Siri nzito yafichuka CHADEMA

Siri nzito yafichuka CHADEMA

Nipashe wanaugua ugonjwa gani? Kuna siri gani hapa kama sio kuabisha tasnia ya uandishi wa habari?
Any potilical party inatakiwa ifanye kazi wanayofanya CHADEMA sasa hivi, sasa nini wasichoelewa hawa Nipashe? I am glad sikununua hili gazeti maana ningewafuata kudai hela yangu.
 
huyu mwandishi ameandika siri ambayo yeye mwenyewe haifaham.
 
Kwa ujinga huu nimegoma kununua wala kusoma gazeti la Nipashe kwa wiki hii yote.. Kuondoa hasira..
 
hiv mwandish mpk kutoa habari....huwa inaptiwa na nan na nan??na huwa kwel wa cfaa za kufanya hivyo...??
 
Scrap!

Mimi sioni siri hapo. Kujenga chuki ndio nia hasa na siku zote Dr. Wa ukweli husema hivyo kwamba watawaambia wananchi ubaya wa serikali yao ili waichukie, sasa huyu JUHA aliyehariri hii habari na kuitoa anajiona amevumbua nini kipya hapa cha kutujazia ukurasa na kuuza kwa sh 500?
 
Mashaka Mgeta | Nipashe Jumapili | 3rd June 2012

Maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imebainika kuwa ni sehemu ya mikakati yake inayolenga kuibua chuki za wananchi na kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Vyanzo vya habari ndani vya Chadema ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, vimelieleza NIPASHE Jumapili kuwa, chama hicho kilifanya tathmini na kubaini kasoro zilizochangia kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Miongoni mwa kasoro hizo, ni ari ndogo iliyojitokeza kwa wananchi kulinda kura za wagombea urais na ubunge kupitia Chadema.
“Ili wananchi wawe tayari kuona umuhimu wa kulinda kura za chama cha siasa, inabidi wawachukie watawala, sasa tunachokifanya ni kueleza upungufu wa chama tawala ili wananchi waamke, waichukie CCM,” kilieleza chanzo hicho.

Hata hivyo, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mahakama jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitaendelea kuwachochea wananchi kuiasi CCM na kukiunga mkono chama chake.

Mbowe alisema, “wanasema Mbowe ni mchochezi, wanasema Chadema inapandikiza chuki, mimi na chama changu tutaendelea kuuhamasisha umma kuondokana na woga, wawachukie watawala walioshindwa kuwaletea maendeleo.”

Chadema imekuwa na utaratibu wa kuandaa maandamano na mikutano ya hadhara kupitia kile kinachojulikana kama operesheni maalum, mathalani kwa sasa ikijulikana kama Operesheni Okoa Kusini.

KUCHUKUA MFUMO WA CCM

Kwa upande mwingine, mkakati uliobuniwa na kuzinduliwa na Chadema, ukijulikana kama Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) umetajwa kama wenye lengo la kukisimika chama hicho hadi kwenye ngazi ya ubalozi, kama ilivyo kwa CCM.

Kupitia M4C Chadema inajikita kwa ‘kuvuna’ wanachama na kusimika uongozi katika ngazi tofauti kuanzia mabalozi, matawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hatimaye taifa.

Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.

Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.

“Tunapoingia ndani ya jamii kufikia ngazi za msingi, tawi na kata, tutajihakikishia kuichukua nchi kwa urahisi zaidi,” kilieleza chanzo hicho.

Chadema imetoa maelezo ya taratibu za uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ngazi za msingi na matawi, kikitumia ibara ya 11-1 ya chama hicho na kuzisambaza nchi nzima.

Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa, alithibitisha kuchapishwa kwa maelezo hayo na kwamba yatafanikisha chaguzi hizo kufanyika kwa mujibu wa Katiba.

Maelezo hayo yanataja Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.

Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11 mwakani (mkoa).

Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake (Bawacha) na Wazee.
Chanzo kimeeleza kuwa kupatikana kwa uongozi katika ngazi hizo kutaiwezesha Chadema kuwa na mtandao utakaohusika katika kulinda nafasi za wagombea uwenyekiti wa mitaa, vitongoji na vijiji, udiwani, ubunge na urais.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwembe Mmoja (CCM) mkoani Mtwara , Abdallah Suleiman Mnyalu, alisema kazi za kisiasa hususani kukutana na kuzungumza na wananchi, zitaiathiri CCM katika chaguzi zijazo.

Alipotakiwa na NIPASHE Jumapili atoe maoni yake kuhusu athari za Chadema katika ngazi za msingi kwenye jamii, Mnyalu alisema chama hicho kinafanya kazi zilizopaswa kufanywa na CCM, lakini chama hicho tawala kimelala.

“Wenzetu hawa wanapita na kukutana na wananchi, lakini sisi wenye dola hatufanyi hivyo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Mnyalu alisema pia kuwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi za msingi vimechochea chuki ya wananchi kwa chama tawala, hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani hususani Chadema kuungwa mkono.

MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO

Imebainika kuwa Chadema imejizatiti kutumia njia mbalimbali kuwafikia wapiga kura, wakiwemo wasiojitokeza na kushiriki shughuli za kisiasa hadharani.

Kupitia mkakati huo, imeelezwa kuwa chama hicho kitatumia njia ya mitandao ya kijamii iliyopo kwenye mawasiliano ya kisasa, kupenyeza kampeni na hoja zake.

MKAKATI WA KUJIENEZA

Kikiwa katika Operesheni Okoa Kusini inayoendelea kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, Chadema kinawatumia viongozi na makada wake kufika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata ambapo wanazungumza na wananchi, kufungua matawi na kusimika uongozi wa muda.

Jana, Chadema kilichoanza ziara zake mkoani Mtwara Mei 27, mwaka huu, kimeingia mkoani Lindi ambapo kitafanya mikutano ya hadhara na kufungua matawi yake hadi Juni 9, mwaka huu kitakapofanya mkutano wa hadhara mjini Lindi.
Waandishi wengine bwana sijui hawajaenda shule?inasikitisha kuona mwandishi anaandika vitu hivi napenda kumuuliza hivi ametumwa na nani?
 
Unapokuwa chama mbadala lazima kuchunga sana namna unavyowaandaa wananchi kupokea utawala wako.Ukifanya mambo yasiyo na tija ujue nawe utafanyiwa hivyo hivyo kwenye utawala wako.
 
huu ni ufisadi wa wazi kabisa, yaani ningejua ndo ni huu upuuzi umeandikwa wa mambo yanayosemwa majukwaani huku utitiri wa watu ukishuhudia kuwa ndo siri, wala nisingepoteza muda wangu kusoma hii sredi.. imeniudhii...
 
Nimefurahishwa na hii habari, kutokana na kichwa cha habari hii naamini imepata wasomaji wengi,
wasomaji wameweza kujua kuwa chama wakipendacho kimedhamiria kushika dola. Safi sana!!!
Tuna ichangia CDM ili iweze kufanya hayo yaloandikwa. hongereni sana makamanda!
 
Mm, bado hii ni siri, akiiweka wazi itakuwa si siri tena. Huyu mwandishi alitaka kujaza tu gazeti ili litoke. Kwani huwezi kutoa gazeti ukurasa mmoja ukiwa empty?

tehe tehe tehe..ati ukurasa mmoja ukiwa empty..
 
Persistance!Persistance!Persistance!
GO CDM GO!
Mwandishi kapewa kibahasha kaishia kuandika udaku!kwi kwi kwi!
 
Hii ni siri na kwa maana ya siri anae ijua siri hiyo ni mwenye siri yake, hapa mwandishi aliye taka kuitoa siri yeye kaitangaza na bado ameamua kuificha siri yake na kutufanya tupate tabu kuitafuta siri aliyo ianika kwa siri.
Kumbe Mgeta nae ni walewale wa global publisher.
 
Mashaka Mgeta | Nipashe Jumapili | 3rd June 2012

Maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imebainika kuwa ni sehemu ya mikakati yake inayolenga kuibua chuki za wananchi na kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Vyanzo vya habari ndani vya Chadema ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, vimelieleza NIPASHE Jumapili kuwa, chama hicho kilifanya tathmini na kubaini kasoro zilizochangia kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Miongoni mwa kasoro hizo, ni ari ndogo iliyojitokeza kwa wananchi kulinda kura za wagombea urais na ubunge kupitia Chadema.
“Ili wananchi wawe tayari kuona umuhimu wa kulinda kura za chama cha siasa, inabidi wawachukie watawala, sasa tunachokifanya ni kueleza upungufu wa chama tawala ili wananchi waamke, waichukie CCM,” kilieleza chanzo hicho.

Hata hivyo, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mahakama jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitaendelea kuwachochea wananchi kuiasi CCM na kukiunga mkono chama chake.

Mbowe alisema, “wanasema Mbowe ni mchochezi, wanasema Chadema inapandikiza chuki, mimi na chama changu tutaendelea kuuhamasisha umma kuondokana na woga, wawachukie watawala walioshindwa kuwaletea maendeleo.”

Chadema imekuwa na utaratibu wa kuandaa maandamano na mikutano ya hadhara kupitia kile kinachojulikana kama operesheni maalum, mathalani kwa sasa ikijulikana kama Operesheni Okoa Kusini.

KUCHUKUA MFUMO WA CCM

Kwa upande mwingine, mkakati uliobuniwa na kuzinduliwa na Chadema, ukijulikana kama Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) umetajwa kama wenye lengo la kukisimika chama hicho hadi kwenye ngazi ya ubalozi, kama ilivyo kwa CCM.

Kupitia M4C Chadema inajikita kwa ‘kuvuna’ wanachama na kusimika uongozi katika ngazi tofauti kuanzia mabalozi, matawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hatimaye taifa.

Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.

Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.

“Tunapoingia ndani ya jamii kufikia ngazi za msingi, tawi na kata, tutajihakikishia kuichukua nchi kwa urahisi zaidi,” kilieleza chanzo hicho.

Chadema imetoa maelezo ya taratibu za uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ngazi za msingi na matawi, kikitumia ibara ya 11-1 ya chama hicho na kuzisambaza nchi nzima.

Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa, alithibitisha kuchapishwa kwa maelezo hayo na kwamba yatafanikisha chaguzi hizo kufanyika kwa mujibu wa Katiba.

Maelezo hayo yanataja Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.

Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11 mwakani (mkoa).

Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake (Bawacha) na Wazee.
Chanzo kimeeleza kuwa kupatikana kwa uongozi katika ngazi hizo kutaiwezesha Chadema kuwa na mtandao utakaohusika katika kulinda nafasi za wagombea uwenyekiti wa mitaa, vitongoji na vijiji, udiwani, ubunge na urais.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwembe Mmoja (CCM) mkoani Mtwara , Abdallah Suleiman Mnyalu, alisema kazi za kisiasa hususani kukutana na kuzungumza na wananchi, zitaiathiri CCM katika chaguzi zijazo.

Alipotakiwa na NIPASHE Jumapili atoe maoni yake kuhusu athari za Chadema katika ngazi za msingi kwenye jamii, Mnyalu alisema chama hicho kinafanya kazi zilizopaswa kufanywa na CCM, lakini chama hicho tawala kimelala.

“Wenzetu hawa wanapita na kukutana na wananchi, lakini sisi wenye dola hatufanyi hivyo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Mnyalu alisema pia kuwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi za msingi vimechochea chuki ya wananchi kwa chama tawala, hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani hususani Chadema kuungwa mkono.

MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO

Imebainika kuwa Chadema imejizatiti kutumia njia mbalimbali kuwafikia wapiga kura, wakiwemo wasiojitokeza na kushiriki shughuli za kisiasa

wandugu nimetoka mweupee,kama ni mtihani nimefeli maana sijajua hiyo siri kaandika kwenye aya ya ngapi
 
Kweli hiyo ni siri nzito,pamoja na kusoma habari yote bado imebaki kuwa siri
 
Ndiyo kazi ya dada joyce mhaville hii,
inaelekea amesahaulika kwenye wakuu wa wilaya
anatafuta namna ya kukumbukwa.
 
Huyu mlevi alikuwa amelala baa ya jirani hapo sinza kwa remi, baada ya kufakamia viroba, ndo anakurupuka na kuandika uharo wake hapa jamvi takatifu 'JF'
 
Kichwa cha habar hakiendan na habar yenyewe. Mwandishi anataka u dc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom