Sitakaa nimsahau mwanamke yule fedhuli….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
DSCN3827.JPG

Picha haihusiani na habari hii........

Nilikuja Dar mwaka 1990 kwa mara ya kwanza. Nililetwa na mjomba wangu kwa ajili ya kuzungumza na mzee mmoja ambaye alikuwa anahitaji kijana wa kumsaidia shughuli yake fulani ambayo mimi niliwahi kuifanya siku za nyuma.

Nilipofika Dar, kesho yake nilipelekwa ofisini kwa huyo mzee maeneo ya Posta na mjomba wangu ambaye ndiye aliyekuwa akifahamiana naye. Kwa bahati mbaya nilipofikishwa hapo ofisini kwa huyo mzee alikuwa ametoka hivyo mjomba wangu aliomba niwekwe hapo mapokezi ili nimsubiri na yeye akaondoka zake kwenda kwenye shughuli zake ferry. Nilikabidhiwa kwa sekretari wa yule bosi ili nimsubiri.Ile kukabidhiwa tu, alivyoniangalia, nilijua ana kisirani.

Unajua kuna jicho lingine mtu anakupiga hadi unaogopa hata kabla hajakusemesha. Basi, jicho la yule dada aliyekuwa amejichubua na uso wake kufanana kama pupa wa kipepeo liliniambia kwamba, sikuwa nahitajika hapo ofisini. Lakini kwa bahati yake mbaya, nilikuwa ni mgeni wa bosi wake, angefanya nini?
Unajua, kuna watu ambao wenyewe, wanapima heshima, hadhi na thamani ya mtu kwa namna mtu huyo alivyovaa au anavyozungumza na sifa nyingine za nje. huyu dada alinipima kwa namna nilivyokuwa nimevaa bila shaka na hata muonekano wangu kwa ujumla.

Wakati nasubiri hapo kwa mashaka makubwa, nilihisi mzigo wa tumbo, yaani kutaka kwenda kujisaidia. Nilivumilia kwa sababu, nilijua vyoo vya jengo kama lile nisingeweza kuvihimili. Nilijua ningeweza kuvumilia hadi nitakapotoka hapo, ili nikamalize shida kule Mwananyamala nilikofikia kwa mjomba wangu. Lakini tumbo halikuwa pamoja nami. nilizidi kuhisi kuwa natakiwa kuelekea chooni haraka iwezekanavyo. Unajua ugali wa mtama na maharage yaliyoungwa kwa mawese unapotaka kufanya fujo zake, unafanya hasa. Ilibidi nimuuulize yule dada mahali choo kilipo. ‘Mlangio ule pale.' Alisema bila kunitazama.

Nilisimama na kwenda huko chooni.
Nilipoingia humo ndani nilibabaika sana nikijiuliza choo ni kipi. Hatimaye kwa akili ya kuzaliwa nikajua ni kile kinu kilichokuwa mle ndani. Lakini nakaa vipi kwenye kinu hicho, ikawa shughuli pevu. Niliamua kudandia kwenye kinu hicho na viatu vyangu na kuanza kujisaidia.Nilipomaliza nilishuka na kuchukua karatasi ya choo (toilet paper). Hizi ninazijua, kwa sababu, hata kule kijijini kwetu Kideleko zinauzwa.

Nilikuwa sijawahi kuzitumia hivyo nilichukua furushi kubwa sana la hizo karatasi na kujisafisha halafu nikazitumbukiza hapo kwenye kinu.
Nilitoka na kurejea pale mapokezi. Yule sekretari kisirani, aliniangalia wakati nakuja na bila shaka alijua wazi matumizi ya choo kwangu yangekuwa ni mtihani wa Cambridge. Aliinuka na tulipishana, mimi nakaa na yeye anaelekea kule chooni nilikotoka.

Sikujua kwamba anaenda kufanya ukaguzi, kwa hiyo sikujali.
Lakini dakika moja tu baadae nilisikia sauti. 'Wewe kaka uliyetoka chooni sasa hivi, ndiyo ustaarabu gani ule. Hebu nenda kafanya usafi kule, uondoe uchafu wako. Halafu uliona wapi mtu anapanda juu ya choo badala ya kukaa.' Aliongea kwa kelele sana na wale wote waliokuwa pale mapokezi walikata shingo kumkagua huyo mshamba mchafu.

Niliduwaa kidogo, na yule dada alinishinikiza. ‘Nenda kafanye usafi basi au hunielewi…! Wee choo kimekuwa kichafu utadhani Tembo walikuwa wanaoga…..!' Alizidi kusema yule dada na watu waliokuwa pale mapokezi walinicheka sana. Watu wasio na huruma kwa hisia za wengine. Nilisimama na kwenda kule chooni, ingawa sikuwa najua huo usafi unafanywa vipi. 'Nenda kaflash, halafu safisha mle ulimokanyaga.' Aliniambia wakati naenda nikiwa nimeelemewa kwa aibu.

Sikuwa najua maana ya kuflash. Niliingia mle chooni. Wakati najiuliza maana na namna ya kuflash, nilisikia mlango ukifunguliwa. Kijana mmoja alikuwa amesimama nyuma yangu.
‘Wewe si mgeni wa mzee?' Aliniuliza. Nilisema, ‘ndiyo.'Yule kijana alinimbia kwamba, atanisaidia kufanya usafi kwa sababu yeye ni mhudumu wa ofisi ile. 'Huyu dada ana roho mbaya sana. Mtu akija kumwona bosi anachukia sana.'

Nilirudi mapokezi na aibu tele, kwani watu wote walikuwa wakinitazama mimi. Kwa bahati nzuri yule mzee alikuja. Pamoja na kufedheheshwa kule, alisema, niruhusiwe mimi kwanza kuingia…….
 
Maofisini hii hali ipo sana,watu wanadharau sana kama hujavaa kama walivyo tegemea utikelezeee

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Haa haa, Mtambuzi bwana, sasa kama haikuhusu si ungetoa angalizo pale pale mwanzo...

Anyways, kila mtu ana siku ya kwanza yake, tatizo tu ni huyo anayekutana naye kwenye hiyo siku, bahati mbaya kwake ni akiwa kama huyo dada.
 
unajihami mzee mzima ushamba mzigo mwenzangu,mimi nilipokuja dar 20yrs ago nilielekezwa tu nanilifika nilipoelekezwa bila kumuuliza yeyote na ni mara yangu ya kwanza ,toka pale nina ujasiri sana na huu mji ,ila niwakwenda nao taratibu sana unaumbua kwelikweli
 
unajihami mzee mzima ushamba mzigo mwenzangu,mimi nilipokuja dar 20yrs ago nilielekezwa tu nanilifika nilipoelekezwa bila kumuuliza yeyote na ni mara yangu ya kwanza ,toka pale nina ujasiri sana na huu mji ,ila niwakwenda nao taratibu sana unaumbua kwelikweli

Acha kujisifu nivea, hakuna mtu anayejua kila kitu, ipo siku tu utapatikana.....LOL
 
Last edited by a moderator:
Acha kujisifu nivea, hakuna mtu anayejua kila kitu, ipo siku tu utapatikana.....LOL
hee mtambuzi raha jipe mwenyewe kama sikusema ungejulia wapi babu wewe lol nitasubiri nani anisifie ,mbona nuilikwenda morogoro nikapotea kwiwkwiwkwiwkwiwkiwwi wacha mtambuzi mji ule umefanana sana hakuna hata gorofa kipindikile niweke alama
 
Hahahaaaaa! Babu Mtambuzi weekend nimebananishwa pahala, hata sihemi!!!!!! We acha tu, 40 yangu ya mwizi imefika. Jua tu kuwa sijawekwa ndani kwenye maandamano.
 
Hahahahaha mkuu Mtambuzi, kweli kabisa wakuja tunapata taabu sana hapa mjini siku ya kwanza.

Dawa ya visirani kama huyo dada ni wewe kujifanya Chonya of Chilonwa me!! nadhani unaikumbuka ile i take this girl to hospital.
Hata wale wazoefu wa mjini, kwa masekretari huwa wanakwama. Unajua masekretari wengi wanavisirani, sijui ndivyo wamefundishwa huko vyuoni kwao?

Mimi nachokifanya nikifika ofisini kama nataka kumuona boss, cha kwanza ninamfanyia tathmini sekretari, nikihisi kwamba kisirani naingia kwa lugha ya Chonya of chilonwa, na gazeti langu la daily news la zamani lakini natembea nalo kila siku, hapo kwisha habari yake.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaa! Babu Mtambuzi weekend nimebananishwa pahala, hata sihemi!!!!!! We acha tu, 40 yangu ya mwizi imefika. Jua tu kuwa sijawekwa ndani kwenye maandamano.

somebody poppin dat cherry!???:hail:

Mtambuzi kaka yangu pole sana...la kwako kubwa mno aisee afu aibu yake imekutokea wengi wakiona.

Mi nakumbuka nikija jijini mara ya kwanza nikashukia Kinondoni manyanya kwa dada yangu. Siku moja nikaenda Mwenge kuosha macho. Sasa mi nilishazoea nikitoka ubungo au Mbagala nakuja huko nashuka manyanya, navuka barabara nashuka na hiyo njia naenda home.
Hiyo siku jioni kama saa mbili, natokea mwenge, nikashuka nikavula barabara bwana kumbe naelekea mwananyamala...mara nakutana na kibao sijui nini complex...vi-bar dah nlitembea jamani kila saa narudi barabarani naanza upya.
Mimi alama yangu ilikuwa mnara wa simu uko pale maeneo ya kanisa la DPC, sasa huu upande wa pili siuoni.
Kilichonisaidi ile siku nikakuta madereva taxi nikamwambia nipeleke kwenye mnara uliopo karibu na kanisa...dahh
eti namwona anarudi barabarani afu anavuka..nlijiona mjinga sana ile siku...ila tangu ile siku sijawahi potea tena dar hii!!!
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi, huyu Receptionist hapa kwetu ni zaidi ya huyu nadhani, hivi wanakuaga na matatizo gani hawa dada zetu??? yaani customer care kwao ni zero
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom