Siri nzito yafichuka CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri nzito yafichuka CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 4, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mashaka Mgeta | Nipashe Jumapili | 3rd June 2012

  Maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imebainika kuwa ni sehemu ya mikakati yake inayolenga kuibua chuki za wananchi na kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao.

  Vyanzo vya habari ndani vya Chadema ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, vimelieleza NIPASHE Jumapili kuwa, chama hicho kilifanya tathmini na kubaini kasoro zilizochangia kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

  Miongoni mwa kasoro hizo, ni ari ndogo iliyojitokeza kwa wananchi kulinda kura za wagombea urais na ubunge kupitia Chadema.
  "Ili wananchi wawe tayari kuona umuhimu wa kulinda kura za chama cha siasa, inabidi wawachukie watawala, sasa tunachokifanya ni kueleza upungufu wa chama tawala ili wananchi waamke, waichukie CCM," kilieleza chanzo hicho.

  Hata hivyo, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mahakama jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitaendelea kuwachochea wananchi kuiasi CCM na kukiunga mkono chama chake.

  Mbowe alisema, "wanasema Mbowe ni mchochezi, wanasema Chadema inapandikiza chuki, mimi na chama changu tutaendelea kuuhamasisha umma kuondokana na woga, wawachukie watawala walioshindwa kuwaletea maendeleo."

  Chadema imekuwa na utaratibu wa kuandaa maandamano na mikutano ya hadhara kupitia kile kinachojulikana kama operesheni maalum, mathalani kwa sasa ikijulikana kama Operesheni Okoa Kusini.

  KUCHUKUA MFUMO WA CCM

  Kwa upande mwingine, mkakati uliobuniwa na kuzinduliwa na Chadema, ukijulikana kama Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) umetajwa kama wenye lengo la kukisimika chama hicho hadi kwenye ngazi ya ubalozi, kama ilivyo kwa CCM.

  Kupitia M4C Chadema inajikita kwa ‘kuvuna' wanachama na kusimika uongozi katika ngazi tofauti kuanzia mabalozi, matawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hatimaye taifa.

  Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.

  Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.

  "Tunapoingia ndani ya jamii kufikia ngazi za msingi, tawi na kata, tutajihakikishia kuichukua nchi kwa urahisi zaidi," kilieleza chanzo hicho.

  Chadema imetoa maelezo ya taratibu za uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ngazi za msingi na matawi, kikitumia ibara ya 11-1 ya chama hicho na kuzisambaza nchi nzima.

  Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa, alithibitisha kuchapishwa kwa maelezo hayo na kwamba yatafanikisha chaguzi hizo kufanyika kwa mujibu wa Katiba.

  Maelezo hayo yanataja Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.

  Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11 mwakani (mkoa).

  Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake (Bawacha) na Wazee.
  Chanzo kimeeleza kuwa kupatikana kwa uongozi katika ngazi hizo kutaiwezesha Chadema kuwa na mtandao utakaohusika katika kulinda nafasi za wagombea uwenyekiti wa mitaa, vitongoji na vijiji, udiwani, ubunge na urais.

  Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwembe Mmoja (CCM) mkoani Mtwara , Abdallah Suleiman Mnyalu, alisema kazi za kisiasa hususani kukutana na kuzungumza na wananchi, zitaiathiri CCM katika chaguzi zijazo.

  Alipotakiwa na NIPASHE Jumapili atoe maoni yake kuhusu athari za Chadema katika ngazi za msingi kwenye jamii, Mnyalu alisema chama hicho kinafanya kazi zilizopaswa kufanywa na CCM, lakini chama hicho tawala kimelala.

  "Wenzetu hawa wanapita na kukutana na wananchi, lakini sisi wenye dola hatufanyi hivyo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu," alisema.

  Mnyalu alisema pia kuwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi za msingi vimechochea chuki ya wananchi kwa chama tawala, hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani hususani Chadema kuungwa mkono.

  MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO

  Imebainika kuwa Chadema imejizatiti kutumia njia mbalimbali kuwafikia wapiga kura, wakiwemo wasiojitokeza na kushiriki shughuli za kisiasa hadharani.

  Kupitia mkakati huo, imeelezwa kuwa chama hicho kitatumia njia ya mitandao ya kijamii iliyopo kwenye mawasiliano ya kisasa, kupenyeza kampeni na hoja zake.

  MKAKATI WA KUJIENEZA

  Kikiwa katika Operesheni Okoa Kusini inayoendelea kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, Chadema kinawatumia viongozi na makada wake kufika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata ambapo wanazungumza na wananchi, kufungua matawi na kusimika uongozi wa muda.

  Jana, Chadema kilichoanza ziara zake mkoani Mtwara Mei 27, mwaka huu, kimeingia mkoani Lindi ambapo kitafanya mikutano ya hadhara na kufungua matawi yake hadi Juni 9, mwaka huu kitakapofanya mkutano wa hadhara mjini Lindi.
   
 2. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Sasa kuna siri gani nzito hapa. Waandishi wengine bwana!! Nilifikiri gazeti la udaku kumbe...
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mbado sijaona hiyo siri
   
 4. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,799
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mie Mpaka nimevaa na miwani, sijaona hiyo siri. Nimejaribu kutranslate kwa lugha nyingine bado sijaona hiyo siri.

  Magazeti bwana, ndio maana mie sikuhizi naishia JF tu.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... Mgeta, hii ndio siri nzito - my foot!! Siri ya mwizi wa twiga za Tanzania kuhamishia Uarabuni utauandikia lini??
   
 6. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,560
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Mashaka, Sasa ulitaka wafanyaje? Uliona chama gani hakihamasishi watu? Sasa waipende CCM kwa vile mafisadi?
   
 7. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,005
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Hivi hii ni siri sasa? Mbona kwenye mikutana wanasema wazi kwamba wanajiandaa kuchukua dola?
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  sioni siri labda sir sirini
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hata mimi sijaona siri
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Du, ngoja nijaribu kutranslate kwenda kilatini labuda nitaona hiyo siri, make nimetumia kiswahili sijaona, nimetranslate kwenda kingereza sijaona, ngoja nijaribu kilatini labuda nitbahatika kuon ahiyo siri
   
 11. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kwani nn maana ya siri wandugu?
   
 12. M

  Mantisa Senior Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Aisee kuna watu hawana kazi. Maelezo mengi kumbe pumba tu

  Itabidi akajipange tena
   
 13. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,799
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Ukiiona naomba nitupie na mimi, maana Im still searching..........
   
 14. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hii siri ni siri haswa, mpaka haionekani kwa mimacho yetu ya kibinadamu!
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Maaaa, mbavu yangu!!!!!!!!!!!! Kwa kadiri nijuavyo mimi, Mgeta hawezi kuandika kituko kama hiki labda 'KABANDIKIWA TU KESI' na Mhariri wa zamu.

   
 16. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  siri yenyewe hii hapa

   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa inabidi hawa chadema wachunguzwe hizi fedha za kampeni inayoanza mapema hivi wanazitoa wapi? kikijulikana chanzo chao cha fedha, mchezo utakuwa umekwisha. Kuna mengi yamejificha.
   
 18. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  He, hiyo siri ilyofichuka umesahau kuiandika, rudia tena uiandike!
   
 19. M

  MTK JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Kumbe kweli na wewe haupo; hapo kuna siri gani?!! tafadhali wacha kuwa mbadhirifu wa maneno! post kitu chenye maana na uzito for great thinkers to put their minds in to gear kabla hawajachangia hoja.
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,531
  Likes Received: 10,444
  Trophy Points: 280
  kwani nafasi za ukuu wa wilaya zimeisha.?
   
Loading...