Sitta atoboa siri ya CCJ

Sitta atoboa siri ya CCJ

ENYI MNAOONEKANA KUWA WASAFI NA KUMBE NDANI WACHAFU mko kama maji safi lakini machungu,ambayo kwa kutazamwa kwa nje yanaonekana safi kabisa lakini yakipimwa hakuna hata tone linalokubaliwa. Naam mwonzi wa jua huangukia sawasawa juu ya vumbi au juu ya kioo lakini hutofautiana katika kurudisha nuru kama nyota inavyotofautiana na dunia
Huyu aliyeandika haya ndiye yuleyule Mufiyakicheko kweli? Au uliamua kutuua kwa kicheko?
 
Mkuu mbona hueleweki? Hiki ulichoandika ni kiswahili au? Unasoma darasa la ngapi?

sita

Ameeleza ni jinsi gani wenye pesa ndani ya ccm walivyo kuwa wamepania kumtoa ikashindikana kwa maelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea uraisi bado alibaki imara anashangaa kusakamwa

Mimi sihusiki na ccj hao walionifuata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama yvao leo wananipaka matope kajifananisha na chuma chapua hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama 6 kayaeleza hayo Mbeya.

chanzo live G fm mbeya
 
Sitta ni mnafiki alitaka kusaliti ccm baada ya kuhaidiwa madaraka akawatema ccj.
 
ENYI MNAOONEKANA KUWA WASAFI NA KUMBE NDANI WACHAFU mko kama maji safi lakini machungu,ambayo kwa kutazamwa kwa nje yanaonekana safi kabisa lakini yakipimwa hakuna hata tone linalokubaliwa. Naam mwonzi wa jua huangukia sawasawa juu ya vumbi au juu ya kioo lakini hutofautiana katika kurudisha nuru kama nyota inavyotofautiana na dunia
↲Hii umeandikiwa kaka/dada
 
Unapopost usitetemeke mkubwa,tulia andika kitu chenye maana siyo unaandika utadhani ni mipasho.rudia tena ulikuwa unamaanisha nini?

Anawahi kuanzisha thread, asije kuta imeanzishwa humu.
 
↲Hii umeandikiwa kaka/dada
EWE MWANA WA ROHO Hakuna amani yoyote kwako ila tu kwa kujikana mwenyewe na kumgeukia mngu kwani ya kupasa kujitukuza katika jina la mngu na siyo katika jina lako mwenyewe weka imani yako ndani ya mngu wekeza kwa mngu
 
sita

ameereza nijinsi gani wenye pesa ndani ya ccm walivo kuwa wamepania kumtowa ikashindikana kwamaelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea uraisi bado alibaki imala anashanga kusakamwa

mimi sihusiki na ccj hao walionifata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama yvao leo wananipaka matopo kajifananisha na chuma chapuwa hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama 6 kayaeleza hayo mbeya

chanzo live G fm mbeya

Mufiyakicheko,

Thread yako ilipaswa isomeke hivi: Sitta ameeleza ni jinsi gani wenye pesa ndani ya CCM walivyo kuwa wamepania kumtoa ikashindikana. Kwa maelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea Uraisi lakini bado alibaki imara. Anashangaa kwanini anasakamwa!

''Mimi sihusiki na CCJ,hao walionifuata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama vyao leo wananipaka matope'' alisema Sitta. Amejifananisha na chuma cha pua na akasema hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama yeye. Yote haya kayaeleza huko Mbeya.

Chanzo: Live G FM Mbeya.
 
Anawahi kuanzisha thread, asije kuta imeanzishwa humu.
EWE MWANA ANASA ZA DUNIA Ni ya kupendeza milki ya kuwa hai kama ungeifikia ni ya fahari milki ya umilele kama utapita dunia ya mauti ni tamu furaha kuu takatifu kama utakunywa katika kikombe kisichoelezeka kutoka katika mikono ya mngu kama utafikia daraja hili utaokolewa kutoka katika maangamizi ya dhambi
 
Mufiyakicheko,Thread yako ilipaswa isomeke hivi: Sitta ameeleza ni jinsi gani wenye pesa ndani ya CCM walivyo kuwa wamepania kumtoa ikashindikana. Kwa maelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea Uraisi lakini bado alibaki imara. Anashangaa kwanini anasakamwa! ''Mimi sihusiki na CCJ,hao walionifuata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama vyao leo wananipaka matope'' alisema Sitta. Amejifananisha na chuma cha pua na akasema hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama yeye. Yote haya kayaeleza huko Mbeya. Chanzo: Live G FM Mbeya.
Asante mkuu nifani za watu
 
jf napenda niwakumbushe kunaandiko

EWE MWANA WA KUWA !

usiitakie roho yeyote kile ambacho wewe usingejitakia na usitamke lile usilolitenda maneno yako yaendane na vitendo vyako fahamu kwa ukweli yule awambiaye watu wawe wa haki nayeye mwenyewe akatenda udhalimu huyo siye wa mngu ata akiitwa kwa jina la mngu

Ungeandika Mungu na sio Mngu! uwe unaanza na herufi Kubwa... Heshima Muhimu
 
EWE MWANA WA ROHO Hakuna amani yoyote kwako ila tu kwa kujikana mwenyewe na kumgeukia mngu kwani ya kupasa kujitukuza katika jina la mngu na siyo katika jina lako mwenyewe weka imani yako ndani ya mngu wekeza kwa mngu
Hongera ndugu, inaonesha unaimani ktk Mungu (nadhani ulimaanisha hivyo ulipoandika mngu)Samahani, hivi, mtu wa imani kwa nini umejipa jina la Mfia Kicheko?
 
Myie watu vp mbona mmevuruga mada, tbc iliroga kwenye taarifa ya mbeya haikutoa sauti wakaipotezea tuliishia kumwona 6 na Nape wakiandamana na watu wasiofika hata 1000, dk slaa alikusanya zaidi ya watu 40,000 mbeya, kuna anayebishaaaa? Je, je, unabishaaaaa
 
Hongera ndugu, inaonesha unaimani ktk Mungu (nadhani ulimaanisha hivyo ulipoandika mngu)Samahani, hivi, mtu wa imani kwa nini umejipa jina la Mfia Kicheko?
unapendekeza niitwe nani?
 
Hii inakuwaje siri jamani ? Mbona ukweli uko wazi au kuna mtu alimtegemea huyu fisadi mnafiki kukiri uhusika wake CCJ. Amesahau aliyoyasema wakati akiulilia Uspika ? Naona baada ya kuhakikishiwa kuwa ataendelea kukaa kwenye ile nyumba ya mamilioni na zile furniture za bei mbaya, sasa anaweza akaropoka anavyotaka. Anachosahau ni kuwa kama kuna wakati angetakiwa kutulia na kupima kwanza kina cha maji kabla ya kuyajavulia nguo ni huu ! Mbona Sitta hakukanusha madai ya huyu kada wa CCM ? Tukumbushane yaliyotokea mapema mwaka huu


Na Mwandishi Wetu - Majira

KIZUNGUMKUTI cha uasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ), kimeendelea kuwazunguka makada waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
vigogo walioko serikali, ambapo 'muasisi' mwingine amejitokeza akiweka hadharani madai yake juu ya waliohusika katika mpango huo.

Daniel Ole Porokwa, ambaye alijitambulisha kuwa ni kada wa CCM, akizungumza jana na waandishi wa habari Dar es Salaam, alikiri kuombwa kuwa mmoja mwanzilishi wa CCJ, akidai kuwa alishawishiwa kufanya hivyo baada ya kukutana mara kadhaa na Bw. Nape Nnauye, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bw. Fred Mpendazoe na Bw. Samuel Sitta.

Alidai kuwa katika mikutano zaidi ya mitano aliyofanya akiwa na Bw. Nnauye na Dkt. Mwakyembe, wenzake hao walimweleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM, kwa hoja kuwa chama hicho kilipofikia hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka kuongoza dola.

Kwa madai ya Bw. Porokwa, viongozi hao aliokuwa akikutana nao katika mipango ya kuanzisha CCJ, walisema CCM haiaminiki tena machoni mwa Watanzania na kimepoteza mvuto mbele ya umma, kwa sababu kimeacha misingi yake, iliyowekwa na waasisi wake, akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

"Nimeamua kufanya hivi (kutoa madai hayo) kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaoneshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita, tuamini katika hiyo njia tunayoelekea. Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu ni kusema ukweli...uongo na fitina ni mwiko.

"Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mheshimiwa Nape Nnauye, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe na Mheshimiwa Fred Mpendazoe.

"Aidha nilikutana mara moja na Mheshimiwa Samwel Sitta baada ya Mheshimiwa Nape na Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza. Naye Sitta alieleza kuwa nilichoelezwa na Nape na Mwakyembe hakina chembe ya mashaka," alisema Bw. Porokwa.

Aliongeza sababu nyingine ya kuamua kusema hayo ni baada ya kuwasikia Bw. Nape na Dkt. Mwakyembe wakimkana Bw. Mpendazoe, ambaye ndiye aliyeibua tuhuma hizo za vigogo wa CCM na serikali waliohusika kuanzisha CCJ, akijenga hoja kuwa itakuwa ni vigumu kwa chama hicho na serikali yake kuwatumikia wananchi;

Kama viongozi wake wamefikia hatua ya kusigana kiitikadi na kutokuwa wamoja katika masuala ya msingi ya utawala na uongozi wa nchi, kwa maslahi ya Watanzania wote.

Akijibu shutuma hizo baada ya kupigiwa simu na Majira, Bw. Sitta ambaye alisema alikuwa safarini kutoka Arusha, alijibu;

"Hivi waandishi wa habari hili suala...people can change parties let alone kuanzisha vingine...kwa hiyo amenizungumzia mimi...let us forget it, sisi tunashughulikia mambo makubwa zaidi ya hayo," alisema kisha akakata simu.


Naye Dkt. Mwakyembe alipoulizwa bila kufafanua alisema 'Muulizeni huyo Porokwa kama aliacha kugombea ubunge kwa sababu ya pesa, leo kapewa shilingi ngapi ili azungumzie suala hilo.
 
Jamani Mfiakicheko kasema hajasoma but kaona atupe yaliyo jiri huko .Mie nimesoma na kurudia mara 4 hadi nikapata maana sasa nawe fabya hivyo .Asante ndugu mleta mada mie pia nimekuelewa .
 
Back
Top Bottom