Siri nzito yafichuka CHADEMA

Najuta kupoteza muda kwa kusoma habari hii yooote na kuambulia patupu. Hili gazeti nalo nalipeleka kwenye orodha ya magazeti ya udaku.
 
tunatoa sana michango mkuu, umezoea uwizi wa magamba!

Uchunguzi utabaini kama ni michango yenu tu au kuna njia zingine zisizo za halali.

TUNTEMEKE, endelea na mzigo ingawa wamejaribu kuweka kauzibe huko lakini tunaijuwa kazi nzuri unayoifanya na tuna-uhakika hawakuwezi. Tuko pamoja nawe.
 
Mie Mpaka nimevaa na miwani, sijaona hiyo siri. Nimejaribu kutranslate kwa lugha nyingine bado sijaona hiyo siri.

Magazeti bwana, ndio maana mie sikuhizi naishia JF tu.
Between lines bonge la promo. mwandishi amechagua headline nzuri na imemfanya kila mtu asome wakiwemo magamba
 
Yaani wakati najaribu kuisoma hii habari,..
nilipatwa na wasiwasi kidogo nikahisi hiyo siri nzito ni ipi haswa.

Kumbe bila kutarajia mwandishi ameishia kuandika mwendelezo wa CHADEMA kuwafungua watu upeo wao katika siasa...

Hongera mwandishi wetu kwa kuifatilia CHADEMA!
 
nimejaribu kumulika kwa tochi natafuta siri sijaiona, nimevua miwani nimesoma tena sioni nimeuliza na wenzangu sioni siri, waandishi wengine bwana, hovyoooooooooooo
 
Kwanza kabisa inabidi hawa chadema wachunguzwe hizi fedha za kampeni inayoanza mapema hivi wanazitoa wapi? kikijulikana chanzo chao cha fedha, mchezo utakuwa umekwisha. Kuna mengi yamejificha.

Jibu lake ni dogo sana peoplessssssssssssss power! hiyo ndiyo siri ya mafanikio kwa chama kujengwa na nguvu ya wanachama bila kutumia pesa chafu.
 
Mashaka Mgeta nina mashaka na wewe.

U DC mbona umeshapita au bado ndoto zinakurudia?
Hahahahaaaaaa tutututttuuuuuu kwi kwik kwiwwwwwiiiiiiii..........................................
Ukanjanja una mambo kweli.........
 
Hakuna siri hapa, nia ipo wazi ni kuwadosha ccm.
Nadhani uyu mwandishi bado yuko field\mazoezi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mashaka Mgeta | Nipashe Jumapili | 3rd June 2012

Maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imebainika kuwa ni sehemu ya mikakati yake inayolenga kuibua chuki za wananchi na kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Vyanzo vya habari ndani vya Chadema ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, vimelieleza NIPASHE Jumapili kuwa, chama hicho kilifanya tathmini na kubaini kasoro zilizochangia kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Miongoni mwa kasoro hizo, ni ari ndogo iliyojitokeza kwa wananchi kulinda kura za wagombea urais na ubunge kupitia Chadema.
"Ili wananchi wawe tayari kuona umuhimu wa kulinda kura za chama cha siasa, inabidi wawachukie watawala, sasa tunachokifanya ni kueleza upungufu wa chama tawala ili wananchi waamke, waichukie CCM," kilieleza chanzo hicho.

Hata hivyo, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mahakama jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitaendelea kuwachochea wananchi kuiasi CCM na kukiunga mkono chama chake.

Mbowe alisema, "wanasema Mbowe ni mchochezi, wanasema Chadema inapandikiza chuki, mimi na chama changu tutaendelea kuuhamasisha umma kuondokana na woga, wawachukie watawala walioshindwa kuwaletea maendeleo."

Chadema imekuwa na utaratibu wa kuandaa maandamano na mikutano ya hadhara kupitia kile kinachojulikana kama operesheni maalum, mathalani kwa sasa ikijulikana kama Operesheni Okoa Kusini.

KUCHUKUA MFUMO WA CCM

Kwa upande mwingine, mkakati uliobuniwa na kuzinduliwa na Chadema, ukijulikana kama Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) umetajwa kama wenye lengo la kukisimika chama hicho hadi kwenye ngazi ya ubalozi, kama ilivyo kwa CCM.

Kupitia M4C Chadema inajikita kwa ‘kuvuna' wanachama na kusimika uongozi katika ngazi tofauti kuanzia mabalozi, matawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hatimaye taifa.

Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.

Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.

"Tunapoingia ndani ya jamii kufikia ngazi za msingi, tawi na kata, tutajihakikishia kuichukua nchi kwa urahisi zaidi," kilieleza chanzo hicho.

Chadema imetoa maelezo ya taratibu za uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ngazi za msingi na matawi, kikitumia ibara ya 11-1 ya chama hicho na kuzisambaza nchi nzima.

Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa, alithibitisha kuchapishwa kwa maelezo hayo na kwamba yatafanikisha chaguzi hizo kufanyika kwa mujibu wa Katiba.

Maelezo hayo yanataja Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.

Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11 mwakani (mkoa).

Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake (Bawacha) na Wazee.
Chanzo kimeeleza kuwa kupatikana kwa uongozi katika ngazi hizo kutaiwezesha Chadema kuwa na mtandao utakaohusika katika kulinda nafasi za wagombea uwenyekiti wa mitaa, vitongoji na vijiji, udiwani, ubunge na urais.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwembe Mmoja (CCM) mkoani Mtwara , Abdallah Suleiman Mnyalu, alisema kazi za kisiasa hususani kukutana na kuzungumza na wananchi, zitaiathiri CCM katika chaguzi zijazo.

Alipotakiwa na NIPASHE Jumapili atoe maoni yake kuhusu athari za Chadema katika ngazi za msingi kwenye jamii, Mnyalu alisema chama hicho kinafanya kazi zilizopaswa kufanywa na CCM, lakini chama hicho tawala kimelala.

"Wenzetu hawa wanapita na kukutana na wananchi, lakini sisi wenye dola hatufanyi hivyo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu," alisema.

Mnyalu alisema pia kuwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi za msingi vimechochea chuki ya wananchi kwa chama tawala, hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani hususani Chadema kuungwa mkono.

MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO

Imebainika kuwa Chadema imejizatiti kutumia njia mbalimbali kuwafikia wapiga kura, wakiwemo wasiojitokeza na kushiriki shughuli za kisiasa hadharani.

Kupitia mkakati huo, imeelezwa kuwa chama hicho kitatumia njia ya mitandao ya kijamii iliyopo kwenye mawasiliano ya kisasa, kupenyeza kampeni na hoja zake.

MKAKATI WA KUJIENEZA

Kikiwa katika Operesheni Okoa Kusini inayoendelea kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, Chadema kinawatumia viongozi na makada wake kufika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata ambapo wanazungumza na wananchi, kufungua matawi na kusimika uongozi wa muda.

Jana, Chadema kilichoanza ziara zake mkoani Mtwara Mei 27, mwaka huu, kimeingia mkoani Lindi ambapo kitafanya mikutano ya hadhara na kufungua matawi yake hadi Juni 9, mwaka huu kitakapofanya mkutano wa hadhara mjini Lindi.

nipashe sikuhizi limekuwa gazeti la kimajungu sana...
 
hao ndio waandishi wetu makanjanja
mkapa alikuwa anawatukana sana waandishi wasio na viwango hatukumwelewa
ndo kama hivi.
 
Hivi hii ni siri sasa? Mbona kwenye mikutana wanasema wazi kwamba wanajiandaa kuchukua dola?

Yaani mwandishi huyu kaniharibia siku yangu na kuanzia leo nimesikitika kwamba kumbe Ipp Media nayo haiko nyuma ina MAKANJANJA na mmoja wao ni huyu.
 
Kwanza kabisa inabidi hawa chadema wachunguzwe hizi fedha za kampeni inayoanza mapema hivi wanazitoa wapi? kikijulikana chanzo chao cha fedha, mchezo utakuwa umekwisha. Kuna mengi yamejificha.


Pambaf zako.
Wewe ni Zoba au ni zomba?

Mbona unaongea pumba. Kwani CCM nani kawakataza kwenda kwenye matawi na mashina yao kuhamasisha wanachama wao wasihamie CDM? Tunajua CCM wana hela za ufisadi na hela ya Ruzuku. Je, wakianza nao kuzunguka nchi nzima utasema wachunguzwe ati wapi wanapata pesa?

CHADEMA ni chama makini. Kwanza kabisa kinapata ruzuku kulingana na idadi ya Wabunge walio nao lakini pia wana pesa inayotokana na Wasamaria wema kama kina SABODO wanaojitolea kuichangia CHADEMA tena kupitia mabenki na mitandao ya simu kama Tigo-pesa,M-pesa, Z-pesa n.k.

Kwa hiyo mawazo yako ya kusema wachunguzwe wapi wanapata pesa ni upuuzi mtupu!
 
Kama kwako ni siri una matatizo huo ni mkakati sui siri. Jifunze kupambanua mambo usiyachukue kama yalivyo
 
Yaani mwandishi huyu kaniharibia siku yangu na kuanzia leo nimesikitika kwamba kumbe Ipp Media nayo haiko nyuma ina MAKANJANJA na mmoja wao ni huyu.


You know what? Kiwete amesha waroga Waandishi wa habari baada ya KUWAPA HONGO AU RUSHWA YA U-DC.
Kwa hiyo kinachofanyika sasa ni kila mwandishi kuipigia debe CCM na kuviponda vyama vya upinzani hasa CHADEMA ili mwisho wa siku na yeye aukwae U-DC. Kwa kweli CCM inakoelekea ni giza tupu!!!
 
Back
Top Bottom