Sitta ajitosa mgogoro wa Umeya Arusha

Tutofautiane kwa hoja si mapanga.. Hii ndio demokrasia tunayotaka.. Tukianza kutosikilizana kisa itikadi zetu zimetofautiana tutakuwa tunajichimbia kaburi letu wenyewe.

Tucheke na tunywe juice pamoja kudumisha Utanzania wetu.. But Hoja ya msingi ijadiliwe kwa maslahi ya taifa letu

Think Big
 
title na ulivyoviandika havishabihiani kabisa
Hata hivyo bado tunaombea sana amani ipatikane Arusha Kama alivyosema mkuu tatizo hata yeye halijui maana aliagiza wakae walimalize lakini kuna wachache kwa masilahi yao hawataki
 
Hakuna urafiki kati ya binadamu na nyoka. CCM ni nyoka na stahili ya nyola ni kupondwa kichwa mpaka afe. Hakuna amani wala haki Tanzania hadi CCM iondoke madarakani. CCM NA JANGA LA KITAIFA.
 
haikuwa sehemu ya tutakiane amani, ilikuwa ni wkt wa kuchangia harambee ya ujenzi wa cathedral mpya Arusha. nampongeza lema kwani alitambua uwepo wa meya, mkuu wa mkoa kakiri ni mara ya kwanza kumwona live lema,Lema alimshika mkono Mkuu wa Mkoa alipomaliza hotuba yake,lkm meya bila aibu wkt anajitambulisha hakumtaja lema kama walivofanya wengine. Sita nampongeza pia kwa kukubali kuwapatanisha lkn kushikana kwao mikono haimaniishi Lema kakubali kuwa meya kachaguliwa halali,Cha muhimu amani iwepo arusha. (yote haya nimeyasikia radio maria ndo walokuwa waanrusha live ibada hiyo)
nawapigia debe tujitolee ujenzi wa hilo kanisa litakaogharimu bil 5 na mil 800 hivi kama sijakosea.
 
Kupatana ni sawa lakini haki itendeke namwuunga mkono mh mb Lema kuwa hatachoka kutetea haki
 
hicho kichwa cha habari sijakielewa...! Kushikana mikono haimaanishi ndiyo mmepatana. Ikulu watu hawakuishia kushikana mikono tu...watu walichekeana kama ngedere na kuna wakati Mkulu mwenyewe alikuwa anatoa huduma za juice kama beki tatu....je walipatana?

Muwe na ukarimu kwa wageni pindi wanapowatembelea majumbani kwenu, hata kama hamuwapendi.
 
Exegate kidogo hichi kifungu cha mandiko. Tunashindwa kuelewa kwamba ni nani hasa alifunga hapa duniani ni wana wa Arusha au ni serekali ya CCM. Iliyomteua diwani huyo kuwa meya wakitumia kivuli cha uchaguzi geresha, a.k.a usanii wa kishamba.

Mi nadhani wamefunga wa2 wa arusha na wanaharakati wote kwa ujumla kwamba,magamba no, wamefungiwa,i think thats t
 
Hakuna urafiki kati ya binadamu na nyoka. CCM ni nyoka na stahili ya nyola ni kupondwa kichwa mpaka afe. Hakuna amani wala haki Tanzania hadi CCM iondoke madarakani. CCM NA JANGA LA KITAIFA.

Ndoto za mchana zina raha yake bwana. Endelea kuota tu kwakuwa hiyo nayo ni sehemu ya afya ya mwanadamu. CCM ikiondoka nani atawale?
 
Kwa uelewa wangu mdogo na finyu, hapa sioni upatanisho zaidi ya kuzingatia itifaki. Upatanisho hutokea baada ya mazungumz ya upatanisho kufanyika. Mazungumzo hayo hufanywa kwa watu au kikundi cha watu waliogombana au kutokuelewana ktk jambo fulani. Ili kuweza kutoa suluhu ya tofauti zao, ni lazima wakubali kuwa wanatofautiana, wakubali kusuluhishwa, wamkubali msuluhishi, na mwisho wakubali sehemu ya kusuluhishwa. Hili sioni kutokea Arusha kama ambavyo inasemwa hapa.
 
Back
Top Bottom