Sisi wanawake ni watu wa ajabu sana

😂😂 nimecheka hapo mtu anakimbia hata nyuma hageuki!!! Kwani ameona mganga..? Mtu akiona hata jini atageuka tu ahakikishe!! Sasa aone sura mbaya mpk asifanye second selection ya kugeuka kwamba kaona vibaya dah! Ebhana hatari poleni dada zetu
 
Ukiona unatumia vipodozi vingi usoni mwako na bado hauwi utakavyo, hadi ukalazimisha kwa kutumia image editing. Dada yangu jua wale wenye watoto wanaoingia sekondari na waliyopo huko. Ndiyo wa rika lako, waliwahi kujitambua kabla yako.

Shtuka, hizo habari waachie wanao tena, maana itakuwa si wadogo zako hao hadi kufikia rika hilo. Wamezaliwa na wenye umri sawa na wewe
 
Ukisoma 1Wakorintho 11: 3-9 utagundua kuwa wanawake wako sahihi kufanya wanayofanya. Kwa maana wao wameumbwa kwa ajili ya wanaume na si vinginevyo. Kichwa cha mwanaume ndiyo akiruhusiwi kuchezewa maana ni kichwa cha Mungu. Ila kichwa cha mwanamke ukiwemo uso au sura yake ruksa kuchezewa chezewa maana vichwa vyao sio vya Kristo, ni vichwa vya binadamu yaani mwanaume.

Hivyo hakuna shida kabisa, hata wakijiedit wakawa kama paka ila biblia inasistiza wakumbuke kufunika/kusitiri vichwa na maungo yao wakati wa kusali/kuongea na Mungu.

Niliwahi kusalia kanisa Katoliki Abuja Nigeria, aisee wanawake wote wanafunga vitambaa/kufunika vichwa vyao wawapo kanisani. Hiyo ndivyo inavyotakiwa kuwa. Siyo huku kwetu binti unaenda kanisani umesuka style ya sina mchumba alafu ufungi hata kitambaa, ujue kuna watu unawaharibia ibada zao.

1Wakorintho11:3-9

3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. 4 Kwa hiyo mwanamume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anaaib isha kichwa chake. 5 Na mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anaaibisha kichwa chake, ni sawa kama ame nyoa nywele zote kichwani. 6 Kama mwanamke hataki kufunika kichwa chake, nywele zake zinyolewe; na kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa kichwa chake, au kukata nywele zake, basi afunike kichwa chake. 7 Mwanamume asifunike kichwa chake kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8 Kwa maana mwanamume hakuumbwa kutoka kwa mwanamke, bali mwanamke ame toka kwa mwanamume. 9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwa namke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.
 
Kama kawaida mwenye picha yake Divathebawse atapita hapa kimya kimya
Halafu lipo humu jamiiforum kazi yake kuiba story za watu kwenda kuweka kwenye kpindi chake eti kuna mdau kanitumia mesej anaomba ushauri linaniuzigi sana

yess BiShoo haswaaAaa
 
Back
Top Bottom