Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe: Nashangazwa na wanaume wanaojiua kisa mapenzi wakati sensa inaonesha wanawake ni wengi kuliko wanaume

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amesema anashangazwa na Wanaume wanaojiua kwasababu ya mapenzi wakati Sensa inaonesha kuwa Wanawake wako wengi nchini kuliko Wanaume hivyo wanaweza kuoa zaidi ya Mke mmoja.

DC Mahawe amesema hayo leo Jumatatu Mei 8, 2023 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mbozi.

DC amesema "Mimi nawashangaa Wababa, ujue kwenye Sensa nyinyi ni wachache kuliko Wanawake sasa unamuuaje Mwanamke au na wewe unaanza kujiua wakati Wanawake wengine wanakusubiri kule ukawaoe?"

"Sisi tunataka hata mchukue mbilimbili au tatutatu lakini wewe unamuua Mwanamke halafu na wewe unajiua kwa sababu ya Mwanamke!, sio sawa Wanaume acheni kuuua Wanawake na kujiua kisa mapenziL

DC pia amewataka Wananchi wa Kata ya Nambozi kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.
 
Kipo kikundu kilichoshikilia ufahamu wetu wa kuoa mojamoja mbilimbili mpaka nnenne
 
Yuko sahihi. Wanaume wengi hufanya upumbavu wa kufikia kujiua kwa sababu za kijinga sana.

Kosa la kwanza mwanaume kufanya ni kumpenda mwanamke, mwanamke pekee unaetakiwa kupenda ni mama yako tu.

Kumpenda mwanamke ni kuweka rehani moyo wako, wanawake ni watu wanaongozwa na hisia zaidi, any time hisia zake zikimwambia hakutaki ama zikibadilika anakuacha ghafla. Kama ulikua unampenda utajinyonga tu.

Kosa la pili na kubwa zaidi mwanaume unafanya ni kua na mwanamke mmoja na unampenda yeye tu. Hapa unakua umebeba mayaii yote kwenye bakuli ama kapu moja, yakianguka yanavunjika yote.

Mwanaume hakikisha hufanyi hayo makosa mawili hapo juu vinginevyo utaishia kulia mapenzi yanauma na utajiua tu.
 
Back
Top Bottom