Sitasahau mwaka 2002 ndugu yangu alipochunwa ngozi wilaya ya Mbozi wakati huo ilikuwa mkoa wa Mbeya

Kuna mambo ukiyaskia alafu anayeyafanya ni mwenzako tena wakati mwingine ni ndugu yako unahisi kuchizika na kujiuliza kwa nini ulikuwa mtu mweusi. Sijui ni laana gani sisi watu weusi tulipewa. Afrika tuna matukio ya ajabu sana.
Nenda kwa wazungu ukutane na serial killers kuna mama Australia alichemsha kichwa cha mumewe kama anachemsha kongoro
 
Mbozi ndio sehemu inayoongoza kwa matukio ya Kinyama

Miaka ya 2000's kuna jamaa huko mbozi ndugu yao alipigwa mpaka akafa na sababu ilikuwa ni mwizi sasa familia iliyoshiriki kumuuwa yule jamaa baada ya siku mbili ikavamiwa na ndugu wa Marehemu ambao ni Wanyiha wako na mapanga, lungu Mashoka wakenda wakaanzisha tifu kwaajili ya kulipiza kisasi

Aisee ndugu wa jamaa aliyeuwawa wakafanikiwa kumkamata mtu mmoja wa familia ile iliyotekeleza mauaji walichokifanya ni kumkamata na kumfunga kamba ili asiweze kukimbia

Kilichofuata jamaa wakammbeba kwenda kumzika mzimamzima ili kulipiza kisasi cha damu ya ndugu yao

Upande wa jamaa ambao ndugu yao kaja kukamatwa wakaenda polisi kutoa taarifa kuwa tumevamiwa na watu na wamemchukua ndugu yetu polisi fasta wakatoka na defender kwenda kuwafuatilia jamaa

Mwisho wa siku polisi na ndugu wa jamaa waliambiwa ndugu yao ameshazikwa mzimamzima baada ya kwenda kumfukua kwa bahati mbaya ikawa tayari ameshatangulia mbele za haki

Jaman hivi nyinyi wanyia na watu wa Mbozi, Mlowo, Vyawa nyinyi ni wabongo au wazambia? Maana mnaroho ngumu sana
Duh Jaman watu wana roho sio za dunia hii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binti yangu alikua na miaka 7 kipindi kile. Alimuona yule marehemu ITV. Ilikua vigumu sana kumkonvins akalale chumbani kwao.
Hata mtu mzima ulikua huangalii mara 2.
Ndio maana polisi walio wengi wanapata tabu sana wakati wa kufa.
 
Huyo boss ni Ch...la aka I..si? Au mwingine?

wanajifanyaga ka mazoba flan hivi.hawa watu bwana nawachekigi hata hapo kariakoo.Usikute tayari alishafirisika au alishakufa.Kumbe mali za hovyo kabisa hizo.bora tubaki na mia mia zetu za kuunha unga
 
Unawapenda wanyaki ehee!?

Kwa taarifa yako mambo ya kuchuna ngozi na nondo yalikua yanafanywa na Wanyiha.

Wanyakyusa wanapatikana Rungwe na Kyela, Huko Mbozi ni kwa wanyiha
Kumbe! Hilo kabila ndo nalisikia leo.

Likely litakuwa subset tu kama ilivyo ntuzu au wadakama kwa wasukuma.
 
Mbozi kwa matukio wapo vizuri, na Makanisa yamejazana ova Gesti Bubu Songea.
 
Mwaka 2002 mkoa wa Mbeya kabla haujagawanywa kuwa mikoa miwili yani Songwe na Mbeya ilikuwa asubuhi nilipopokea simu kunitaarifu kuwa ndugu yangu amekutwa amechunwa ngozi kijiji cha Isansa wilaya ya Mbozi.

Nilikurupuka kwenda eneo la tukio nikakuta watu wengi wakisubiri polisi wafike. Nilipomtazama mwili wake wote ulikuwa mwekundu na hakuwa na jeraha lolote zaidi ya uvimbe kisogoni.

Ngozi ilivuliwa kuanzia shingoni hadi miguuni kama nguo vile maana walivyokuwa wanachuna unapigwa na kitu kizito kichwani kabla haujafariki wanakuchoma sindano ngozi inaumuka inaachana na mwili hivyo wanakuja kukata shingoni na huku mikononi alafu wanaivua kama nguo huku ukiendelea kutapatapa. Baada ya hapo wanaiweka dawa isiharibike then wanasepa hivyo tulikuta ashafariki muda mrefu.

Polisi walikuja na kuruhusu tukazike. Baada ya siku nne wale wachunaji walikuwa wako Vwawa ambayo sasa hivi ni makao makuu ya mkoa wa Songwe Wilaya ya Mbozi.

Walikuwa guest house wakisubiri wafanye biashara USD 30,000. Wakati mhudumu wa guest anafanya usafi akasikia harufu isiyo ya kawaida na kwenda kuripoti ndipo walipokamatwa na kupelekwa kituoni.

Ngozi ilikuwa imehifadhiwa kwenye kopo. Wengi tulikusanyika kushuhudia lile tukio, wakaitoa nje watu tukaiona.

Taarifa zikasambaa kuwa kumbe ni boss mmoja pale Vwawa ndiye ilikuwa biashara yake. Alikuwa na vituo vya mafuta, shule, magari nk

Inaaminika Polisi walipoenda akawapa bakishishi wakapiga kimya. Matukio ya uchunaji yaliendelea baadaye yakapotea hadi leo. Wapo waliodai ngozi ile ilikuwa inauzwa Congo.

Hadi leo sijui wale watuhumiwa walifungwa wapi lakini sasa hivi ni full amani hakuna tena uchunaji.
Chaula nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom