Wingi wa watu ambao ni wazungumzaji sana ni waongo

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
3,626
12,057
Kwa utafiti wangu binafsi ambao nimeufanya nimethibitisha kwamba wingi wa watu waongeaji sana ni waongo waongo.

Ni wataalamu wa kuchanganya uongo na ukweli ili uamini anachokisema, yaani waswahili husema kuongezea chumvi.

Ni aina ya watu ambao huwa wana wivu, kama ni rafiki yako mmetoka level moja basi huumia kuona unasonga mbele.

Wanajua sana kujipendekeza kwa watu waliowazidi uchumi na kipindi hiki huweza kuzungumza uongo na kuwachafua wenzie ili kusudi yeye apate nafasi either ni kazi/ connection au vyovyote.

Hujizungumzia kwamba wana uwezo mkubwa hali ya kuwa hakuna wanachokifahamu.

Kwenye mahusiano huwa waongo sana.

Aina ya watu wa aina hii uwezo wao wa IQ huwa ni mdogo, hivyo hutumia mdomo kama kipaji kufanikisha mambo yake kwa maana huwa hawajiamini.

Ni walamba viatu wazuri.

Wanasiasa wengi wanaingia kwenye kundi hili.

Watu wakimya ni tofauti mara nyingi uwezo wa kiakili ni mkubwa, hawapendi kupelekeshwa kipuuzi.

Watu wakimya wenye uwezo wa kufanya mambo makubwa huwa wanatumikishwa na hawa wapiga domo.
Unakuta engineer anatumikishwa na kupelekeshwa na mpiga mdomo kisa tu mpiga domo anajua kujipendejeza kwa boss na ni mlamba viatu mzuri.

Ni weupe vichwani ila hujikuta wajuaji sana.

Chunga sana kuwa na urafiki na watu wa aina hii, kama unae unaweza elewa nasema nini, lakini pia kama huna kuwa nao makini sana.

Ukikutana na mtu ana maneno mengi anza kumchunguza kwa makini,.

Nimesha delete washkaji wa namna hii wote. Mi sio mzungumzaji.
 
Hawawazidi hawa kwa Uongo.

20240319_163514.jpg

PambanaZaidi/CottonandMore
 
Uko sahihi, Mtu mwongeaji huwa simpatii nafasi anizoee, kama ni Mwanamke, basi vile anakitobo, natoboa tobo napita hivi.
 
Back
Top Bottom