Siri nje kujisalimisha kwa anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka

yaaani wamefikria njia zoote wameamua kuja na hii,duuh tat^zo mfumo wa majeshi upo hovyo wanaajiri form 4 failure ndio maana m2 anashindwa hata kudanganya,ishu nyingine ni walivyopanga kumteka hawakupanga mpango wa matokeo ya utekaji ule so walipanga nusu ss wanaumbuka,nimeamini jeshin wanatakiwa waajiriwe wasomi!duuuuh
 
Kwa mawazo yangu ya Hangover, ni hivi.

Utekaji wa Dr. Umewapa wengi hasira, na wengi tumeulaani sana. Na mtekaji

Anajua kabisa kuwa jamii ina hasira nae sana.

Anajua kuwa polisi nao wanahasira nae sana mana kawafanya wao wabebe kesi (Kama kweli si wao)

Anajua Ikulu ina hasira nae sana kwa kuwabebesha kesi ( kama kweli hawahusiki)

Anajua serikali ina hasira nae sana kwa kuichonganisha na wananchi (kama kweli haihusiki)

Na anajua CCM pia ina hasira nae sana (kama hawahusiki).

Sasa huyo mtu najiuliza ana courage kiasi gani ya kujitokeza wazi wazi tena kienyeji bila kuomba Protection huku akijua kuwa tayari ana hao maadui tajwa hapo juu??

Sio ujasiri wa kawaida, najua mtasema kuwa amejisikia guilty sana. Ndio kama ni kweli ndio mhusika ingewezekana "guilty concious" kumtesa ila sio kumtuma alichofanya, zaidi huyu angejiua na kuacha waraka.


NIONAVYO MIMI.
Hii ni njia tu ya whoever anaehusika kufunika tracks zake, lakini ni so cheap and ya kitoto.

Huyu Mkenya sio.
(Hapa hapa JF ilishatabiriwa hii trick yao)
 

Kinachoniudhi ni jinsi akili za watanzania zinavyofanywa kuwa viza kila na siku na vyombo vya usalama. Polisi waliwezaje kumfikisha huyo mtu mahakamani with story kama hiyo, inanikumbusha yuke Dumisani Dube, aliyemgonga marehemu Sokoine. Huu mchezo wa kuua watu haujaanza juzi, umeanza siku nyingi na wanapandikizwa watu wa kutoka nje, huyu mkenya kapandikizwa kama alivyopandikizwa Dumisani Dube aliyetokea ANC ya South Africa

Tangu lini jambazi, mwenye kikundi cha ujambazi, anayejihusisha na silaha, ajisalimishe kwa tukio kama la Ulimboka ambaye wala hajafa.Kama ni jambazi sugu, amefanya mangapi makubwa kabla, why atubu kwa hili tukio moja tu. Kama ni kujisalimisha, aliacha makanisa mangapi hadi aende hilo? mbona hakwenda polisi? Polisi sio vyema kuwafanya watanzania viazi kiasi hicho, it is shameful kwa nchi kama Tanzania kuwa na jeshi la polisi lenye kuwafanya watanzania wapumbavu
 
Sijawai sikia toka tarehe 7/5/1984 nazaliwa kuwa jambazi mtekaji eti ameenda pahala kumuulizia mtu haf akajitambulisha eti mi ndo nlimteka dr ulimboka hawa wabhungaji nao wasituzingue bhana
 

siasa ni mchezo unaonuka..kwa harufu tu urfinished! But as for me,hmm mm sijisumbui kuiweka akilini coz hata kwenye nywele zimegoma! Nastygame..
 
Haiyaaaaa. Tutasikia mengi.
Nimeshangazwa Na jambazi sijui gaidi Sugu, limeenda kutubu tena kwa Mchungaji, wakati hawa wachungaji hawaamini katika kutubu kwa mtu. Ni wakatoliki tu ndio huenda kutubu kwa padri. Sasa la huyu kiboko.
 
Reactions: Nzi
Huyo jamaa mkenya wala sio muhusika wa tukio nahisi. Tokea lini muhusika akaenda kujisalimisha kiulaini namna hiyo?. Huu ni mchezo ambao Usalama wa Taifa wamepanga kuucheza kwa nia ya kuficha kilichotokea na wahusika halisi wa tukio.


Ulichoandika ndio ukweli halisi......hakunaga mtu wa hivyo eti akajisalimishe wakati anajua fika kuwa amefanya jambo baya la kumdhuru mtu......yaani hili ni bonge la movie afu nzuri zaidi stelingi kesha kufa sasa halinogi tena.....labda Kova aje kivingine!
 
.........kweli nimeamini ni heri kuwa mfuasi wa shetani na wanae kuliko kuwa mfuasi wa CCM na serikali yake lol!!

wameshindwa hata ku-plan vizuri jinsi ya kujinasua kwenye mchezo mchafu walioufanya wenyewe, matokeo yake wanajikanyaga kanyaga kwa kutunga tukio la kitoto.
 
Kwanini kova hakuwasiliana na gwajima? Sasa anaumbuka

ina maana kule kwa gwajima waumini criminal wanaotubu hupelekwa polisi sio?
Kanisa lina kazi ya kujisafisha HUYU SELEMANI AMEAMUA KUMTUKANISHA YOHANA MBATIZAJI
 
Tokea Jana najidunga tursker lakini bado hazipandi sijui niende kigogo kwa mama muuza nikanywe ile Yao inayozima macho

Mkulu nakusihi kigogo don't try that at home!! njoo nikuonyeshe manywaji ya kuondoa uchafu wa kina kova akilini, wanaumbuka mwaka huu, hii serikali!! yaani that is the best they can do!???, aliyesema Jk anaangushwa na watendaji wake naanza kumuamini,maana yeye(jk) alishaanguka tayari siku nyingi sasa hawa nao kila wakijaribu kumnyanyua wanambwaga tena, duh! No wonder anapenda kwenda nje, hata ningekuwa mimi I cant stand to see the flaws of my government! SHAME ON ME!
 

Natamani sana kwenda kusali kwa gwajima kesho...najua lazima awapige madongo ya kweli
 
Wana Jf hivi huyu Prezdaa amewahi kutoa tamko lolote khs shutuma zinazotolewa dhidi ya serikali yake kuhusiana na matukio yanayoambatana na kutekwa kwa Dr. Ulimboka? Hivi si ndio viashiria vya wazi wazi vinavyo onyesha kwamba kumbe inawezekana hata wakati Dr. Ulimboka yuko katika mateso usiku ule Rais JK alikuwa anajua kilichokuwa kinaendelea? After 2015 huyu prezdaa anatakiwa aonje joto ya Segerea..
 
Sijawai sikia toka tarehe 7/5/1984 nazaliwa kuwa jambazi mtekaji eti ameenda pahala kumuulizia mtu haf akajitambulisha eti mi ndo nlimteka dr ulimboka hawa wabhungaji nao wasituzingue bhana

Laiti ungelimsikia mchungaji huyu. Amelaani vikali kitendo hicho. Inavyoonekana picha ilichezwa bila kumshirikisha Gwajima.
 
Huo ni mchezo2 haiwezekani muhusika kujitokeza kirahisi hvyo kwn alishindwa kwenda kutubia kwao,apo ni njama2 za serikali anahukumiwa miaka kumi na k2 hv anafungwa mi2 badae anapotea zake na dau nono...
 
Tetesi ni kuwa, ripoti iliandaliwa kabla ya utekaji, ambapo siku 3 baada ya kutoonekana kwa Uli, mwili wake ukiwaumeanza kuoza ungekutwa huko Magwepande ambapo uchunguzi wa kiitelijensia ungeanza mara moja na kuja na iyo ripoti. Bahati nzuri Mungu alikua upande wetu, dr hakufa, kuonyesha Mungu bado anatupigania, akawasahaulisha akina Kova na kenge lake, wakashindwa ku-edit ripoti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…