All the best Malila, nifikishie best wishes zangu pia kwa wenzako. songeni mbele MSIRUDI NYUMA
Bado hujanipata, sisi/mimi nazungumzia small scale ya eka 30 mpaka 50,ambazo kwa mishahara yetu bado hata kuziendeleza ni kazi ngumu,kama umepitia post zote utaona wengi wanalalamikia ugumu wa kilimo. Sasa hawa wachache wanaojitahidi ni sehemu ndogo sana ktk mamilioni ya Watz wanaotaka kuingia ktk kilimo cha Kisasa. Ukisoma sera za kilimo kwanza utaona kabisa,lengo ni kuwa na wakulima wenye tija ili taifa liweze kujitosheleza kwa chakula na hatimaye ziada iuzwe.
Ukitoka Mkuranga mpaka Lindi ni pori tupu,ukitoka Mikumi mpaka Ilula ni pori tupu,ukipita na Reli ya Tzr kuna mapori kibao yenye mito. Hoja yako inakosa nguvu kwa sababu,kilimo chetu hakitoshelezi mahitaji yetu. Hakuna aliye nyimwa ardhi ya kilimo. Watz tunapenda vitu laini kama DECI hivi,juzi kiongozi kawapa wawekezaji shamba la umma pale Usangu Chimala,badala ya kulima mpunga wao wanalima mibono,mbona hiyo husemi,bado sisi/mimi nasisitiza tukiweza kulima,basi tulime kilimo chenye tija cha mashamba makubwa,tuache paper work.
Leo pale Dar tunakula mpunga toka Thailand/India nk lakini mabonde yetu yenye maji yapo yapo pale Moro na Rufiji,na kesho jamaa toka middle east wanakuja kumegewa hekta 5000 walime.
Nadhani tunaongelea hii issue at two different levels naona hapa hatu communicate as we use different languages..so mi nasema leta tofali tujenge mnara we unasema we nipe sahani yangu mi nile maana nasikia njaa.... My dear analysis yako iko objective au subjective.
Eneo la Tanzania ambalo ni arable ni kiasi gani? Au ili mradi unapona mapori tu basi wewe unaingiza fyekeo na matrector? Ndo maana na sisitiza sustainability ya hizo project zenu... normally agenda kama hizo zina leta short term economic boosts lakini kuja kufanya restoration ya impact yake kwenye ecosystems will take a century tena ultimate results ni umaskini ulio mbaya zaidi kuliko uliopo sasa...Ideology ile ile ya high time preference ambayo mara nyingi ni thinking inayoletwa na poverty zaidi..For ur interest is to see millions of money now bila kuangalia how long you gonna get those millions and if can the receipients of these be extended to the next generation. Kumbuka hiyo theory ni ile ya technochrats ambao kwao wanafikiri kila kitu kiko perfectly substitutable can ask you for example; uki replace natural forest na plantation, biodiversity ya hiyo ecosystem itabakia vile vile? If that is not the case then what if kama ume wipe out key species ambao wako responsible na hiyo ecosystem resilience think of the effect on soil which is linked to hydrological issues; this is to say hayo maji unayoona yana tiririka sasa soon yanakauka yote na umesha affect may be micro climate so hata mvua maeneo hayo inaanza kua tabu sasa utaendelea kupata hayo mamilion unayotushawishi sasa?..this means discounting future.. Navyo maanisha generation ni zaidi ya hao descendants wako unaowafikiria zaidi. So you better use a good discounting factor when you think of these projects....It needs a proper economic analysis na siyo financial analysis tena ukifikiria cost benefit analysis kwa kutumia theory ya total economic value na see use value pekee amabyo iko zaidi katika monetary valuation na ku eliminate component ya non-monetary values.
Think of the population projection ya TZ after say 50 years, think of unsubstitutable component of the nature and the role of key species in ecosystem resilience which means by the means of research you should operate under safe minimum standards. Waulize wazungu kwanini pamoja na high tech yao environment imewa betray?
Nawatakia kila la heri...
Dada nimekupata,tunahitaji kuangalia kizazi chetu na vijavyo kuhusu mazingira. Bahati mbaya ni kwamba nchi yetu haijatenga maeneo ya kilimo/ufugaji. Sheria ya nchi yetu imetenga na inaendelea kutenga hifadhi za wanyama pori nk. Kama umesikiliza wabunge wanaotoka ktk maeneo ya wafugaji ktk bunge la sasa ungejua tatizo liko wapi. Mimi naamini nchi yetu ingesema wanaotaka kulima basi walime pale na kwa mpango huu,haya unayosema yasingekuwepo. Haya naomba unijibu,hivi kilimo kwanza ardhi yake iko wapi? Nakushauri nenda pale wizara ya kilimo kawape ushauri huo ili nchi yetu ipone na janga la uharibifu, na mimi nitakwenda niwape ushauri huu ili kwa sehemu yangu niokoe taifa.
Dada, hawa jamaa wanaokuja kulima toka nje ya nchi huwa mnawaambia ushauri huu au ni sisi tu Watz ndio mnatushauri? Na swali la mwisho tukiacha kulima kilimo cha mashamba makubwa nani atatulisha? Mimi nitajitahidi kulima kwa kutumia mbinu za kilimo hai. Ila kuwa na shamba kubwa ni lazima.
La mwisho ni hili,ktk kuhifadhi mazingira,mimi ni miongoni mwa Watz wanaopanda miti ya matunda,kivuli,mbao mingi kwa kila mwaka. Je wewe ktk kutunza mazingira yetu unashiriki kwa vitendo ? au unahamasisha basi.
dada kulima lazima nilime shamba kubwa sana,ila kama mdau wa mazingira ninajitahidi hata sasa/nitajitahidi kulinda mazingira nitakayoyatumia ili yasiharibike kwa kushiriki kilimo hai kama nilivyosema. Huko nyuma mimi nilishiriki kupinga sera za kilimo kwanza kwa mdahalo ila kama ujuavyo,viongozi wetu hawasikilizi kabisa maoni ya watalaamu wetu. Naamini peke yako huwezi ila tukishirikiana tutafanikiwa. Majukwaa ya watalaamu muhimu yamekuwa finyu sana.
Mapendekezo yangu kwako ni haya,ukionana na waziri husika mwambie,serikali itenge maeneo ya kilimo,ili wanaotaka kulima kwa scale kubwa wapewe kwa mikataba na maeneo yatolewe bure, kama wametenga maeneo ya kukaa fisi,wanashindwa nini kutenga maeneo ya kulima wakulima wa kati kama mimi ninavyotaka? ni suala la kuamua kuwa bonde la Rukwa wanaotaka kulima kwa scale kubwa waende huko na sisi serikali tunawapa huduma hizi,na bonde la Mbinga huko mkalime mahindi na Tunduru hivyo hivyo,tena watoe bure ili mtu asipolima ndani ya mwaka mmoja anapewa mwingine. Ninaposema mapori sina maana ya misitu,nina maana maeneo mazuri ya kilimo kama bonde la Ruvu,linatosha kulisha mji wa Dsm kama lingetumika,lakini liko tupu.
Tutakuwa na tea party (chai day) mimi na wenzangu pale Dsm mwezi ujao,tutakutana kujadiliana mafanikio ya msimu huu na vikwazo tulivyopambana navyo na namna nzuri ya kuingia msimu ujao. Vipi tukikualika utakuja ushiriki nasi siku hiyo? Ni masaa kidogo sana,kama mawili hivi au matatu. Chai tu ndio kiburudisho cha kusanyiko letu.
Asante kwa mwaliko wa chai... nitashukuru Mungu iwapo nitaweza just give me the dates venue and amount to contribute for that tea, for vya bure vinanikwaza maana vitaninyima uhuru wangu na hivyo principal yangu ya kwanza ni to pay for all what is not my right and never to pay for what is my leagal right.... Angalizo dont quote me wrong, sijasema kuhusu misitu tu hata mabonde ni sehemu ya ecosystem pia.. Habari mbaya kama unategemea kuweka investment huko fanya kwa uangalifu maana hayo mabonde yote soon tutayawekea leagal protection maana ndo moyo wa uchumi wa Taifa... Its said vita vijavyo vitakua vita vya maji, and some of us are working day and night to make sure that all wetlands and their catchment areas are leagerly protected.
Malila,dada kulima lazima nilime shamba kubwa sana,ila kama mdau wa mazingira ninajitahidi hata sasa/nitajitahidi kulinda mazingira nitakayoyatumia ili yasiharibike kwa kushiriki kilimo hai kama nilivyosema. Huko nyuma mimi nilishiriki kupinga sera za kilimo kwanza kwa mdahalo ila kama ujuavyo,viongozi wetu hawasikilizi kabisa maoni ya watalaamu wetu. Naamini peke yako huwezi ila tukishirikiana tutafanikiwa. Majukwaa ya watalaamu muhimu yamekuwa finyu sana.
Mapendekezo yangu kwako ni haya,ukionana na waziri husika mwambie,serikali itenge maeneo ya kilimo,ili wanaotaka kulima kwa scale kubwa wapewe kwa mikataba na maeneo yatolewe bure, kama wametenga maeneo ya kukaa fisi,wanashindwa nini kutenga maeneo ya kulima wakulima wa kati kama mimi ninavyotaka? ni suala la kuamua kuwa bonde la Rukwa wanaotaka kulima kwa scale kubwa waende huko na sisi serikali tunawapa huduma hizi,na bonde la Mbinga huko mkalime mahindi na Tunduru hivyo hivyo,tena watoe bure ili mtu asipolima ndani ya mwaka mmoja anapewa mwingine. Ninaposema mapori sina maana ya misitu,nina maana maeneo mazuri ya kilimo kama bonde la Ruvu,linatosha kulisha mji wa Dsm kama lingetumika,lakini liko tupu.
Tutakuwa na tea party (chai day) mimi na wenzangu pale Dsm mwezi ujao,tutakutana kujadiliana mafanikio ya msimu huu na vikwazo tulivyopambana navyo na namna nzuri ya kuingia msimu ujao. Vipi tukikualika utakuja ushiriki nasi siku hiyo? Ni masaa kidogo sana,kama mawili hivi au matatu. Chai tu ndio kiburudisho cha kusanyiko letu.
Malila,
Hao Wakulima mko wangapi?Je wapo humu Ktk JF,naomba list yao,mimi ningependa kuja ,ila nakunywa Kahawa,(ile ya kienyeji)tupe Venue and Time
Malila why tarehe 5? nimecheck diary inaniambia ni katikati ya week Haiwezekani muipeleke tarehe 8 ili hata sie wa idodomya tukajimuvuzisha
Kilimo Kwanza ni SiHasa, ni usemi tu wa wataalamu wa kuunda sera za kisiasa na kulima kwenye madaftari,89% ya pesa zitaliwa katika expert /tecknikal support,facilitation,mahotel ya bagamoyo na kununua magari,na matangazo,Hivi kwenye kilimo kwanza kuna funds za kuwezesha wakulima? Au maneno matupu?
Felister,
Asante sana kwa ushauri wako murua.............huu ndio uzuri wa JF.............shule kila kukicha...........sio kuangalia upande mmoja tu............hisia yangu inaniambia uko/ulikuweko sana kwenye maeneo ya utafiti ...........kama assumption yangu kuhusu wewe ni sahihi............je kuna maeneo hapa nyumbani ambayo yametengwa/highlighted kuwa protected kwa kuwa ni highly sensitive kwenye ecosystem................je kama yapo information hizi ziko wapi............
Wakuu hii argument...................iliyoletwa na Felister ni muhimu kuizingatia...................
Chai yetu tutakunywa 5 may 2010,pale dar,mmoja wetu anashughulikia venue na pengine gharama za chai zitajulikana muda si mrefu. Je huoni kuwa tumechelewa kutoa hiyo sera ya kuyalinda mabonde yetu? Ngoja niwashitue na wenzangu kuwa mabonde tuyakwepe kwa sababu tutalia muda si mrefu. Vipi kuhamisha maji kwa mifereji mtaruhusu au nayo itakuwa hairuhusiwi?
Malila ,umeanzisha topic na kupotea, kaka au ndo umeamua KURUDI NYUMA, vipi chai meeting ilitokea ,if yes wangapi walifika,na waliokosa kufika walisemaje ?
umeahidi kutoa feed bak yet umekaa kimya or network not reachable