Sitta ajitosa mgogoro wa Umeya Arusha

Duh !! Kweli Arusha wameamua..

Mathayo 18:18
Amin,nawaambieni,yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.

Kwa hiyo Nape Nauye aipofungiwa na Yusuph Makamba wakati ule na hata mbinguni alifungiwa?
 
Aiyekuwepo kaniambia hivi "

Mimi nilikuwepo na habari ilikuwa kama ifuatavyo , Mb Arusha mjini ( Lema) alipewa mic na Mh Sitta asalimie wananchi na kuchangia harambee hiyo na Bwana Lema , alimtambua Meya feki kama Diwani wa Olorieni na siyo meya huku akisisitiza kuwa yeye ana ugomvi binafsi na Meya isipokuwa mfumo uliompata meya unamfanya meya huyo kuwa katili wa haki za binadamu na utu . nukuu Lema " Mh Baba Askofu na mgeni rasmi mimi kama mbunge nitakuwa mtu waq ajabu kama nitashindwa kusimamia haki mbele ya madhabau hii ya Mungu na hivyo ukweli unabaki kuwa Arusha mjini hakuna Meya na mimi mbunge simtambui meya ila natambua uwepo wa Diwani wa Kata ya Olorieni bwana Gaudensi Lyimo , naomba ileweke kuwa mimi sina ugomvi binafsi na Bwana Gaudensi na hata hakitaka kunywa chai kwangu namkaribisha sana isipokuwa nimuombe tena Mh Sitta kama mzee wetu kwenye siasa muda mrefu awaambie wakubwa wengine hasa waziri mkuu kwamba tatizo hili si afya kwa Arusha lakini hata hivyo hatutarudi nyuma kupigania haki iliyoporwa katika uchaguzi wa umeya na kama kuna mtu anakerwa na mgogoro wowote unaotafuta hakli basi yeye aendelee kukerwa na sisi kwetu ni baraka kwani haki tutaitafuta by the ballot or the bullet.
Bwana Gaudensi alivyotaka kumjibu Lema ndipo waumini wote wakaanza kumzomea Bwana Lyimo, na Mh Sitta akahaidi kusaidia mchakato wa mazungumzo yalioanzishwa na Bwana Pinda na Mbowe kufikia tamati kabla ya 2012.
 
Lile zimwi la kutokukubalika kwa diwani wa kata ya Olorien kama Meya wa jiji la Arusha limeendelea kumwandama Diwani huyo leo baada ya kupata mapokezi hafifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt. Teresia jijini Arusha inayoongozwa na Mh. Samwel Sitta. Tofauti na wageni wengine waliokuwa wakishangiliwa kwa vigelegele na makofi wakati wa utambulisho, Mh. Gaudence Lyimo hakupata mapokezi hayo kutoka kwa waumini hao kama wenzake. Waumini walionyesha kupoa hadi alipotangazwa mgeni mwingine ndipo hali iliporudi kama awali.

Mbunge wa Arusha ameendelea kutomtambua "Meya" huyo kwa kumtambulisha kama diwani huku akimwomba Mh. Sitta kuongea na wakubwa wake ili wakamilishe haraka kuumaliza mgogoro uliopo kupitia kamati iliyoundwa na Pinda na Mbowe.

Ninachojiuliza ni kwamba, ni lini atapata hekima ya kujiuzulu hiyo nafasi ili apate tena heshima kwa jamii ya Arusha. Licha ya kampuni yake ya ujenzi kufanya miradi mingi ya kanisa hilo kabla ya mgogoro huo, waumini hao hawamdhamini tena kama awali. Poor him!

acheni unafiki jameni hiyo misa nilikuepo wala hayo unayo ya creat hayakuepo, laiti ungelijua ni jinsi gani huyo unaemwita meya feki alivyo changia nguvu zake na kwenye hili kanisa.
 
ALIYEKUWEPO KATUMA HIVI

Jamaa si member wa JF nawe nakuomba ufanye jitihada za kuwasiliana naye au wasaidizi wake uweze kumpa huu ujumbe .Hapa JF tunajadili tu
 
"haki tutaitafuta by the ballot or the bullet" Lema (via Martin jr wa Jf)... Hii kauli haijakaa vyema, inaweza kuwapa CCM credit kwa dhana kwamba CHADEMA ni chama cha fujo, watch out guys..!
 
"haki tutaitafuta by the ballot or the bullet" Lema (via Martin jr wa Jf)... Hii kauli haijakaa vyema, inaweza kuwapa CCM credit kwa dhana kwamba CHADEMA ni chama cha fujo, watch out guys..!

Ili ccm wawe sahihi kwa hili wasiibe kura, waache kura ziamue, wakiiba kura bullet must be the next option, kamwe haitatafsiriwa kuwa kupenda fujo.
 
Mbele ya Askofu mkuu Josephat Leburu, Mbunge wa Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta .Mbunge Lema ashikana mikono na mkuu wa mkoa wa Arusha na Meya wa Arusha. Lema akihaidi hadharani hana chuki na mtu yeyote binafsi ila hata choka kupigania haki kama haki haita tendeka katika jamii. Amemwomba Mbunge huyo wa Afrika Mashariki kumaliza mgogoro huo mapema. Wadau toeni mchango wenu katika hili.

Hilo si jipya kwani CHADEMA wanawaogopa wafadhili wao 'kanisa' hivyo ni lazima wawasikilize.

CCM shule ipo, nao hawkuona jingine ispokuwa kutumia udhaifu huo. Mwalimu sijui alikiachia nini chama hiki, pengine kale kafimbo hakakuzikwa naye bali kapo ikulu kakifanya vitu vyake.

Sasa mchezo umekwisha!
 
wamekufadhili wewe pia kumbuka shule zao, hospitali zao na wakufunzi kibao waliojaa nchi nzima wamesoma shule zao na hata waalim waliokufundisha chuoni kama uliwahi kukanyaga walifadhiliwa na wao kwahiyo kwa namna moja ama nyingine wamefadhili asimilia kubwa ya watanzania kama siyo kaka basi dada na kama siyo shangazi basi mjomba. kiumbe uliyekosa fadhila we, leo unajaribu kulipakazia kanisa baada ya miaka chungu mzima ya huduma zao kwa jamii.
 
Sasa mkuu kama uelewa wako ni mdogo na finyu ungeonaje upatanisho hapo. Hapa ni kwa great thinkers sio kwa wenye uelewa mdogo na finyu.
 
Sunday, 04 December 2011 20:37

Filbert Rweyemamu, Arusha

HARAMBEE ya ujenzi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu, Tereza katika Jimbo Kuu la Arusha, jana iligeuka uwanja wa kupigana vijembe vya kisiasa na njia ya kuelekea mapatano ya mgogoro wa umeya wa jiji hilo ambao umekuwa chanzo cha machafuko kwa muda mrefu.

Mgeni rasmi katika harambee hiyo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, ndiye aliyekuwa chachu ya upatanisho huo, pale alipowakutanisha Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema na Meya wa jiji hilo, Gaudence Lyimo na kuwataka waache tofauti zao.

Sitta aliwataka Lema na chama chake cha Chadema kuacha kudai wanachokitaka kwa maandamano na vurugu kama chama kinachotaka kushika dola, badala yake aliwashauri wajenge siasa za kuvumiliana.

Dalili za siasa kutawala harambee hiyo zilijionesha mapema baada ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu kufika kanisani hapo na Sitta kusimama na kusema "taifa linahitaji viongozi vijana kama Nyalandu."

“Vijana kama hawa tunawahitaji sana, wakiungana na mbunge wenu mheshimiwa Lema, wanaweza kuleta mabadiliko ambayo ni muhimu sana katika kizazi hiki kwani Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana na Mungu,” alisema Sitta huku akishangiliwa.

Baada ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kukaribishwa na Sitta na kisha kuwasalimia waumini na wananchi waliofika kwenye harambee hiyo, alisema anamheshimu sana Sitta kutokana na uwezo aliounyesha wakati akiwa Spika wa Bunge la Tisa.

Lema alidai hana ugomvi binafsi na Lyimo bali utaratibu uliotumika hakubaliani nao na atahakikisha anasimamia hilo hadi ufumbuzi upatikane.

Awali, Waziri Sitta alisema hakuja Arusha kuongoza harambee hiyo kwa lengo la kujisafisha kama wanavyofanya wengine kwa kuwa anaamini kuwa yeye ni mwadilifu.

“Ndugu zangu sikuja kujisafisha kama wanavyofanya wengine, kwa kuwa sina sababu ya kufanya hivyo. Nyie mnajua watu waadilifu sihitaji hata kuwaambia,” alisema Waziri Sitta.

Januari 5 mwaka huu, Chadema kiliongoza maandamano ya kitaifa yaliyopoteza maisha ya watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa, wakipinga Gaudence Lyimo kuwa meya huku viongozi wa Chadema wakifunguliwa kesi ya kufanya mkusanyiko bila kibali.

Vingozi wengine waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo,Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi na wafanyabishara mbalimbali.

Code:
"Ndugu zangu sikuja kujisafisha kama wanavyofanya  wengine, kwa kuwa  sina sababu ya kufanya hivyo. Nyie mnajua watu  waadilifu sihitaji hata  kuwaambia," alisema Waziri Sitta.
Hii ni kali!
2015 races at maturing stage!
 
Mh S.Sitta akiwa ktk harambee Mjini Arusha.Ameombwa na kutafuta amani ktk mji wa Arusha kwa kuwapatanisha Mbunge Mh Lema na Meya wa Mji wa Arusha,na akachukuwa jukumu hilo kama ambavyo picha inavyojieleza.
Nawasilisha

Eeeh hii kiboko kweli nabii hakubaliki kwao,wakati wakatoliki wa mwanza wanamuona lowassa ni lulu wa nyumbani kwao arusha wanamuona si lolote si chochote na kumkimbilia mzee samuel sitta!hii si habari njema bwana lowassa....
 
Mbele ya Askofu mkuu Josephat Leburu, Mbunge wa Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta .Mbunge Lema ashikana mikono na mkuu wa mkoa wa Arusha na Meya wa Arusha. Lema akihaidi hadharani hana chuki na mtu yeyote binafsi ila hata choka kupigania haki kama haki haita tendeka katika jamii. Amemwomba Mbunge huyo wa Afrika Mashariki kumaliza mgogoro huo mapema. Wadau toeni mchango wenu katika hili.
Kichwa cha uzi kinasomeka 'kanisa lawapatanisha...' lakini habari yenyewe inasema hawajapatana bado, bali walikwenda kushikana mikono tu. Kiukweli wanasiasa wetu watz hawaaminiki. Kazi yao ni kukaribishana juisi, kushikana mikono na kuuza sura kwa kuchekacheka tu. Hakuna cha maana hapo, ni kupotezeana muda tu. Mb. Umeitwa na askofu wako upatanishwe na RC na Meya, badala yake unamwomba mb. mwenzio aumalize 'mgogoro' mapema, ww umeshindwa nn! Siasa zingine ni uchwara kweli.
 
quote_icon.png
By Sangarara
Anakunywa Maji kidogo, kisha anaendelea
Pale Kenya pale, wakati wa mchakato wao damu imemwagika pale, sasa mimi siko tayari kuona hili linatokea hapa,na ndio maana hata kwenye swala la madiwani wa arusha, mimi niliwaelekeza Waziri Mkuu na Katibu wangu Mkama kuhakikisha Mnakaa, mnazungumza na kulimaliza hili, lakini kinachoendelea pale mi hata sikielewi nikiuliza naambiwa tatizo ni Lema, vyombo vya habari kwanza vilikuwa vinasema tatizo ni Chitanda, sasa Chitanda simsikii tena naambiwa tatizo ni Kamanda wa Polisi Zuberi na Mkuu wa Mkoa, mimi sielewi kabisa nini kinaendelea Pale, na hali hii inachafua kabisa picha ya nchi yetu uko nje.

Ninacho kiona hapa kuna watu ambao huu mgogoro una maslahi kwao ndiyo maana hawataki kuumaliza kwa makusudi mazima ili hali uwezo wa kuumaliza wanao tena mkubwa tu

Siasa za namna hazionyeshi kuwa tumekomaa bali ni wachanga sana ktk siasa Mapema sana EL alishauri viongozi wakae wayamalize haya kwa mazungumzo mezani lakini wajinga wachache hawataki sasa tuangalie madhar yake

  • watu wamekufa
  • madiwani wamekuzwa uwakilishi wa wananchi
  • maandamano yasiyo koma mioyoni mwa watu na barabarani
  • tunapoteza pesa ambayo ingeingia kwa utalii
  • heshima ya nchi inapungua na hasa Arusha
  • gharama za uchaguzi mwingine wa madiwani
  • hatujui nini kitatokea kwenye uchaguzi wa madiwani (Mungu aaepushie mbali yote yasiyo stahili)
yote haya na mengine mengi yanazalishwa na kutukufuata taaratibu za uchaguzi wa MAYOR tu !!!!
 
Huo ndo unafiki wa kisiasa ambao umeanza kufanywa mbele ya nyumba ya mungu,ee mungu wasamehe maana hawajui walitendalo
 
Nani amemteau kuwa msuluhishi wa suala hili?au ndo yaleyale ya samaki kujifanya ana ngozi soft kwa kuteleza huku bado yuko kwenye kundi la wenye magamba??
 
Mimi nilikuwepo na habari ilikuwa kama ifuatavyo , Mb Arusha mjini ( Lema) alipewa mic na Mh Sitta asalimie wananchi na kuchangia harambee hiyo na Bwana Lema , alimtambua Meya feki kama Diwani wa Olorieni na siyo meya huku akisisitiza kuwa yeye hana ugomvi binafsi na Meya isipokuwa mfumo uliompata meya unamfanya meya huyo kuwa katili wa haki za binadamu na utu .

Nukuu Lema " Mh Baba Askofu na mgeni rasmi mimi kama mbunge nitakuwa mtu waq ajabu kama nitashindwa kusimamia haki mbele ya madhabau hii ya Mungu na hivyo ukweli unabaki kuwa Arusha mjini hakuna Meya na mimi mbunge simtambui meya ila natambua uwepo wa Diwani wa Kata ya Olorieni bwana Gaudensi Lyimo.

Naomba ileweke kuwa mimi sina ugomvi binafsi na Bwana Gaudensi na hata akitaka kunywa chai kwangu namkaribisha sana isipokuwa nimuombe tena Mh Sitta kama mzee wetu kwenye siasa muda mrefu awaambie wakubwa wengine hasa waziri mkuu kwamba tatizo hili si afya kwa Arusha lakini hata hivyo hatutarudi nyuma kupigania haki iliyoporwa katika uchaguzi wa umeya na kama kuna mtu anakerwa na mgogoro wowote unaotafuta hakli basi yeye aendelee kukerwa na sisi kwetu ni baraka kwani haki tutaitafuta by the ballot or the bullet.

Back
Top Bottom