Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Suala la Kenya, serikali yetu ilikuwa haina msimamo na haikuwa na nia ya kuingilia kati au hata kutoa tamko la kulaani uvunjwaji haki wa binadamu nchini mle kwa kile ambacho kilionekana kutokuingilia kati mambo ya nchi nyingine. Ndipo JK kama aliyepigwa funguo na akawa kama energizer bunny akaruka kwenda Nairobi na masaa machache ujumbe ukafika!
Msimamo huo hata hivyo ulikoma masaa machache baada ya Ikulu ya Marekani kuzungumza na Ikulu yetu na kutoa "pendekezo" na ushauri kwa Rais wetu kupeleka ujumbe wa wazi kwa Kibaki kuhusu "fimbo na karoti"...
Likaja suala la Zimbabwe ambapo serikali yetu haikutaka kujihusisha kabisa na kumuacha Rais wetu aendelee na misafara yake ya ki Vasco Da Gama hadi pale alipokuwa Uchina alipopata simu nyingine toka kwa Bush iliyomtaka (kama kiushauri wa kirafiki) afuatilie suala la Zimbabwe na Marekani iko nyuma yake. Zaidi ya yote wakaamua kufuta ziara ya Waziri Mkuu na kuona ni bora aje yeye mwenyewe ili "wazungumze". Kwa mara nyingine tena JK akakatisha ziara yake ndefu huko Ulaya na Asia na kugeuza ili kujiandaa kwenda US huko Makamu wake akienda kule UK na Scandinavia kuziba pengo na hivyo kwa mara ya kwanza kumuachia Pinda "kufanya vitu vyake" huku nyuma.
Sasa kama Rais wetu hawezi au hataki kupima uzito wa mambo ya bara letu yeye mwenyewe na kuona umuhimu wa kuonesha uongozi basi ajiandae kuongozwa na wanoona uongozi! Sipendi kabisa Rais wetu asubiri simu na ahadi toka DC ili aweze kuamua nini cha kufanya next.
Well, on the other hand yawezekana kuwa this is the best thing to happen to Kikwete kuwa angalau ana mtu/watu wa kumuongoza! Sasa Bush akiondoka itakuwaje?