Sitarudia kutumia usafiri wa meli

Acha uongo spice islander ilizama 2011
Kweli kabisa. Nakumbuka vizuri hii ajali ilitokea mwezi wa tisa mwaka huo 2011 ambapo inasemekana zaidi ya watu 1,500 walipoteza maisha. Hadi hii leo ajali za vyombo vya usafiri majini zilizotokana na vyombo hivyo kujaza abiria kupita uwezo wake hazijatupa somo la kutosha.
 
Wajuba dah kweli tuko tofauti sana sijawahi kuwa na Hofu kabisa na Maji kwa ujumla japo sio mzoefu wa kusafiri Majini ila sioni hatari kufanya ivo na wala sina shaka yoyote niwapo chomboni kwangu usafiri wa Maji naona ni safest zaidi
 
Usafiri Mgumu Labda Ziwa Tanganyika, Victoria, Nyasa,
Lakini Kwenda Zanzibar Kuna Boti Nzuri Za Kisasa
Ambapo Ukiwa Ndani Utulivu Ni Mkubwa Sana
Kilimanjaro IV(Pearl Of Stone Town)(Pride Of The Union)


Nilianza Kwenda Zanzibar 2011 Boti Za Wakati Ule Zilikuwa Bora Ila Nilipokuja Kwenda Tena Unguja Zikawa Nyingine Nzuri Zaidi
 
Umenikumbusha safari moja nilikua naenda Unguja, jamaa niliyekua nae jirani alikua akilia kwamba angejua angepanda ndege ,
Tulipigwa na dhoruba kali sana , sema safari za maji zinataka moyo
 
Hamna raha kama kukwea flying horse inayolala baharini usiku kucha...
Ile boat nilipanda siku moja sababu ya dharura tu ila kwa experience niliyoipata nilifika Dar nimechoka, nitaipanda ikiwa kuna dharura tu usafiri bora kwa binadamu ....
 
Maji hapana aise. tunapanda tu kwasababu ya harakati za maisha ila maji sio kabisa. maji mazuri niyakwenye ndoo tu.
 
Mm mara yangu ya kwanza kupanda hivi vitu vya majin nakumbuka ilikua 2015 nilifika mwanza kwa mara ya kwanza ikatakiwa nielekee sehem moja inaitwa sengerema hapo ikanibidi nipande kivuko nilienda kukaa karibu na zile boya
 
Wakuu,

Nilikuwa sijawahi kusafiri majini kwa kutumia meli ama boti.

Weekend nikasema ngoja nitoke Mwanza to Ukerewe (Nansio). Aisee hapana.

Chombo kilikuwa kinayumba yumba majini safari nzima , na kila nikitizama huko nje naona milima ya maji tu na mawimbi. Kuna mahala niicheck kila upande sikuona mji wala watu, ni maji tu tena mengi balaa.


Nilihofia sana aisee. Wakati nageuza jana nilisafiri roho juu mno. Kufika tu Mwanza nilipiga Serengeti Lite baridii kwanza ili kukata kiu.

Nini raha ya usafiri wa majini?

Aisee hapana.


Nitafia nchi kavu aisee. Maji hapana.
Ukipanda meli ziwa Victoria june to september, tegemea kutapika na kuhara kama una karoho kepesi... huu msimu sio
 
Wakuu,

Nilikuwa sijawahi kusafiri majini kwa kutumia meli ama boti.

Weekend nikasema ngoja nitoke Mwanza to Ukerewe (Nansio). Aisee hapana.

Chombo kilikuwa kinayumba yumba majini safari nzima , na kila nikitizama huko nje naona milima ya maji tu na mawimbi. Kuna mahala niicheck kila upande sikuona mji wala watu, ni maji tu tena mengi balaa.


Nilihofia sana aisee. Wakati nageuza jana nilisafiri roho juu mno. Kufika tu Mwanza nilipiga Serengeti Lite baridii kwanza ili kukata kiu.

Nini raha ya usafiri wa majini?

Aisee hapana.


Nitafia nchi kavu aisee. Maji hapana.
Mkuu samahani, wewe ni msukuma???
 
Aisee umenikumbusha safr yangu ya mwaka 2013 kutoka Dar kwenda Zanzibar (Unguja).

Mwanzo niliogopa sana mpaka kutaka kuhairisha safr lkn nilijaribu kuwashawishi wanibadirishie kituo cha mazoez yaan field mwalimu akagoma kabisa, ikumbukwe wakati huo meli ya spices imetoka kuzama kama wiki moja imepita, aisee siji sahau safr ile.
Kwani rafiki yangu tuliye pangiwa sehemu moja alinitia moyo kwamba yeye kusafr kwenye maji anajisikia ni salama zaidi kuliko kwenye nchi kavu yaan kusafr kwa gari.

Eeh bwana, tukafika Dar tukitokea Moro tukakata tiket kwenye Boti ya Kilimanjaro by that time ilikua ni meli bora zaidi maana inasemekana imetengenezwa kisasa zaidi. Ni kweli mle ndani ilikua kama mpo loyal sana.

Safari ikaanza eeh bwana eeh nilijitahidi kuzuia macho yasitazame nje maana niliona kama vile ndo naenda kufa nikasali sala yangu ya kuomba toba ili kama siku ndo imefika basi nipokewe na malaika huko mbinguni.

Njiani tuliona boti ndogo zikiendelea kutafuta miili ya watu kufuatia ajali ya spices.

Mungu mwema tulifika salama salimini Unguja, tukaweka kambi Madizini siku nyingin tukawa tunaend Bweleo huko aisee ni waislamu asilimia 95 lkn ukweli niliwapenda maana walikua wakarimu kwetu kwa kiasi kikubwa.

Mziki ukawa siku ya kurudi, aisee ni hatari tupu kwani siku hiyo ilisemekana bahari imechafuka, Boti ikawa inapanda juu inashika chini as if ndo inazama, nakumbuka watu wengi walitapika sana mpaka aliye nitia moyo mimi kwenda Znzr alitapika sana, nikamuuliza vipi tena mbona unatapik hivo?? Akasema mawimbi ya bahari ni makubwa kuliko ya kwao ziwani huko Mwanza.! Dah nashkur pamoja na hayo mimi sikutapika kabisa.

Usafir wa meli siji rudia tena, ukiangalia pemben unaona maji ya bluee na mawimbi. Nakumbuka meli ilikua na mwendo kasi kiasi ambao hauongezeki waka haupungui, baada ya kuona meli inayumba sana nilimfuata mmoja wapo wa watumishi mle ndan nikamwambia, " mwambie dereva apunguze spidi haoni tunavyoyumba !?" Jamaa aliniangalia, akacheka akasema spidi ikipungua ndo hatar zaid hata hivyo mbona mawimbi madogo sana haya.?? Duu nikarud kwenye sit yangu nasubir kitakacho tokea muda wowote.!!

Mungu mwema tulifika salama salimini, ila tu miguu iliishiwa nguvu kwa hofu ya kifo.!!
Aiseee wewe jamaa.

Halafu mbona kila mtu siku hizi akiongelea population ya Zanzibar anasema asilimia 95% ni waislam. Hivi kwanini mnazipunguza hizi asilimia??
 
Aiseee wewe jamaa.

Halafu mbona kila mtu siku hizi akiongelea population ya Zanzibar anasema asilimia 95% ni waislam. Hivi kwanini mnazipunguza hizi asilimia??
Ndo uhalisia mjomba, hata wao wakija huku watatoa takwimu ambazo kinyume na hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom