Sitta ahoji harambee za Lowassa Makanisani na sasa misikitini

Sitta ahoji harambee za Lowassa Makanisani na sasa misikitini

Swali moja halijajibiwa;
Kwa nini hao rafiki zako wasichange moja kwa moja Kanisani au Msikitini na badala yake wakuchangie wewe?
Usiwafanye watanzania wajinga.Nyuma ya pazia unataka urais na hao wanaokuchangia wataifilisi nchi kama ikitokea ukawa rais.Mbona humtaji Rostam na mafisadi wengine?
Wanaokuchangia wanapoteza fedha zao bure kwa sababu huwezi kupata urais.Umechafuka sana wewe.

ANAYEKIMBILIA IKULU MWOGOPE KAMA UKOMA - Mwl Nyerere
 
sitta naye ni wale wale.hivi unakumbuka suala la MKEWE BI MAGRETT SITTA kukamatwa na takukuru akitoa rushwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2010,wakati wa kampeni za ndani ya chama chake CCM,SITTA aliwaka ohh mke wangu awezi toa rushwa,sasa kama umeshindwa rusha katika kitanda unacholalia utaweza katika TAIFA lote?Tafakali kumbe hata SITTA naje hana sifa ya kuwa mgombea urais
 
Na mimi namhoji Sitta. Kwanini alihitimisha ile hoja ya Richmond kihuni? Alitaka kumwudhi nani au kumfurahisha nani? Kwa kuwa hana msimamo hana moral authority ya kumhoji Edtwalib.Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Wakati mwingine ni vigumu kumuelewa Mh.6, kwa nini yuko obsessed na Edtwalib - mbona hata na yeye ana kawaida ya kutoa maoni yake kanisani wakati mwingine anazungumza as if hayuko kwenye Cabinet ya Mh.Kikwete - kwa nini ahondoki ndani ya baraza la mawaziri la JK alafu akawa free kuzungumza atakalo. Nani ambaye hajui alikuwa na ambition za kuwania uwaziri mkuu, alipo hukosa ndio akatafuta mbinu za kumuondoa Lowassa kwa kisingizio cha Richmond - wakati ukweli wa mambo Lowassa alikuwa ni mtekelezaji tu sio mtaalamu na bila Mtambo wa Richmond kufua umeme nchi hii ingepata hasara kiuchumi na mitambo hiyo bado inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa mpaka leo. Looking back now naona Mh.Lowassa was right all along aliposema kinacho tafutwa si Richmond bali ni Uwaziri mkuu. Mbona wakati fulani Mh.Sita alitaka kuzima kashfa ya ufisadi wa EPA alisema hawezi kufanyia kazi mambo yanayo andikwa mitandaoni!! Alipo gunduwa kuna mtaji wa kisiasa katika kizungumzia Ufisadi/EPA basi akawa mstari wa mbele na kikundi chake kuzunguka Tanzania nzima wakisingumzia EPA na Ufisadi kasahau kwamba aliwahi kubeza mambo ya ufisadi/EPA alipo kuwa Spika. Lowassa kama binadamu wengine anaweza kuwa na mapungufu yake laliki at least huwa ni mwepesi wa kutoa mahamuzi na kuhakikisha yanatekelezwa, azungumzie sera zake lakini sio kila siku kutafuta mbinu za kumchafulia mwenzake, mbona hatujawahi kumsikia Edtwalib akimsema SITA mikutanoni au Kanisani.
 
Mpaka 2015 tutashuhudia sarakasi za ajabu, pale zitakaporukwa kwa kutumia ulimi na masikio!!!! kwi kwi kwi kwi kwi.
 
Kambi za Urais CCM zina makubwa zaidi ya haya,tusubiri tu!!!
 
Wote wanautaka urais. Lowasa anachowazidi wenzie ni kidogo sana. Wao wanaongea weeee yeye anatenda. Mwisho wa siku vitendo vinadumu muda mrefu kuliko maneno. Hata kauli ya waswahili kuwa mkono mtupu haulambwi nayo ina mashiko.
 
usimsingizie mtumishi wa Mungu mambo ya EL. hakuahidiwa kushinda urais wala nini, TB kamwambia nenda karudishe ulivyopora na Mungu anaweza kukurehemu. sasa unataka kuniambia ndio kamwambia utakuwa rais?!
mengine aliambiwa private, umemwona tena anarudi huko? kaamua kumpotezea pasta, kule chemba alimchana noma

Kuna ushahidi japo wa youtube video ku-justify your statement in bold above?
 
Gombaneniii weee, ila cha msingi mtukabidhi nchi yetu 2015.
 
kelele na kulialia kwa Sitta kunamfanya Lowasa akubakike zaidi. sitta naye mnafiki tu anachangia kuiua ccm
 
Me cna tatizo na hawa wazee wote wawili,naamini miezi 3 tu ya mwanzo ya Urais wa Dr.slaa,watakuwa wamebaki masikini kwa kurudisha utajiri wote waliotuibia.Acha wavutane tu lkn hz kauli mwisho wake 2015.
 
Maskini Sitta amesahau mara hii kwamba yeye mwenyewe juzi juzi tu alitoa mchango akisema amechangiwa na marafiki zake akina Membe, Magufuli na wengine. Baadaye magufuli alimkana.

Mwaka 2010 pia alikuwa anapita kwenye majimbo yake na wale aliokuwa anawaita wapiganaji wa ufisadi akitoa michango makanisani na kwamba ni pesa zake na marafiki zake.

Hivi kweli Sitta kayasahau hayo?
 
Uchungu wa ufisadi alionao mzee Sitta siku zote umekuwa selective!Pale Lowassa anapohusika ndipo Sitta hujifaragua na upambanaji wake fake wa ufisadi.

Yeye ni mpinga Lowassa na tayari amezidiwa kete na Lowassa.Asitafute huruma kwa kujivika upambanaji fake kama alivyozoea.Hapendi ufisadi ajiuzulu uwaziri na ikiwezekana kujitoa ccm.Vinginevyo ni kufikiri wote ni wajinga!

Katibu wa Lowassa amemjibu huyu Sitta vizuri sana.
 
sitta ni mnafiki mkubwa, hana lolote, kwanza jambo mpja tuelewa Lowassa htoi pesa nyingi, yeye aweza toa milioni 5 au kumi kisha akahamasisha watu wengine wachange na mpaka pesa inafika milioni mia tano, so pesa hizo wala si za Lowassa

PIli kama kufanya harambee, Sitta ni mlutheri, Lowassa Mlutheri, Sumaye Mlutheri na kwa kanisa hili kama mjuavyo minada na harambee ndio nyumbani, kama anataka si awe nkwenda kwenye makanisa ya KKKT na kutoa michango yake?

Tatu, Lowassa hajipeleki kwenye matukio bali watu wanamfuata ssa kama hawamuoni yeye Sitta na wanamuona Lowassa, ajue hana nyota, huwezi kulazimisha watu wakupende, awe mpole tu
 
Tuache upinzani na uongo kukwepeshwa,Lowassa ni hatari/Janga sana kwa Taifa,ambition aliyonayo anaweza hata kuua kwa ajili ya Urais 2015,na ndo kete aliyobaki nayo tu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ndio kete pekee inayotafutwa,
 
Sitta ----- tu, mbona yeye anaiuwa East Afrika kwa uzembe na ubwege wake, tangu lini vikao vinafanywa kwa siri bila Tanzania, kasababisha tudharauliwe. yeye afanye yake tuone, sio kuwashambulia kiunafiki na uchoyo wenzake.
 
Sita nae alishaishiwa tokea wamtoe kuwa spika amabaki kama debe tupu tu kwa hiyo lazima lilolome kwa vyovyote vile.Siku likijazwa maji hata kama yawe maji machafu linatulia tuli.That is what we call politics,hivi unamkumbuka Nape Nauye wakati unagombea jimbo la Ubungo kura za maoni kupitia CCM huku akishindana na Shamsi Mwangunga na yule dada mwingine aliewashinda sijui alikuwa mkuu wa wilaya za Shinyanga.Nape alikuwa akisema kuwa wanaCCM wasikubali kuhongwa hela za swala na tembo za Mwangunga eti kwa sababu alikuwa waziri wa utalii.
Kwa kusema hivo Nape alikuwa anajua kuwa wanyama wetu wanapigwa na kuuawa isivo halali huko mbugani na pia vitalu vya uwindaji vinagawiwa kwa rushwa.Ebwana si jamaa wakamnyamazisha kwa kumpatia ukuu wa wilaya sijui Newala na walivomupatia huo ukatibu mwenezi ndiyo jamaa kimya kabisa mdomo umepigwa super glue na juzi wakati wanyama wanapelekwa Quatar Nape hakufungua mdomo.Kwa upande wangu Nape alitakiwa aende mahakamani kutoa ushahidi wa wanyama kutoroshwa kwa sababu analijua dili lote.So in short that is the politics my brother wala usimwamini huyo debe tupu Sitta
 
kwani we unaona nigeria ni el mwenyewe ndio ana uwezo wa kwenda? mbona kulikuwa na kadamnasi ya kutosha ya watz akiwapo kule! hakuna siri mkristo hapo

Hata mi nimeenda mkuu! Na wala hakuambiwa atakuwa rais, ni uzushi 2 wa watu
 
Wrong advice, wrong strategy! We all know kwamba uhaba wa makanisa au misikiti sio among major issue zinatukabili kwenye jamii zetu. Ukimjengea mtanzania kanisa au msikiti humtatulii matatizo yake yanayomkabili hapa duniani. Mtu mgonjwa ambaye anaishi sehemu ambayo hakuna dawa wala zahanati au mwenye njaa hawezi kwenda kwenye nyumba ya ibada, hata akienda mawazo yake yatakua hayapo hapo. After all, ibada inakubalika ikifanyika popote pale iwe chini ya miti au kwenye uwanja wa mpira! Whats the point watu kujazana kanisani na msikitini kama hawajui kusoma? Kwanini usiwajengee shule au zahanati? Kwanini usijaze madawa kwenye zahanati zao na kuwanunulia madawati watoto wanaokaa chini au kuwajengea darasa wale wanaosomea chini ya mti? Hizi harakati za EL zingekua na maana kama zingeelekezwa kwenye utatuzi wa issue kubwa zinawakabili watanzania wengi badala yake anatumia effort kubwa kufanya mambo ambayo hayasaidii kuboresha maisha ya walalahoi wengi ambao ndo anategemea wampigie kura. FAIL! FAIL! He should sack his advisers.

Naunga mkono hoja!
Angekuwa na washauri wa kumshauri kufanya mambo haya tungekuwa mbali na tungempigia kura bila tatizo
 
Back
Top Bottom