SIRI YA UPONYAJI (UGONJWA WOWOTE)

Marco Seth

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2022
Posts
4,680
Reaction score
5,653
Tumezoea Kuona watu wanaumwa
Na kutegemea Dawa sana
Na wengine wanaenda kwa waganga kumbe wanaongeza matatizo

Kwa Nguvu za Mungu hakuna lisilowezekana
-Imani
Kuwa na Imani na unapo sali
Na pia Omba toba usamehewe dhambi zako

Math 9:22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.


Ukisoma luka8:27-33
Utagundua Mtu aliteseka Kwa sababu ya Mapepo
Kemea mapepo yatoke na kujiondoa kwenye vifungo

Kila Ugonjwa unao uona Unaanzia Rohoni
Mapepo yakipata nafasi ndani ya Mtu yanaacha uharibifu
Kwenye Ulimwengu wa Kiroho
Alf visingizio vya kimwili vinajitokeza kuonyesha kwamba unaumwa ili
Uamini kweli unaumwa


Kuna vifungo vingi unaweza ukawa umefungwa pasipo wewe kujijua
Mtu unakutana naye tu rafiki
Alf usiku anakuja kukufanyia mambo dah Wana Jf dunia imeharibika. Kupost post vitu watu wanakufuatilia kwenye ulimwengu wa Kiroho ila kwa hili wachache wanajua


Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


Kwa nini umekemea sana na bado ugonjwa haujapona au huyo mtu hajaponywa?
Hakikisha unachoomba ni sahihi
Na ikiwezekana Muombe Mungu akuonyeshe chanzo cha tatizo ni nini
Ili unaposali uhit kwenye Target ya chanzo cha Matatizo

Kuna siku nilikuwa naumwa
Nikawa nasali ila sikujua chanzo chake ni nini
Nikagundua Chanzo ni kulikuwa na Mtego kwenye Chakula kupitia ndoto nilijua .Chakula kwenye hiyo mahafali ya form6 . Na wale waliokula wengi sana waliumwa

Usikate tamaa na kusali endelea kuamini na Mungu akuonyeshe zaidi kuhusu Tatizo ulilonalo

Kwa wale wa Rohoni wanaelewa zaidi na zaidi ya hapa nilivyoelezea


Unapotembea sali kuna mitego mingi unapita kwenye maeneo yaliyowekewa uchawi

Unapo kula ombea chakula
Kuna maroho yanapandikizwa humo ndio maana usiku unaota umelishwa vyakula
Madhara yake yanakuja kujionyesha kimwili
 
Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
 
Back
Top Bottom