Waislam tujenge vyuo vya kuwapa vijana ujuzi

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,590
4,277
Kumekuwa na wimbi kubwa la ujenzi wa misikiti ambapo ni jambo jema japo mingine inajengwa karibu karibu sana na mingine nje sana; Kimsingi sipingani na huu utaratibu ILA kwa umuhimu, nimeona tuna nguvu kazi ya Vijana wengi sana mitaani ambao hawana ujuzi (hawa ajiriki) hivyo, nashauri misaada tunayoomba huko nje, tuweke kipaumbele kuwapatia vijana wetu UJUZI na Elimu ya dini.

Hii inawezekana kwa kuomba tujengewe Vyuo vya kati ngazi ya VETA vya kufundisha Vijana juzi mbalimbali, na vyuo vingine vya kutoa Elimu ngazi ya Diploma kama za Afya, Kilimo, nk Vijana wenye ujuzi ngazi ya Diploma ndio wanahitajika kwa wingi sana duniani kwani hao ndio wazalishaji.

Taasisi kubwa kama BAKWATA na Zingine kama hiyo wanaweza kuomba kujengewa vyuo vya juu au hata Hospitali ya Kibingwa. Nafikiri kuomba mfadhili mkubwa ajenge msikiti ni sawa na kumuomba mfadhili atupatie Samaki badala ya kuomba atupatie chuo (Ndoana) ili tuendelee kuvua samaki wetu wenyewe

MUHIMU: Vijana wenye Ujuzi na Elimu ya Dini, wanaweza kuelewa ukuu wa Mungu na kuutukuza kuliko wengine.

VIJANA WAKIPATA UJUZI NA KUIMARIKA KIUCHUMI, WATAKUWA WACHAMUNGU ZAIDI NA PIA WATAJENGA MISIKITI WENYEWE!
 
Acha watu wale nyama za Uturuki. Vyuo vitawasaidia nini. Uislamu ni nyama na ubwabwa.
 
Back
Top Bottom