cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 112,101
- 181,169
Walikufanyaje? Em elezea kwani, LolKila mtu ana experience yake, sitaki kusikia neno UDSM kwenye postgraduate.
Walikufanyaje? Em elezea kwani, LolKila mtu ana experience yake, sitaki kusikia neno UDSM kwenye postgraduate.
Katika makosa niliyofanya katika maisha ni kujiunga na masomo ya PhD pale Open University of Tanzania. Ningelijua ningeeda UDSM. Kwa matatizo ninayopitia sishauri mtu akasome PhD pale OUT.
Chamgamoto nilizopitia ni kama ifuatavyo:
1. Supervisor kutojibu email zangu au hata sms kwa zaidi ya mwaka mmoja.
2. Supervisor kukaa kimya bila kupitia proposal kwa zaidi ya mwaka mzima na Wala hajali. Unamtumia kazi zaidi ya mara kumi ila hajibu na yupo kimya kana kwamba hakujui.
3. Process ya kubadilisha supervisor ni ngumu Sana, unaweza kukaa mwaka mzima unahangaika tu. Nilijaza fomu ya kubadilisha supervisor wakaa kimya, nilipowakomalia wakanipa fomu nyingine, stori ikaishia hapo.
4. Yule mdada au secretary wa ofisi ya post graduate research wa OUT ana dharau Sana. Ukimpigia simu hapokei na hata akipokea akajua ni wewe ana kata simu yako. Yule dada ni shida Sana.
5. Kwa sisi tulioko mikoani ni shida kusoma PhD OUT. Hawajali kabisa. Na ukisema usafiri kwenda huko Dar utazungushwa mpaka uchoke. Nimeenda Dar kituoni kwao pale Biafra ni shida tu hakuna la maana la kunisaidia.
Kutokana na OUT kunisumbua kwa muda wa miaka mitatu huku ada yangu wamekula ila kunisaidia kwao wanaona mzigo au usumbufu kwakweli ni Bora niache kusoma hiyo PhD nifanye mambo mengine. Ila wamenipotezea muda, hiyo miaka mitatu imeenda Bure. Yani miaka mitatu unahangaika na proposal haijawahi kusahishwa hata kusomwa tu na supervisor. Ukienda ofisini kwao Biafra unaambiwa supervisor wako hayupo amesafiri.
7. Kwa kweli OUT mnakatisha tamaa, mtu anakuwa kama hasomi PhD. Kama uwezo wa kusimamia tafiti za wanafunzi wa PhD hapo si mnamwambia mwanafunzi atafute chuo kingine kuliko kupoteza muda wa mtu.
Msimamizi (supervisor) anapokuwa anasimamia mwanafunzi wa postgraduate ana majukumu muhimu sana katika kuhakikisha mwanafunzi anafanikiwa katika utafiti wake na kuhitimu kwa wakati.
yafuatayo ni majukumu
1. Kutoa Mwongozo wa Utafiti – Kumsaidia mwanafunzi kuchagua mada inayofaa, kuboresha maswali ya utafiti, na kuelekeza mbinu sahihi za utafiti.
2. Kusimamia Maendeleo – Kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi kupitia mikutano ya mara kwa mara na kutoa mrejesho wa kujenga.
3. Kuhakikisha Ubora wa Kazi – Kuhakikisha kuwa utafiti unakidhi viwango vya kitaaluma na kitaaluma, ikiwemo tafiti za awali na mbinu za uchambuzi wa data.
4. Kumsaidia Katika Uandishi wa Tasinifu (Thesis/Dissertation) – Kutoa mwongozo katika uandishi wa sura mbalimbali za tasinifu na kusahihisha makosa kabla ya kuwasilisha.
5. Kutoa Ushauri wa Kitaaluma – Kumwelekeza mwanafunzi kuhusu fursa za utafiti, machapisho ya kisayansi, na mitandao ya kitaaluma.
6. Kusaidia Katika Maandalizi ya Viva Voce – Kumpa mwongozo kuhusu jinsi ya kujibu maswali ya mtihani wa mdomo (defense) na kusimamia maandalizi yake.
7. Kuhimiza Nidhamu na Ufanisi – Kuhamasisha mwanafunzi kufuata ratiba ya kazi, kudhibiti muda, na kukamilisha utafiti kwa wakati.
8. Kuwa Kiungo na Chuo au Taasisi – Kuwasiliana na idara ya chuo kuhusu masuala ya kitaaluma, taratibu za chuo, na fursa za ufadhili au usaidizi mwingine.
9. Kumjengea Uwezo wa Kujitegemea – Kumfundisha mwanafunzi kuwa mtafiti huru, kufanya maamuzi ya kitaaluma, na kujenga msingi wa taaluma yake ya baadaye.
NOTE:Hapa hakuna sehemu yoyote inayoelekeza kuwa mwanafunzi atoe rushwa
hebu tuone wajibu wa supervisor akitumiwa kazi ya research proposal
Msimamizi (supervisor) wa mwanafunzi wa PhD anapopokea kazi ya dissertation (tasnifu), ana wajibu wa kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakidhi viwango vya kitaaluma na kitaaluma kabla ya kuwasilishwa rasmi. Wajibu wake ni pamoja na:
1. Kusoma na Kutoa Maoni ya Kina
• Kupitia kila sura kwa umakini ili kuhakikisha mtiririko mzuri wa mawazo na hoja.
• Kutoa mrejesho kuhusu nguvu na udhaifu wa kila sehemu ya tasnifu.
2. Kuhakikisha Ubora wa Utafiti
• Thibitisha kuwa utafiti unafuata misingi sahihi ya kitaaluma.
• Hakikisha kuwa maswali ya utafiti yamejibiwa kwa kina na kwa ushahidi wa kutosha.
3. Kusahihisha Makosa ya Kiufundi
• Kurekebisha makosa ya sarufi, uandishi wa kitaaluma, na upangaji wa sentensi.
• Kuhakikisha matumizi sahihi ya rejea na mtindo wa kunukuu (e.g., APA level one au saba ,MLA, Harvard).
4. Kutoa Mwongozo wa Kuboresha Mbinu za Utafiti
• Kushauri kuhusu uthibitisho wa data, tafsiri ya matokeo, na uchambuzi wa kina.
• Kuelekeza marekebisho katika sehemu ya mbinu (methodology) ikiwa kuna mapungufu.
5. Kuhakikisha Muundo wa Tasnifu Unafuatwa
• Kudhibitisha kuwa tasnifu imepangwa kulingana na mwongozo wa chuo.
• Kuangalia iwapo kuna utangulizi sahihi, sura za msingi, hitimisho, na mapendekezo.
6. Kuandaa Mwanafunzi kwa Viva Voce
na kumpa tarehe maalumu kuwa siku fulani utatakiwa kufanya vivavoce kwa kubandika matangazo kwenye mbao za chuo pamoja na kwenye websites kama mwanafunzi fulani atafanya viva voce hivyo umma unaalikwa
hii inafanywa na SAUT main campus na UDSM kwa ubora wa hali ya juu kabisa
• Kumpa mwongozo wa jinsi ya kutetea tasnifu yake mbele ya kamati ya mitihani.
• Kumuandaa kwa maswali yanayoweza kuulizwa na jinsi ya kuyajibu kwa weledi.
7. Kufanikisha Kuwasilishwa kwa Tasnifu
• Kuridhika kuwa kazi iko tayari na inaweza kuwasilishwa kwa ajili ya tathmini rasmi.
• Kusaini fomu za idhini na kuwasilisha kazi kwenye idara husika.
8.kujibu maulizo,kutoa ushauri pamoja kama una tatizo usaidiwe
kama haya supervisor hafanyi basi sio supervisor tena kama management haifatilii basi ni tatizo kubwa na linashusha ubora wa chuo
Halafu wanapenda rushwa sana. Ukiwapa chochote kitu supervisor anasoma chap. Yaani ni balaa. Mimi nilitaka kusoma PhD OUT nikashtika baada ya kuona jamaa yangu anvyosumbuliwa.
Kila siku nyuzi za kuichafua OUT zinaanzishwa, hii sasa nahizi ni vita kama zilivyo vita zingine.
OUT kwenye supervision wapo vizuri sana ukilinganisha na vyuo vingine, angalia graduates wake kitakwimu wengi wanamaliza ontime!!
Wewe bado huna ground ya kusoma PhD, ungeshajua hatua za kuchukua kuanzia unapopangiwa supervisor na kazi yako inapopokelewa!! Na OUT mtu kama wewe hutoboi, serious nakuambia utaishia kulalamika kwenye social media tu kama mtoto wa kidato cha pili!!
Kuna pande mbili zinakulinda kama mlaji, kwanza Mkurugenzi wa Post Graduate, ulimpa taarifa za usumbufu huo?? Au ulipotuma kazi yako nani alijua ili kuweza kumonitor mwenendo wa hiyo kazi yako??
Pili; Proposal yako imeenda faculty gani?? Kila facult ina departments ambazo zina coordinators wanaopaswa kujua wanafunzi wake wanakwenda vipi!! Umewasilisha malalamiko yako??
Umesema wa mikoani?? Umewasiliana na DRC au unahangaika na Supervisor peke yake??
Supervisor nao ni watu, wana tabia zao ushasema mkali haingiliki, wana matatizo na changamoto mbalimbali. Ujanja ni kutumia zaidi ofisi ya centre, sasa kama ulijua zile ni mapambo rudi nyuma, anza upya. Usipotoboa nipo paleeee....!!
Wewe unaonekana bado una utoto mwingi nenda kasomeWalijua hawezi kutoboa tena UDSM,,angalia hata gpa za open zilivyokuwa kubwa
Mkuu lakini Master's by Thesis na PhD supervisors ni wawili sasa weweKwa PhD mkuu ni shida. Maana supervisor anatokea Makao Makuu Biafra
Asante kwa maelezo.mazuriMsimamizi (supervisor) anapokuwa anasimamia mwanafunzi wa postgraduate ana majukumu muhimu sana katika kuhakikisha mwanafunzi anafanikiwa katika utafiti wake na kuhitimu kwa wakati.
yafuatayo ni majukumu
1. Kutoa Mwongozo wa Utafiti – Kumsaidia mwanafunzi kuchagua mada inayofaa, kuboresha maswali ya utafiti, na kuelekeza mbinu sahihi za utafiti.
2. Kusimamia Maendeleo – Kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi kupitia mikutano ya mara kwa mara na kutoa mrejesho wa kujenga.
3. Kuhakikisha Ubora wa Kazi – Kuhakikisha kuwa utafiti unakidhi viwango vya kitaaluma na kitaaluma, ikiwemo tafiti za awali na mbinu za uchambuzi wa data.
4. Kumsaidia Katika Uandishi wa Tasinifu (Thesis/Dissertation) – Kutoa mwongozo katika uandishi wa sura mbalimbali za tasinifu na kusahihisha makosa kabla ya kuwasilisha.
5. Kutoa Ushauri wa Kitaaluma – Kumwelekeza mwanafunzi kuhusu fursa za utafiti, machapisho ya kisayansi, na mitandao ya kitaaluma.
6. Kusaidia Katika Maandalizi ya Viva Voce – Kumpa mwongozo kuhusu jinsi ya kujibu maswali ya mtihani wa mdomo (defense) na kusimamia maandalizi yake.
7. Kuhimiza Nidhamu na Ufanisi – Kuhamasisha mwanafunzi kufuata ratiba ya kazi, kudhibiti muda, na kukamilisha utafiti kwa wakati.
8. Kuwa Kiungo na Chuo au Taasisi – Kuwasiliana na idara ya chuo kuhusu masuala ya kitaaluma, taratibu za chuo, na fursa za ufadhili au usaidizi mwingine.
9. Kumjengea Uwezo wa Kujitegemea – Kumfundisha mwanafunzi kuwa mtafiti huru, kufanya maamuzi ya kitaaluma, na kujenga msingi wa taaluma yake ya baadaye.
NOTE:Hapa hakuna sehemu yoyote inayoelekeza kuwa mwanafunzi atoe rushwa
hebu tuone wajibu wa supervisor akitumiwa kazi ya research proposal
Msimamizi (supervisor) wa mwanafunzi wa PhD anapopokea kazi ya dissertation (tasnifu), ana wajibu wa kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakidhi viwango vya kitaaluma na kitaaluma kabla ya kuwasilishwa rasmi. Wajibu wake ni pamoja na:
1. Kusoma na Kutoa Maoni ya Kina
• Kupitia kila sura kwa umakini ili kuhakikisha mtiririko mzuri wa mawazo na hoja.
• Kutoa mrejesho kuhusu nguvu na udhaifu wa kila sehemu ya tasnifu.
2. Kuhakikisha Ubora wa Utafiti
• Thibitisha kuwa utafiti unafuata misingi sahihi ya kitaaluma.
• Hakikisha kuwa maswali ya utafiti yamejibiwa kwa kina na kwa ushahidi wa kutosha.
3. Kusahihisha Makosa ya Kiufundi
• Kurekebisha makosa ya sarufi, uandishi wa kitaaluma, na upangaji wa sentensi.
• Kuhakikisha matumizi sahihi ya rejea na mtindo wa kunukuu (e.g., APA level one au saba ,MLA, Harvard).
4. Kutoa Mwongozo wa Kuboresha Mbinu za Utafiti
• Kushauri kuhusu uthibitisho wa data, tafsiri ya matokeo, na uchambuzi wa kina.
• Kuelekeza marekebisho katika sehemu ya mbinu (methodology) ikiwa kuna mapungufu.
5. Kuhakikisha Muundo wa Tasnifu Unafuatwa
• Kudhibitisha kuwa tasnifu imepangwa kulingana na mwongozo wa chuo.
• Kuangalia iwapo kuna utangulizi sahihi, sura za msingi, hitimisho, na mapendekezo.
6. Kuandaa Mwanafunzi kwa Viva Voce
na kumpa tarehe maalumu kuwa siku fulani utatakiwa kufanya vivavoce kwa kubandika matangazo kwenye mbao za chuo pamoja na kwenye websites kama mwanafunzi fulani atafanya viva voce hivyo umma unaalikwa
hii inafanywa na SAUT main campus na UDSM kwa ubora wa hali ya juu kabisa
• Kumpa mwongozo wa jinsi ya kutetea tasnifu yake mbele ya kamati ya mitihani.
• Kumuandaa kwa maswali yanayoweza kuulizwa na jinsi ya kuyajibu kwa weledi.
7. Kufanikisha Kuwasilishwa kwa Tasnifu
• Kuridhika kuwa kazi iko tayari na inaweza kuwasilishwa kwa ajili ya tathmini rasmi.
• Kusaini fomu za idhini na kuwasilisha kazi kwenye idara husika.
8.kujibu maulizo,kutoa ushauri pamoja kama una tatizo usaidiwe
kama haya supervisor hafanyi basi sio supervisor tena kama management haifatilii basi ni tatizo kubwa na linashusha ubora wa chuo
Usipende kuropoka jambo usilolijua. Kama Jambo halikugusi kaa kimya. Sipendi uchawa kwenye mambo serious. Naomba uache mizaha. Au unataka niweke wazi kila kitu ndio ujue jinsi OUT walivyo wazembe na wasiojua majukumu yao.
Nikuulize swali wewe mjuaji, unamfahamu mdada anaitwa Evelyn Shipela? Yupo pale DPGS? Nimeanza na huyo mdada asiyekuwa na haya aliyefanya chuo Cha baba yake. Ukitaka wengine nitakutajia mmoja baada ya mwingine.
Dadeki kumbe nimeingia cha kike, leo ndio nimemaliza kufanya application nataka nisome post graduate
View attachment 3277499
Mkuu lakini Master's by Thesis na PhD supervisors ni wawili sasa wewe
mbona unazungumzia supervisor mmoja je huyo mwingine umeshaongea
nae, mchango wake ni upi?
Kama Evelyn tu kakushinda basi tatizo siyo OUT wewe ndiyo kilaza waheeeed, jiangalie tena!!
Rudi nyuma anza upya kimkakati!
PhD siyo matako kwamba kila mtu lazima awe nayo!!! Frankly speaking, huna akili ya PhD wewe, nenda UD utarudi na thread ya malalamiko tena hapa!!
Sura ya Njaa Yupo OUT?Jamaa Hana sura ya njaa. Naogoppa akinichenjia.
Umeeleza vizuri lakini sehemu kama nimekuelewa vizuri kwa uelewa wangu inahusu vyuo zaidi ku fund hao supervisors vizuri hayo ni yao chuoKwa mfumo wa elimu wa vyuo vyetu Tanzania nadhani tungeishia tu kwenye bachelor degree then post- graduate programs watu waende kusoma nje ya nchi. Kwa kifupi vyuo vyetu haviko tayari bado kuhandle post graduate studies au programs zinazohusisha research. Factors ziko nyingi sana lakini ikiwamo uwezo binafsi wa hawa lecturers, kuna issues za motivation zinaingia hapa, taasisi zetu za elimu ya juu zinadedicate nguvu nyingi kwenye undergraduate programs zaidi kuliko hizo postgraduate programs, lakini pia teaching load kwa undergraduate programs ni kubwa kwa lecturers kiasi kwamba wanakosa muda wa kudeal na post graduates, imani ya kwamba elimu ya post graduate sio ya lazima na inahitaji efforts binafsi za mwanafunzi nayo ni factor nyingine. Kubwa zaidi kiutaratibu academic level inayohusisha research ina complications nyingi sana ambazo zinahitaji facilities nyingi sana ili kuweza ku accomplish objectives ikiwamo pesa (funding). Kiutaratibu kila hatua ambayo mwanafunzi anapiga kwenye usomaji wake lazima kuwe na uhusika wa moja kwa moja wa supervisor. Sasa wewe unandaa proposal peke yako supervisor hana habari, unatengeneza research design supervisor hahusiki, unaenda field kukusanya data supervisor katulia tu hiyo shule haiwezi kuisha vizuri that's why in most cases siziamini sana PhD zinazotolewa bongo maana supervisors hawafanyi kazi yao ipasavyo na huwezi kuwalaumu maana hizo kazi lazima alipwe vizuri kila hatua ili aweze kushiriki kikamilifu na vyuo haviwabani sana maana vinajua kuna sehemu havitimizi wajibu wake vizuri kwenye kuandaa mazingira mazuri ya supervisor kufanya kazi na mwanafunzi. Nje kila kitu kiko well organized na post graduate studies zote ziko well funded, supervisor anaachaje kufanya kazi maana hata kwake inampa credit. Kwa research degrees nashauri mtu aende tu nje kwasababu pia time frame zao ziko standard, kama PhD ni miaka 3,4 au 5 chuo na supervisor watahakikisha unamaliza ndani ya muda huo sio huku kwetu mtu anafanya PhD 7 years na bado hiyo PhD haina tija yoyote kwa mwanafunzi na taifa kwa ujumla. Naomba kuwasilisha 🙏