Sisi tuliochagua wapinzani tumekatiwa umeme na maji. Vipi upande wenu huko majimbo yanayopendwa na serikali?

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Hahahahahaa!! Inabidi nianze uzi kwa kicheko.

Tumepitia kipindi kigumu kama nchi. Licha ya kuwashauri kwa muda mrefu kwa kurudia rudia tukidhani wanatuelewa wakashupaza shingo.

Leo Rais Samia, Makamu wa Rais na makundi yake yote hawawezi kukwepa mdororo huu wa maji na umeme. Tumerudi mwaka 1990s tena kwa uzembe na kutokujali kwa viongozi na wenye mamlaka CCM.

Tulidai viongozi wanaowajibika na kuwa wawazi tukaambiwa sisi wapinzani tunawachelewesha. Sasa kiko wapi?

Leo uovu na uhalifu uliofanywa na serikali ya awamu ya tano wanataka kujivua na kumbebesha Januari Makamba ambaye yuko ofisni kwa Mwezi mmoja tu.

Hata kama Makamba anataka kuihujum serikali hawezi kuwa mjinga kiasi hicho akazima umeme na kukata maji wakati mmoja kwa spidi hii.

Hayati JPM alitamba nchi nzima akashawishi wananchi kwa ngumi na mateke kwamba wakichagua wapinzani hawatapa huduma za kijamii. Wapinzania wakaonekana kama mashetani kwenyr ardhi yao ya Tanzania.

Pale wananchi walipokaza kuchagua wapinzani bado wapinzani hao waliondolewa kwa nguvh ya mitutu na vyombo vya dola.

Mwisho wa siku tukasema haya isiwe nongwa. Majimbo yote, kata zote na vijiji vyote viko mikononi mwa CCM.

Vipi huko umeme na maji mnapata 100 kwa 100?
 
Si mlisema mama anaupiga mwingi anawakomesha mataga na sukuma gang?
 
Hahahahahaa!! Inabidi nianze uzi kwa kicheko.

Tumepitia kipindi kigumu kama nchi. Licha ya kuwashauri kwa muda mrefu kwa kurudia rudia tukidhani wanatuelewa wakashupaza shingo.

Leo Rais Samia , Makamu wa Rais na makundi yake yote hawawezi kukwepa mdororo huu wa
Hadi pale kenge watakapo kuwa wasikivu hapo ndio Hali itakapo badilika
 
Ni kweli amewanyosha kweli kweli. Maana kwangu mimi umeme ni full time shuguli zangu zinaniendea freshi tu.
Kwa hiyo huu umeme unakatika kwa mataga na sukuma gang tu?

Hongereni mabavicha mko vizuri
 
Tutaendelea kuongozwa na CCM kwa sababu nchi hii hakuna chama mbadala. Bora CCM mara mia.
 
Sisi tuliochagua ccm tunatembelea mavi eight, na maji kwetu yanatoka saa14 tunamwagilia ukoka kila baada ya nusu saa na kuoshea nyumba na mbwa wetu!

Mliowachagua wapinzani isomeni namba tu,mlishindwa kuchagua maendeleo
 
Hebu ongeza volume kidogo
images (5).jpeg
 
Back
Top Bottom