mzigo kwa Chama tena ni chanzo cha Chama Kupoteza Mvuto!
Sasa Upepo Uhamia kwa Mapacha watatu CCJ(Laukama wanaikataa CCJ,Mh.Mpendazoe Amewataja na kusema alikuwa Nao).
Watu kuamua Kujenga Chama Chao ndio Siasa,Angalizo kwa Chama Husika ni Kuangalia na Historia ya watu wanao watumia kwa Ujenzi na Umahiri wao wa Kujenga Hoja na Uvumilivu wao katika mapito mbalimbali!Hasa katika Kipindi ambacho chama kimepoteza Mvuto na Kutikisika!

images (1).jpg MB 2.JPG MB 3.JPG
Mathalan,Kule Mbeya Pacha 1 alisema tatizo la Umeme si Uhaba wa Maji ni Mikataba Mibovu ya Umeme!Hapa najiuliza mikataba mibovu ya Umeme mingapi ni ipi zaidi ya Ule wa Dowani na IPTL!Na hata Ukiangalia mikataba yenyewe ilikuwa ya umeme wa Dharura tu na si wa Kudumu,kimsingi mikataba haikuwa ya kutatua tatizo la Umeme bali kukabiliana na Dharura kwani umeme wake haukuwa si kutosheleza hitaji la Taifa!Nilichotegemea Kusikia nini kilifanyaka toka mikataba mibovu imeingiwa katika kumaliza tatizo la Umeme.Kadhalika kuwaeleza wananchi chanzo mbadala zaidi ya kutegemea Maji kuwa Chanzo namba moja cha Umeme wa Taifa,waweke wazi ni vyanzo vingapi vipya vya Umeme wa Kudumu vimeshapatikana na vitaanza kumwaga Umeme lini!
Pili,Historia ya Kujivua gamba iliyotolewa itasaidia nini wananchi,wananchi tunataka majawabu ya matatizo yetu ya sasa na yaliyotuzingira kama Kupanda kwa Gharama ya maisha ya kila siku na Mustakabali wa Elimu Bora kwa Wanetu,Afya zetu sisi wote hasa sie wavijijini,Hatiima ya Kilimo Kwanza,Namna ya Kuwekeza na sehemu za kupata mitaji na Masoko kuuzia mazao yetu na kupata senti walau za Kujikimu wa Familia Zetu!

Tatu,Serikali imejipanga vipi Kuwahudumia wazee wote nchi hii na Makundi ya wasiojiweza ili wakati Serikali inahudumia wazee na makundi ya wasio Jiweza Sie wananchi wengine tunachapa kazi ili kukuza Uchumi wa Taifa utaoliwezesha kujimudu na kuhudumia watu wake sambamba na namna ya Kulinda Rasilimali zetu zilizobaki na kuonesha mchango wa Rasilimali zetu zinazotumika sasa kwa maendeleo ya Taifa

Nne,wengine wanaanza kuwaambia haditi ya Maamuzi Magumu,mara yanatakiwa Maamuzi Makini,Malumbano ya Nini,kwani hamjui katika chama chenu malumbano ndio yaliyo wagharimu!Siku hizi siasa za Malumbano haziuzi Chama!(Waungwana Hulumbana ndani ya Nyumba na Si Hadharani)
Kwahiyo Mambo ya Histori tuwekewe kwenye TV na vombo vya Habari na tuelezewe zaidi Siku ya Sherehe ya Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika(Siyo Tz)!
Jamani Ndg Mapacha 3 wa CCJ nawapongeza kwa kuaminiwa!
Lakini wenzenu tunataka "MAISHA BORA YAYOONEKANE KATIKA MAZINGIRA YETU"
Leo Mkweche kawa "politiko konsaltanti"
 
Mkweche nimekusoma. Sijafahamu kwa undani yaliyojili jana huko Mbeya ila nakubaliana na wewe kuwa kama hizo kauli ndo zilivyotolewa basi ni kweli umekuwa "politiko konsaltanti"
 
Sitta aliponea chupu chupu kunyang'anywa kadi na wanamatandao wa Rostam sasa analipiza kisasi wamemnyima uspika wataona
Nape yeye ni utoto tu akikua ataacha arobaini zake zinahesabika.
 
Hao ndo magamba bwn,leo wanasema hivi kesho wanasema vile,m2 kama samwel sitta ni mnafki 2 kwenye jamii tn ni m2 wa visasi.
 
Mkweche nimekusoma. Sijafahamu kwa undani yaliyojili jana huko Mbeya ila nakubaliana na wewe kuwa kama hizo kauli ndo zilivyotolewa basi ni kweli umekuwa "politiko konsaltanti"
Sitta alisema tatizo la umeme si mvua ni mikataba mibovu anapingana na rais wake aliyesema tatizo ni mvua ila hana uwezo wa kujigeuza mawingu.
Mwakyembe akasema wenye busara hawafanyi maamuzi magumu wanafanya maamuzi Makini, ina maana kuwa Lowassa hana busara.
yalikuwa ni malumbano ya wenyewe kwa wenyewe lakini acha watambiane zamu yao kushika mpini
wanamtandao walie tu wanapukutishwa kama upupu walidhani Mkwe. re ana undugu nao,
nadhani RACHEL hawakumwelewa aliposema urais wake hauna ubia.
Cheki hapa one after another whos next
KATUNI(493).jpg
 
Ingawa kuna watu kadhaa humu wamejitahidi kuifanyia masahihisho thread hii, lakini bado nami naona kuna makosa, basi nami nadhani ingesomeka hivi.

Sitta ameeleza ni jinsi gani wenye pesa ndani ya CCM walivyo kuwa wamepania kumng'oa ikashindikana.
(Ingawa wenye pesa hao anaowasema walifanikiwa kumng'oa katika u-speaker) haya maandishi ya blue nimeyaongeza mie. Kwa maelezo yake anasema, vyama vingine vilimshawishi kugombea Urais kwa tiketi ya vyama hivyo lakini bado alibaki imara. Anashangaa kwa nini anasakamwa! ''Mimi sihusiki na CCJ, hao walionifuata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama vyao leo wananipaka matope'' alisema Sitta. Amejifananisha na chuma cha pua, na akasema hakuna mwanachama ndani ya CCM aliye pata misukosuko kama yeye. Yote haya kayaeleza huko Mbeya. Chanzo: Live G FM Mbeya.

Thread hii ujumbe wake ulikuwa unaeleweka licha ya kasoro zake. Ukisoma thread nyingi humu utakuta makosa ya kiuandishi kibao, hii ni kutokana na ukweli kwamba wengine si wasomi wa lugha nk. Naomba tusiuwe mawazo ya wenzetu kwa sababu la lugha, hata hivyo hili si jukwaa la lugha.
 
Mshkaji umeandika kisukuma, maana hivyo vishindo!!!!! sijakupata.
Kisukuma kimeingiaje hapo jamani! Muulizeni tu kwa ustaarabu alichotaka kuandika ni nini. Pengine mumshauri awe anatafuta mhariri wa mada zake kabla ya ku-post. Itamsaidia, na sisi pia.
 
Wewe Mufiyakicheko aliyekuambia humu JF wote ni wagalatia nani? Mbona unajaza nyaraka tuu? kuwa na adabu ebo!
Sala na maandiko matakatifu ni chakula cho kiroho bila kujali dini au dhehebu hayo siyangu ni yamungu kama mungu hanaadabu misijuwi yabadilishe kwa kialabu utajuwa naamanisha nini
 
hao walionifuata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama vyao leo wananipaka matope'' alisema Sitta. Amejifananisha na chuma cha pua, na akasema hakuna mwanachama ndani ya CCM aliye pata misukosuko kama yeye.

hao waliomfuata walikuwa chadema walimwahidi kumpatia 1bln tshs.

 
Dah! hii thread na wachangiaji wake wamenipa raha, yaani mambo ni prakatumba. teh teh teh teh teh teh teh teh teeeh
 
Wewe Mufiyakicheko aliyekuambia humu JF wote ni wagalatia nani? Mbona unajaza nyaraka tuu? kuwa na adabu ebo!
5:67Qur-an Ewe mtume fikisha uliyoamriwa kutoka kwa mola wako na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wake, na mwenyezi MUNGU atakulinda na watu. Hakika mwenyezi MUNGU hawaongozi watu wanaokufuru
 
Back
Top Bottom