Kama angemuliza huyo dada jinsi ya kutumia iko choo, yote yasinge mkuta.
Ila wanaume vijana hawapendi waonekane wajinga ndio maana wanakutana na hayo yote.
Tena bora alitokea kijijini, huyo dada alimuona mshamba na yupo innocent.
Kama angekuwa mtoto wa town-mtaani wanao jifanya wajuaji, asinge mkubalia hata aingie uko chooni, tena hata hapo mapokezi angemtoa. My experience, ufedhuli unakutana nao, inategemea wewe mwenyewe upoje.
Mie mwanamke nimepita maoffice mengi miaka zaidi ya 10 sasa, sikuwai kukutana na hayo, hapo dar.
Ila kuna siku mwaka 2010 nilienda office moja hivi na Taxi driver, yote yakaenda sawa.
Tunakaribia kukamilisha alitokea kijana mwingine ambae nilimfaham kidogo, huyu jamaa akajingiza kujifanya mjuaji.
Hapo akaribu kila kitu. Akasababisha hadi mimi huwo ufedhuli nikutane nao na madoc kuzikosa.
Huyu jamaa aliniuzi kweli, ila pale sikumwambia lolote. Nikamua nimjibu kifedhuli yule dada tukapandishiana. Na nikamuambia na uduma yake sitaki. Naenda office ingine.
Siku iliofuata nikaenda tena pale pale sababu zile doc nilikuwa nazitaji sana na wao tu ndio wanao toa hizo doc. Basi nilipofika wale madada walinikumbuka na yule tuliefyatuliana maneno aliona aibu hadi nikamuonelea huruma dada wa watu. Wakanitekelezea chapchap, dani ya nusu saa doc zote nikazipata.
Nikagundua yule jamaa yangu yeye mwenyewe ndio kapinda, kujifanya mjuaji.:blabla: