Aisee umenikumbusha safr yangu ya mwaka 2013 kutoka Dar kwenda Zanzibar (Unguja).
Mwanzo niliogopa sana mpaka kutaka kuhairisha safr lkn nilijaribu kuwashawishi wanibadirishie kituo cha mazoez yaan field mwalimu akagoma kabisa, ikumbukwe wakati huo meli ya spices imetoka kuzama kama wiki moja imepita, aisee siji sahau safr ile.
Kwani rafiki yangu tuliye pangiwa sehemu moja alinitia moyo kwamba yeye kusafr kwenye maji anajisikia ni salama zaidi kuliko kwenye nchi kavu yaan kusafr kwa gari.
Eeh bwana, tukafika Dar tukitokea Moro tukakata tiket kwenye Boti ya Kilimanjaro by that time ilikua ni meli bora zaidi maana inasemekana imetengenezwa kisasa zaidi. Ni kweli mle ndani ilikua kama mpo loyal sana.
Safari ikaanza eeh bwana eeh nilijitahidi kuzuia macho yasitazame nje maana niliona kama vile ndo naenda kufa nikasali sala yangu ya kuomba toba ili kama siku ndo imefika basi nipokewe na malaika huko mbinguni.
Njiani tuliona boti ndogo zikiendelea kutafuta miili ya watu kufuatia ajali ya spices.
Mungu mwema tulifika salama salimini Unguja, tukaweka kambi Madizini siku nyingin tukawa tunaend Bweleo huko aisee ni waislamu asilimia 95 lkn ukweli niliwapenda maana walikua wakarimu kwetu kwa kiasi kikubwa.
Mziki ukawa siku ya kurudi, aisee ni hatari tupu kwani siku hiyo ilisemekana bahari imechafuka, Boti ikawa inapanda juu inashika chini as if ndo inazama, nakumbuka watu wengi walitapika sana mpaka aliye nitia moyo mimi kwenda Znzr alitapika sana, nikamuuliza vipi tena mbona unatapik hivo?? Akasema mawimbi ya bahari ni makubwa kuliko ya kwao ziwani huko Mwanza.! Dah nashkur pamoja na hayo mimi sikutapika kabisa.
Usafir wa meli siji rudia tena, ukiangalia pemben unaona maji ya bluee na mawimbi. Nakumbuka meli ilikua na mwendo kasi kiasi ambao hauongezeki waka haupungui, baada ya kuona meli inayumba sana nilimfuata mmoja wapo wa watumishi mle ndan nikamwambia, " mwambie dereva apunguze spidi haoni tunavyoyumba !?" Jamaa aliniangalia, akacheka akasema spidi ikipungua ndo hatar zaid hata hivyo mbona mawimbi madogo sana haya.?? Duu nikarud kwenye sit yangu nasubir kitakacho tokea muda wowote.!!
Mungu mwema tulifika salama salimini, ila tu miguu iliishiwa nguvu kwa hofu ya kifo.!!