Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO



Kaka nimekupata: Lakini huoni mikono ya CCM ikikatiliwa mbali hata hivyo vyeo vinavyompatia sifa hatavipata??. Umeona ya Mchhungaji Msigwa?? We need sometimes to be considerate and rational on important issues!!
 
Hivi haya Magazeti yanayoandika habari kama hizi kwanini wasingepeleka hii taarifa polisi kwa uchunguzi zaidi? pia kwanini mwandishi wa habari kama hii asikamatwe na kuhojiwa kwa uchochezi? je uchochezi upo CDM tu? nawasilisha wakuu
 
Umeambiwa utumie muda kuimarisha chama chako

Acha ujinga kijana, Mimi si muumin wa CHADEMA tu bali ni muumini watu wanaosimamia ukweli ambao wapo CHADEMA mfano Rais wangu Dr.W.Slaa, Sasa yanapotokea mazingira yenye utata kutoka kwa wanafiki kama ww kwa lengo la kuwachafua viongozi ambao wanatupigania, Mimi hapo huwa sileti unafiki bali ni kutoa ukweli tu, Ndio maana huwa nasema mtu yeyote anayepinga na kudharau kazi aliyoifanya Ben Saanane mpaka tukagundua uozo wa masalia basi mtu huyo atakuwa ni mwendawazimu zaidi ya pepo mchafu.
 
Last edited by a moderator:
Mateka wa fikra.
 
wewe sio muumini wa CDM ni mfuasi wa DR pamoja na kijakazi wake Benn.
 
Bwana Mtela, Saanane na Shonza njooni huku mmevuliwa nguo hadharani na kila mtu anatazama viungo vyenu vya uzazi bila hata malipo!! Hongera kamanda Zitto kwa kuusema mtazamo wako hadharani, wengine wangefukia chini ya kapu.
 
Kaka nimekupata: Lakini huoni mikono ya CCM ikikatiliwa mbali hata hivyo vyeo vinavyompatia sifa hatavipata??. Umeona ya Mchhungaji Msigwa?? We need sometimes to be considerate and rational on important issues!!

Do you mean mchungaji msigwa amefanya kosa,amekosa kuwa rational? do you mean zitto anapata favor from ccm? i dont thnk so..
 
...Sidhani kama CCM wamewahi mhofia Zitto. Bali hilo husemwa sana na CCM wenyewe (ZeMacopolo, Ritz nk) ili kumpa kichwa Zitto aikoroge CDM
 
Namwamini Zitto juu ya hili. Hakuna hata picha moja inayoonyesha Saanane amewahi kukutana na Zitto.

Mwambampa na Shonza pia waliandika Saanane alitaka kukutana na Zitto ila Zitto alikwepa.

Kwahayo nafikiri Zitto hajawahi kuonana uso kwa uso na Saanane.

 
kwa kweli zitto umechukua uamuzi wa busara, maana ungenyamaza muda mrefu ingeleta madhara kwani haya yalishatokea long time kwenye forum. Hata hivyo unastaili sifa kwani umekomaa zaidi, hawa vijana wachafuzi, wabaka siasa naona mtaji wao umeishia hapo. kama ni shule wamepata mzinga. Endelea kuwapuuza maana sio wazuri kwako na kwa chama kwani tunakupenda sana kama mpiganaji wetu kijana.
 
kwa serikali ya ccm uchochezi ni upi?
au kwa vile gazeti la mshkaji?

LIFUNGIWE.
 
Pamoja na kwamba Zitto ameongea mambo mengi sana ya maana,lakini pia kwenye mjadala mmoja ambapo issue ya uhusiano wake yeye na viongozi wenzake ilipoibuliwa,aliweka wazi kuwa "majaribio ya kumuuwa yalishafanyika",lakini hakutaja kiongozi mwenzake yoyote yule kwamba anahusika na majaribio hayo.Lakini hoja ilikuwa ni uhusiano wake na ushirikiano wakae na viongozi wenzake.nga

Wengi walishindwa kuunganisha majaribio hayo na wazee wa mabwepande kwasababu pia hatukuona sababu ya wazee hao kutaka kumuuwa Zitto,na wengine hata walidiriki kuleta hoja ya uhusiano wake na Rama.

Hapa kwenye mada hii,anasema kuwa Dr Slaa hana sababu ya kumuuwa,lakini hajasema kuwa haamini kuna viongozi wenzake wanaotaka kumuuwa kwasababu amesema kama wako watu wowote wale wanaotaka kufanya hivyo,yeye hajali kwani kama amepangiwa kufa kwa kuuwawa, ni sawa tu na akasema kwamba kuuwa mwili si kuuwa mawazo na fikra zake.

Hata hivyo aliwahi kusema pia atakayemuuwa huko alikotoka hakutabaki hata panya.

Ndo siasa za wanasiasa...

However sisiti kumpongeza Zitto kwa kuwakemea masalia.
 

Ndugu yangu Zitto nimesikitika sana kwa kuja kulijibu gazeti hapa JF. Habari iliyoandikwa gazetini ilikuwa na nia wewe uje uijibu stori yenyewe na sasa ni kama stori imefanikiwa. Nadhani usahihi wewe ulipaswa kuwa kimya, kimya, kimya, kimya tena kimya sana. Kama umesisitizwa au kushinikizwa ujibu na Dr Slaa ama na yeyote aliye juu yako kiuongozi ndani ya CDM ulichofanya ni sawa. Ila tu nakukumbusha kuwa stori iliyotungwa haikusema wewe ulikuwepo ama ulienda kwenye mkutano ambao pengine ungepewa sumu. Nakumbuka huko nyuma iliwahi kuandikwa katika mkutano au kikao hicho wewe hukufika - hapa nashangaa unajitetea kama vile unatuhumiwa ulikuwepo katika mkutano huo. Saa Nane aliwahi kukiri mnafahamiana lakini hapa umechemka kuwa hujawahi kuwa naye na inaonesha kama unataka kusema humfahamu kabisa.

Jambo kubwa ambalo mimi nakushauri kikawaida tu kwa kuwa sina mahusiano yeyote na wewe zaidi ya wewe kuwa binadamu mwenzangu, watu wanapopanga kuua huwa hawasemi, so ni siri yao. Kwa maana hiyo huwezi kupinga assumption kuwa pengine Dr Slaa ni kweli alikuwa na mkakati huo.Ni Alkaida labda ma Alshababi sijui ndiyo huwa wanajitangaza kuwa wamehusika na mauaji au maafa fulani. Level hiyo ya ugaidi hapa kwetu hatujaifikia, tunaenda kimya kimya tu. The way ulivyokanusha huo uvumi si ajabu siku ingine ukaja kukanusha kuwa hukukanusha, haya mambo inawezekana yapo, sio ya kupuuzwa bali ni kuchukulia tahadhari na wala sio kujifariji kwa kukanusha kuwa hayapo.

Avanti me.
 
Hakumaanisha mtu huyo lazima awe kiongozi bali mwanachama yeyote mfano ni Ludovick aliyeamua kuwa msaliti na inawewzekana na Lwakatare kama naye alisaliti

Mkuu nimekupata pamoja na kwamba una muhukumu Ludovick mapema kwa sababu ukiangalia mashitaka mahakamani, wote wana mashitaka sawa lakini wanasheria wanaowatetea ni tofauti isipokuwa moja tu ndilo tofauti na mengine, halafu lina muhusu Lwakatare. Hata hivyo mpaka pale kesi itakapoanza kusikilizwa, ndiyo tutafahamu zaidi.
 

iilogical ARGUMENT
 
..labda angalizo tu kwa viongozi wa chadema: Ebu angalieni watu wanavyokuwa excited wanapoona mnakana maovu na kuonyesha kutaka kukijenga chama chenu...hu ndio mtazamo wa wanachadema woote TZ.....kila mtu mwenye mapenzi na kutaka mambo mema TZ kupitia upinzani anataka kuona viongozi wao wakiwa safi mbele ya jamii....bila scandles...au hujuma za kijinga zinazoweza kuondoa lengo zima la mageuzi nchi hii......Hamna mtu mwenye akili timamu anayependa kuona kiongozi wake wa chama anaandikwa kwa mabaya tu kila siku.....watu wanataka mageuzi ya kweli kwa kupitia viongozi wao wenye umoja na mapenzi baina yao na kwa chama chao........ebu oneni watu wanavyowatakia mema....na kwa maana hii wanataka muwafanyie mema....Ni angalizo kwa viongozi wote wa chadema..kwa ngazi zote...maana mnasoma comment za watu humu......hizi ni representation za watu wenu koote TZ........
 
Hili ndilo tamko la ZZK dhidi ya habari ya gazeti la Mtanzania na juu ya Mtela Mwampamba na Juliana Shonza

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ' SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA' na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini' dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza'. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013
 
Hongera kamanda Zzk,sahihisho kwako mkuu ni kuwa hayo masalia tuliyafukuza na sio kwamba yamehama chama!!!!Aluta continue!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…