Siri nje kujisalimisha kwa anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri nje kujisalimisha kwa anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyenyere, Jul 14, 2012.

 1. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Yule mkenya anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka na kisha kujisalimisha kwa mchungaji Gwajima hakwenda kutubu. Katika mahojiano kati ya mtangazaji Rita Chiwalo na mmojawapo wa wachungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima (anaitwa Gwandu Mwangasa) , mtu huyo alifika jana kanisani hapo na kukutana na baadhi ya wachungaji akitaka apelekwe kuonana na mchungaji Gwajima. Wachungaji hao walikataa katakata kumruhusu mtu huyo mpaka pale atakapowaeleza sababu hasa ya kutaka kuonana na Mchungaji wao mkuu. Ndio mkenya yule alipodai kuwa anajambo la kumweleza mchungaji Gwajima kwa vile ndiye aliyemteka Dr. Ulimboka.

  Baada ya kusikia hivyo wachungaji wale walistuka na kuamua kumkagua simu yake na kukuta ujumbe unaosema "nimefika lakini bado najaribu kuwazoea." Ni ujumbe huu ndio uliopelekea wachungaji wale kumtilia mashaka mtu yule na kumwona si wa kawaida hivyoo kuamua kumripoti polisi. Pia mtu huyu hakwenda kanisani pale kutubu zaidi ya kujitambulisha tu kuwa ndiye mtekaji. Ndipo wachungaji wale wakaona suala lile si la kikanisa tena bali la polisi.

  Katika hatua nyingine mchungaji huyo ametoa onyo dhidi ya watu wanaofanya usanii makanisani kwa lengo la kufanikisha mipango ya makundi fulani. Ameonya dhidi ya dhihaka zinazofanywa katika nyumba za ibada kwa malengo binafsi na kuwa wanaofanya hivyo wanachuma laana. Amesisitiza kuwa ule ujumbe wa simu unaashiria mtu yule alikuwa na ajenda ya siri.

  Ssource: WAPO radio FM.

  My take... You be a judge!
   
 2. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Kova uko wapi?
   
 3. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,530
  Likes Received: 10,442
  Trophy Points: 280
  tutasikia na kuona mengi chini ya serikali ya jk.!
   
 4. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa mkenya wala sio muhusika wa tukio nahisi. Tokea lini muhusika akaenda kujisalimisha kiulaini namna hiyo?. Huu ni mchezo ambao Usalama wa Taifa wamepanga kuucheza kwa nia ya kuficha kilichotokea na wahusika halisi wa tukio.
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo mwaka huu
   
 6. hodogo

  hodogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 239
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini kama kweli picha ndo hii basi laana ya kujaribu kuitwaa roho ya Dr Ulimoka inaawaandama, na naomba na kusali iwaandame wote walio nyuma ya mpango huu. Ninachojiuliza bila jibu ni kwamba kama kweli kuna mkono wa serikali kama visemavyo vyombo vya habari vikidai kumnukuu mtu huyo, je yuko katika chombo sahihi? Haiwezi kuwa kesi ya Nyani kumpelekea Ngedere awe hakimu? Je hakuna picha mpya inachezwa hapa?
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  It without a doubt that our police forces are trying to "clean" their dirt using a criminal in their records. It is a shame that will go with Kova to his grave.
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa atajieleza kwamba alitumwa na CHADEMA. Hiyo itakuwa imeisaidia sana CCM kuweka ushahidi kwamba CHADEMA ni chama haramu. Na mwisho wa siku hamtakaa msikie kesi ya huyo Mkenya na wala hamtasikia kufungwa kwake, na kazi itakuwa imeisha. Chezea usalama wa CCM wewe?
   
 9. ERASTO SYL

  ERASTO SYL Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hadithi yote hii ni ya kusadikika sana katika uhalisia.Imeandaliwa story itakayoleta maana ili mtu huyo aliyepandikizwa apotoshe ushahidi wa kweli. Jiulize;
  1. Jambazi gani linaweza kwenda kanisani kujitambulisha kirahisi tu kuwa ndiye lililomtaka Dr. Ulimboka? Hii inahitaji mabadiliko ya kweli ya moyo na tabia ambayo yanaambatana na toba ya kweli na kujutia tabia...SIYO TUKIO MOJA TU!!
  Angejikuta anamtafuta yule aliyemtendea na ku-make peace nae kabla hata ya kanisani.Na kama angeenda kanisani angependa iwe siri sana kwanza ili aweze kueleza yaliyotokea si kujipeleka kirahisirahisi na kuweka viashiria waziwazi.THIS IS FAKE!
  2. Mbona hawakuonesha picha yake jana kama huyo mtu wamemwamini kama wanavyofanyaga katiika wahalifu wengine?
  3.Kwa nini huyo raia wa kesha kitambulisho chake ni cha miaka 2 tu wakati ana umri mkubwa sana wa kuwa na kitsmbulisho cha muda mrefu nyuma?

  MY TAKE: Kuna usanii katika hili na jeshi la Polisi wanatuingiza watanzania wote kuamini hili ndio maana wametoa taarifa harakaharaka.It doesnt look true!
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wanajaribu kutudharau kiakili. Kova ajue tu kuwa mtu mwenye akili kubwa hadanganywi na mtu mwenye akili ndogo.
   
 11. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanini kova hakuwasiliana na gwajima? Sasa anaumbuka
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nilishasema tangu jana.
  Kova amewafanya Watanzania wote ni wapumbavu.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tokea Jana najidunga tursker lakini bado hazipandi sijui niende kigogo kwa mama muuza nikanywe ile Yao inayozima macho
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  There u r,hilo ni changa la macho,usikute hadi hao wachungaji kuna baadhi ni TISS na ndio wametoa direction ipelekwe polisi na mkuu wa kituo kashapata maelezo ya kova!
   
 15. manshiroo

  manshiroo Senior Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakupa big up sana Hebu tujiulize hivi kweli kijana mkenya ateke mtu kazi imalizike iwe kwa mafanikioa ama la walikuwa na sababu gani ya kumwacha hapa Tanzania? Pili je yeye kama ni jasusi kweli kazi yake haikufanikiwa walishindwa kumdhibiti hadi amwache eti aende kwenye maungamo? Haya sasa limekuja hili kwammba hakwenda kutubu bali kufanya uhalifu mwingine na sasa this time anamshirikisha hadi Gwajima, swali la msingi je huyu Gwajima alikuwa na interest gani na ulimboka?

  hivi kunashida gani sisi wenye akili tukiona kama vile inatengenezwa fiction ground ambayo wataalaam wa criminal minds and investigation tunaweza kusoma kwamba kijana huyu siyo muhusika kwenye hili bali wanamtengenezea platform ili kuhadaa wenye akili? uzuri ni kwamba Ulimboka can tell us kama ndiye aliye muona ama la.

  Jamani kinachotokea hapa siyo kwamba havipo vipo kabisa na TISS wanauwezo wa kutengeneza platform kwa kutumia records za most crimanals ili kusadikikisha watanzania wakijua kuwa sisi ni mambumbu. wasiunderestimate we can even do surveillance though GIS and see what happened and who were present at scene. tumeona GIS ikitumika kwenye criminal detection sehem nyingi ulimwenguni and now tunaowataalam wa GIS hata kama ni kwa kuchangia wengne tupo tayari we have to stop this foolish.
   
 16. r

  richone Senior Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  huu ni uwongo kabisa. hii ni janja ya CCM,TISS nadhani KOVA anatuona sisi wananchi ni wajinga kama wao.bado tunasisitiza serikali ndio imefanya ujinga huo na hili la aliyejitokeza lwao wenyewe wamelisuka ili kupoteza ukweli.
   
 17. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mtuhumiwa wa kwanza wa tukio hilo ni yule ambaye Dr. Ulimboka mwenyewe alimtambua na kumwambia amrudishie simu yake, huyu Mkenya ni danganya toto tu!. Kama kweli alihusika wasubiri Ulimboka arudi amtambue mwenye halafu akashitakiwe Kenya ikiwa ni kweli kahusika na sio serikali ya CCM kutuletea sanaa zao.
   
 18. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Na mm nmesikiliza waporedio fm kwenye kipindi chao cha patapata asubuhi ya leo .kazi tunayo mwaka huu Mungu atusaidie mana
   
 19. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  ERASTO SYL Tangu jana nilikuwa nataabika akilini kuwaza ni majambazi sugu wangapi wanakwenda makanisani kufanya confession na kisha kuwa waumini wazuri tu wa makanissa bila taarifa zao kuripotiwa polisi. Why this time!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Bila shaka walichukua namba ulikotumwa huo ujumbe.
   
Loading...