Kuibuka kwa Makanisa ya Upako wa mafanikio

Cybercurex

Member
Jan 19, 2023
76
177
Nimetafakari kwa kina kuhusu kuibuka kwa makanisa ya upako wa mafanikio.

Kikubwa nilichogundua ni kuwa Tatizo kubwa ni umasikini na matatizo ya aina tofauti tofauti.

Kwangu mimi ninaweza kusema kwamba kuibuka kwa makanisa mengi ya aina hii si ishara kwamba Wengi wanamtafuta Mungu saana, la hasha bali ni kutatua changamoto zinazowakabili.

wanaofungua makanisa (wachungaji)na wanaohudhuria kanisani hapo (waumini) wote wapo kimahususi kwa ajili ya shida hizo

Matatizo kama magonjwa, umasikini na ukosefu wa ajira ni mambo ambayo yanawapeleka wengi kutafuta sulusisho makanisani.

Imagine mtu ana miaka 3,5 au 7+ amemaliza masomo na hana ajira ametafuta huku na kule hakuna msaada anaposikia makanisa haya ni lazima ashawishike kuhudhuria kanisani hapo.

Ukisiliza matangazo ya haya makanisa utakubaliana na mimi kwamba wanacheza na akili za watu, matatizo makubwa yanayowakabili watu ndio hayo yanakuwa sehemu ya tangazo hilo. Mfano "Je umetafuta kazi muda mrefu na hujapata, umetafuta mtoto kwa miaka mingi? Unafanya biashara na hupati faida? Unahitaji kupandishwa cheo?" na mengine mengi ya namna hii.

Si Tanzania pekee bali afrika nzima, hii ni kudhihirisha kwamba Afrika nzima inakabiliwa na umasikini mkubwa kwa raia wake. Cha kusikitisha ni kuwa umaasikini unaendelea kutawala na wachache sana wananufaika.

kuna siku nilikuwa naangalia kituo fulani cha luninga, yule mchungaji akasema nataka mtu masikini sana kanisani kwangu awe na utajiri kama wa milioni mia mbili(200M), watu wakarukaruka sana na kushangilia.Sasa ni ukosefu wa fikra yakinifu au ni kufungwa akili Sijui.

Lakini bado najiuliza ni kwanini wanawake wengi ndio wahudhuriaji wengi katika haya makanisa
 
Hilo la wanawake kwanini ni wengi muulize mama yako nafikiri atakupatia jibu sahihi. Siku zote mama huwa yuko tiyari afanye chochote kulinda familia.

Pia mbona hushamgai baa na groceries kujengwa kila mahali wewe unashangaa kanisa ambalo linahubiri neno la Mungu. Acha ujinga pumbavu
 
Kweli chanzo ni maskini.

Hata baada ya maombi ya kila siku, hakuna aliyemsafi na hakuna hata mmoja anayemliki mali za maana.

Mtu anashindwa kumiliki tin number,ila ana ndoto za kumiliki magari, makontena toka china.

Ndoto zikiisha ndio anakumbuka kuanzisha genge, mama ntilie nk

Kama ilivyo kwa waganga wa kienyenji na wachawi, wanasiasa , mitume na manabii. Wanawake ndio wateja wao wakubwa.
 
Back
Top Bottom