Hapa siitetei OUT wala Evelyn na wala huwa sicomment popote ila najaribu kutafakari mtu wa kusoma PhD kushindwa kujua njia sahihi ya kutatua tatizo lake na kukimbilia kwenye social media!! Mimi nipo hapo tuu!!
Sasa, arguments za mtu anayetaka kusoma PhD, ndiyo hizi?? Like serious??
Umeshindwa kuelewa phrase ndogo tu "Evelyn anakushinda...!" Utaweza kuandika hata hiyo concept note? Bro you are not serious hahahaahaaaaa!!! No wonder hata kazi yako haijasomwa hahahaaaaaa!!
Sikumaanisha ukashindane na Evelyn, nimemaanisha kutumia akili za kawaida kuwasiliana na Evelyn ukasolve unapokwama!! Namna hiyo ndiyo tunakutegemea ufanye tafiti zenye tija za kuisaidia jamii, nakuleta solution mujarabu kwa jamiii!! Hahahaaaaaaaaa!! Too narrow bro....!! Hivi hata jeshini hukupita ukapata mbinu mbadala za kukabiliana na binadamu na vikwazo vyao???
Tafuta PostGraduate Diploma yoyote kwanza uchangamshe ubongo kabla!! PhD naona OUT wapo right kabisa, hatuwezi kukutegemea uwe kwenye management na then mambo madogo tu unakimbilia kwenye social media! Yaan hukujua hata hatua za kuchukua, kweli?? Unataka PhD?? Aaaah!! Big no....!! WASOMI nyie ndiyo mnatuingiza kwenye mikataba isiyo na tija kwa taifa
mkuu
Uongozi wa chuo kikuu una wajibu mkubwa wa kuwajibika kwa wanafunzi wanaosoma kuanzia undergraduate & postgraduate
kwa sababu utafiti wa kiwango cha degree ya pili na ya tatu ni muhimu kwa manufaa ya chuo na nchi mwanafunzi anahitaji mazingira mazuri ya kitaaluma, msaada wa kutosha, na mifumo madhubuti ya usimamizi. Umuhimu wa uongozi wa chuo kuwajibika kwa wanafunzi wa masters and PhD ni pamoja na yafuatayo:
1. Kuboresha Ubora wa Utafiti
• Uongozi wa chuo una jukumu la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa masters and PhD wanapata rasilimali muhimu kama maktaba, maabara, na mifumo ya kisasa ya utafiti.
• Kusimamia ubora wa usimamizi wa tafiti ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata mwongozo bora kutoka kwa wasimamizi wake.
mfano wakati supervisor anapelekewa chapter one wajibu wa supervisor ni kushauri kutoa mapendekezo sasa kama supervisor hatoi ushirikiano hata wa kujibu email huyo ni supervisor hicho ni chuo?nini maana ya uongozi
mfano umepeleka title kama
The Influence of Green Human Resource Management (Green HRM) on Performance and Productivity in Higher Academic Institutions”
wajibu wa supervisor ni kukaa na mwanafunzi kushauriana pamoja na kutoa mapendekezo na sio ukimya wa kujibu email
2. Kulinda Haki za Wanafunzi
• Kuweka mifumo ya kushughulikia changamoto zinazowakumba wanafunzi wa PhD, kama ucheleweshaji wa usimamizi, migogoro na wasimamizi, au ucheleweshaji wa tathmini za tasnifu.
• Kuhakikisha wanafunzi wanahifadhiwa dhidi ya unyanyasaji wa kitaaluma, upendeleo, na changamoto zingine zinazoweza kuathiri maendeleo yao.pamoja na mazingira ya rushwa
3. Kuwezesha Mazingira Rafiki ya Kujifunza
• Kuanzisha sera zinazoimarisha mazingira mazuri ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa fursa za mafunzo ya ziada, ushauri wa kitaaluma, na msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi wa masters and PhD.
• Kutoa ufadhili wa tafiti au usaidizi wa kifedha kwa wanafunzi wanaohitaji, ili kuhakikisha kuwa masomo hayaendi kusuasua kutokana na changamoto za kifedha.
4. Kuhakikisha Usimamizi Bora wa PhD
• Kuweka na kusimamia taratibu madhubuti za kuhakikisha kuwa wasimamizi wa masters and PhD wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kutoa mrejesho kwa wakati.
• Kusimamia tathmini za mara kwa mara za maendeleo ya wanafunzi wa PhD ili kubaini changamoto na kuzitatua mapema.
5. Kukuza Sifa ya Chuo Kikuu
• PhD zenye ubora huongeza hadhi ya chuo kimataifa, kwani machapisho ya kisayansi yanayotokana na tafiti hizo yanasaidia kupandisha viwango vya chuo.
pamoja na kupunguza malalamiko na kujenga huduma bora yenye huduma safi na yenye kuigwa
hapa ndio tatizo lilipo
• Wanataaluma waliomaliza kwa mafanikio huchangia maendeleo ya jamii, jambo linaloleta heshima kwa chuo husika.
Kwa ujumla, uongozi wa chuo unapaswa kuhakikisha kuwa mfumo wa usimamizi wa wanafunzi wa masters and PhD unafanya kazi kwa ufanisi, ili kuwasaidia wanafunzi kumaliza masomo yao kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. Ikiwa uongozi hautawajibika, wanafunzi wanaweza kukumbana na ucheleweshaji, msongo wa mawazo, na changamoto nyingine zinazoweza kuathiri mafanikio yao kitaaluma.
kama haya mambo hayapo chuoni ama hayapo kwa kiwango hiki tarajia malalamiko mengi
nafikiri kama kuna utaratibu mzuri malalamiko hayawezi kuwepo hata yakiwepo yatatuliwa kwa ubora wa hali ya juu
Tusibeze watu wanaosoma duniani imeendelea kutokana na tafiti hizihizi kusoma PhD sio kwamba ndio usipewe huduma bora kabisa
taasisi inayodharau wateja huwa inaanguka sababu ni vitu viwili vinategemeana