Sisi Tanzania ni watu wa ajabu sana! Hakuna tunachoweza zaidi ya UCHAWA!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Yaani watu mnakwenda tu kwenye maonyesho na mnarudi mmesainishwa mikataba ya kimangungo ya " kuuza" bandari zenu kwa waarabu!

Baada ya TICTS kumaliza muda wao iko wapi taarifa ya kina ya utendaji wao ili tuone manufaa, changamoto na skills transfer ambayo Watanzania wamepata ili kuweza kujiendesha wenyewe!?

Tumejenga miundombinu kama SGR , tumekopa fedha nyingi kutengeneza magati bandarini na maeneo mengi ya kimkakati halafu bila ushindani wowote mnamkabidhi Mwarabu Bandari zetu kirahisi hivyo!?

Kuna kauli kwamba kazi ya kutafuta fedha itakuwa ya DP World! Kwahiyo hawana fedha baada ya kupata concessions ndipo watazitumia kutafuta fedha!!
Nchi ya watu wa ajabu sana hii!
 
Back
Top Bottom