Sisi kama Jamii tujadili namna ya kuwasaidia vijana wanaofeli shule na kuachwa mitaani

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Umuofia kwenu,

Nguvu ya Taifa lolote ni vijana. Nchi inaweza kuwa na advancement kubwa kwenye teknolojia na sekta zingine lakini kukiwa na ombwe la vijana kwenye jamii ama nchi hiyo ni kujiweka rehani. Vijana wa jamii yeyote huandaliwa kushika hatamu pale wazee ama wazazi wao wanapoishia.

Nimeanza na dibaji hiyo kwa kuangazia kwa umuhimu dhima ya vijana ndilo Taifa la kesho, mimi ninadhani Vijana na Taifa iwe ndiyo slogan yetu kwa sababu neno Kesho kutumika ni kuwabagua ama.kuwaengua vijana kwenye michakato muhimu inayohusu Taifa letu kujikwamua kutoka nyanja mbalimbali.

msomaji wangu, hebu jaribu kuvuta hisia na kumbukumbu ya safari yako ya maisha. Tuangalie kwenye stream ya elimu. Tangu umeanza shule mlikuwa wangapi, na endapo ilifanikiwa kusonga mbele, ni wanafunzi wangapi mlipata alama za kusonga mbele kielimu? Ni wangapi waliachwa kwa kukosa vigezo vya kuchaguliwa elimu ya mbele?

Ukiangalia kwa jicho tunduizi utagundua kuwa vijana wengi wanaachwa mitaani bila tentative plans kuwasaidia juzi mbalimbali ili kuwaandaa kuwa wanafamilia ama viongozi wa baadaye.

VIjana wanapopishana na maarifa yanayoweza kuwasaidia kuyakabili na kuyabadili mazingira ni dalili na maandalizi mabaya kwa Taifa zima. Nasema Taifa kwa sababu tunapokuwa na wataalam wachache na kundi kubwa la illetrate ni ngumu sana kufikia malengo chanya ya kisekta.

Tunaona polisi wakikabiliana na mamundi ya kihalifu ambapo wengi ni vijana. Tunapaswa kuweka mikakati ya kuondoa uhalifu kwenye jamii hususan vijana ili kuwaepusha kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa

USHAURI
  1. Sera ya elimu iboreshe hitaji la kila Mtanzania kuanzia umri wa miaka 18 awe anakiwango cha elimu ya cheti au juu ya hapo. Cheti ninachozungumzia hapa ni cha ujuzi na siyo certificate of attendance.
  2. Shirika la Viwango TBS wabuni mkakati wa kutoa elimu ya viwango kwa uzalishaji unaofanyika ngazi za awali kabisa. Hivi sasa TBS imegeuka mradi wa maafisa wachache ambao wamejifungia maofisini wakiwasubiri wazalishaji kwenda kujisajili huku ikiweka urasimu mkubwa kwa wateja. Sana sana outreach ya TBS yaani kazi za nje ya ofisi ni kwenda kukagua, kukamata na kuharibu bidhaa zilizochini ya viwango. Vijana wakianza kuelimishwa mashuleni kuhusu umuhimu wa ubora wa bidhaa itassidia kuondokana na uzalishaji wa kienyeji ambao umeshamiri nchini
  3. Serikali ngazi ya wilaya kuanzisha makambi ya vijana ili kuwakutanisha na wataalam, wajuzi na wakufunzi mbalimbali wajifunze ujasiriamali wa uzalishaji, ufundi na huduma mbalimbali. Wahitimu wa makambi hayo wapewe vyeti ama.leseni za ujuzi husika.
  4. Jeshi la Magereza lianzishe program ya uzalishaji kwa kuwahusisha vijana ambao watajitolea. Programu hizo zijikite kwenye kutoa ujuzi kwa vijana ili kuongeza soko la ajira kwa wahitimu
  5. Vijana waliopo ngazi ya familia na hawana ajira, elimu wala ujuzi wowote waanze kuandaliwa program za kuwafikia na kuwapatia ujuzi na nyenzo za kujikimu.
  6. Mikopo ya vijana, wanawake na wenye ulemavu iboreshwe ili kusaidia wimbi kubwa la vijana ambao kwa namna mbalimbali wamekosa nafasi za kuendelea kimasomo.
NInawaalika wanajamii tujadili namna ya kuwasaidia vijana wetu wengi ambapo wengi huongia kwenye shinikizo rika hatimaye kuzalisha makundi ya kihalifu na fananizi nayo.

CC: Pascal Mayalla Retired LIKUD FaizaFoxy Maxence Melo Depal Deborah9007 raraa reree Extrovert Erythrocyte G70 mangi jr mrangi ChoiceVariable MP0NJ0LI
 
Naunga mkon hoja
Kuna watu watasema zipo Veta kama huyo mkutupukaji hapo juu.

Lakini kwa umakini sana utakuta hizo VETA hazijaweza kutatua tatizo la dropout.

Kuna familia hawana uwezo wa kulipia gharama za elimu hivyo serikali kama Mzazi mkuu inapaswa kuangalia kwenye mipango yake namna ya kuwafikia hao.

Jamii ikiwa bize kwenye shughili za uzalishaji na ugavi itaondokana na majanga mengi yakiwemo ya kihalifu
 
Sasa wewe Imetoa maoni Yako na Mimi nimetoa maoni yangu.

Kuna vyuo kibao vya Veta ukimaliza unapewa na vifaa kazi eg Dakawa

Hakuna njia ya shortcut sehemu pekee wanayoweza pata ujuzi ni Veta.

On top of that Kuna mikopo ya Halmashauri,Kuna jkt,Kuna BBT,na Kuna wazazi.

Sio swala la kuachia Serikali ni swala la Kila mmja.

Mwisho Vijana wa saizi wanataka maisha Short kiasi kwamba ni shida sana kwenye kazi manual.
Mindset uliyonayo ni kwamba kila.jambo ni AUTOMATIC driven.

Badili mtazamo. Angalia efficiency ya hayo uliyoyataja.

Halafu kuwalaumu vijana ni mapungufu ya kifikra. Mmezoa kuwapiga watu gubu ili wabadilike na huo ni ulevi wa madaraka
 
Mfumo wa elimu hauwasaidii kabisa. Mi natamani elimu ya ufundi ingekuwa o'level.

Masomo ya ufundi yapo kwenye shule za vipaji ambavyo mi naona wale hawaihitaji kiivyo ukilinganisha na hawa wa shule za kawaida (kata) wanaomaliza secondary na division 4 au 0, mtoto uwezo wake ni wa kawaida au wa chini cha ajabu hata jina lake hajui kuandika ila anashindiliwa tu physics chemistry sa atatoboaje huyu? Miaka minne anakaa bure tu. Angefundishwa hata welding si angemaliza na kitu.
 
Ni swala linalotakiwa kuanzia kwenye mitaala ya shule, elimu ya kuanzia shule za awali ilenge kuwapa vijana ujuzi na maarifa na pia vyuo vya kati vikiwemo VETA vinavyotoa certificate, diploma vianzishwe kila kona ya nchi ili kuwa absorb vijana wote watakaokuwa wamemaliza masomo ya sekondari na wale wachache wenye ufaulu wa juu ndo waendelee na masomo ya shahada.​
 
Mtoa mada nikupongeze kwa mawazo Yako lakini Niseme tu ukweli
1. Lazima hao vijana unaowaongelea wajua sometime kutoboa ni mchakato. Wapo wachache ndani ya muda mfupi wanatoboa
2. Uaminifu sifuri kwa vijana. Nilishawahi mwambia kijana mmoja wewe unalalamika huna mtaji wakati wafanyakazi wengi wa serikali wanamitaji/ anaweza kwenda bank na kukopata hata milioni 20 kwa ajili ya biashara na wanatamani kweli kweli lakini kwa madhila wengi waliyokutana nayo kutoka kwa wasimamizi wa hizo biashara hawana hamu.
3.Waeleze starehe wazifanye kwa kipimo. Huwezi pata 15 leo jioni umeshinda baa na washkaji mnafurahisha Malaya wa bar alafu utoboe kirahisi. Lakini tusichoke kuwasapoti
 
Kama serikali inawapuuza vijana wanaofeli sisi wengine tutawasaidia kwenye mkwamo waliokwama ili wafikie ndoto zao za kujiletea maendeleo. Serikali huwa inashangaza sana pale inapojivunia kundi dogo la waliofaulu mtihani wao huku wengi waliofeli ikiwaacha watokomee gizani kusikojulikana, haina mkakati wa kuwasaidia kuendelea na matamanio yao ya kuendelea kupata elimu kwa stadi wanazozisomea
 
Back
Top Bottom