Sioni vita dhidi ya ufisadi ikifanikiwa

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,241
113,613
Wakati mwingine huwa nikifikiri sana juu ya hii iitwayo vita dhidi ya ufisadi, naishia kukata tamaa kabisa.

Nyakati zingine huwa najiuliza kama kweli huo ufisadi upo au ni jambo la kufikirika tu.

Wale waliokuwa mstari wa mbele kupigana hiyo vita sasa wamekuwa ndo watetezi wa watu wale waliokuwa wakiwatuhumu kuwa ndo mafisadi.

Na wale walokuwa na kigugumizi kukemea na kuupiga vita ufisadi sasa eti ndo wako mstari wa mbele kupigana hiyo vita.

Hapo ndo unaona ubovu na uozo wa siasa.

Leo hii wale wote waliotajwa kwenye ile iliyoitwa ‘list of shame’ wakikamatwa na kwenda kufunguliwa mashitaka, wale ambao ndo waliyoiandika na kuisoma hiyo ‘list’ watageuka kuwa watetezi wa watu hao hao waliowatuhumu kuwa ndo mafisadi!

Inafika kipindi mtu unashindwa kutambua ni yupi hasa aliye mzalendo wa kweli anayeuchukia ufisadi kwa dhati na nguvu zake zote!!!!

Tanzania hakuna ufisadi. Neno ‘fisadi’ ni chambo cha kujipatia kiki za kisiasa tu.

Bure kabisa!!!!
 
Yote haya ni sababu ya kuiga maneno,hili neno fisadi tulilidaka toka kenya.
Bora kiswahili chetu Tz kinetumika kuwa ni Wizi wa mali za uma.au washukiwa wizi mali za serikali.
 
lowassa juzi alikaribishwa ikulu na jpm kamsifia
unategemea huyu atapelekwa mahakama ya mafisadi kama ccm wanavyosema ni fisadi?
tatizo mafisadi ni wazito,..
kuna mtu alikwapua nyumba za serikali leo hii tunaambiwa anachukia ufisadi!!!!

Na CHADEMA wana ubavu wa kumpeleka nani mahakani endapo wangekuwa na dola??
 
Mmeanzisha mahakama ya mafisadi kwa sasa wanaishi ndege na popo. kila anayekamatwa anaishia kuachiwa kwamba mwendesha mashtaka hana nia ya kuendelea na kesi.

Serikali ya CCM ni kama filamu ya vichekesho maana wapinzani kwa sasa ni kama mmewafunga midomo na sasa Vita ya ufisadi imewashinda na kuanza kuulaumu Upinzani.
Endeleeni kununua viongozi wa upinzani labda mtafanikiwa
 
Nyani Ngabu Mkuu nakuambia kama kuna awamu ya uongozi ambao unaiibia nchi yetu,basi ni hii awamu ya tano.

Sina ushaidi lakini kwa akili yangu kidogo na elimu yangu ndogo nilionayo,inanitosha kupambanua mambo.huo ufisadi unaousema ni kelele zinapigwa tu ili tusielewe wanachokifanya nakuambia tena,Watz tunaibiwa. Mungu atutetee tu.!!.
 
Sasa mkuu hivi unafikiri kuna mwenye ubavu wa kumkamata Chenge au mama tibaijuka hebu waambie wajaribu tuone
Tatizo mnapebda kuhamisha magoli,hata akidakwa chenge mtasema bado kikwete
Jinai haina ukomo,kama chenge alivurunda sehemu utafika wakati atatendewa tu haki
 
Mkuu nakuambia kama kuna awamu ya uongozi ambao unaiibia nchi yetu,basi ni hii awamu ya tano.sina ushaidi lakini kwa akili yangu kidogo na elimu yangu ndogo nilionayo,inanitosha kupambanua mambo.huo ufisadi unaousema ni kelele zinapigwa tu.ili tusielewe wanachokifanya.nakuambia tena,Watz tunaibiwa.Mungu atutetee tu.!!.

Huna ushahidi halafu unasema uongozi wa awamu unaiibia nchi?

Duh!! Akili za makamanda bana!!
 
Tatizo mnapebda kuhamisha magoli,hata akidakwa chenge mtasema bado kikwete
Jinai haina ukomo,kama chenge alivurunda sehemu utafika wakati atatendewa tu haki
Umeongea la msingi sana...sisi tunachochea kuni tu...hadi pale pogba na kundi lake nao watendewe haki
 
Kinachonifurahisha ni pale kila upande unamchekea Lowassa ambaye ndo starring mwenyewe wa kashfa kubwa ya ufisadi kuwahi kutokea.
Huku walimpokea na mabusu baada ya miaka nane ya kumponda.
Huku wanamkaribisha na kutukumbusha wao ni dam dam.

Tuseme tu kwamba nchi sio yako, tumekodisha tu.
 
Lakini ingefaa kufafanua fisadi ni nani au anapayikana wapi Magufuli alisema hakuja Ikulu kufukuwa makaburi, alichofanya yeye ni kuweka kufuli jipya kwenye mlango uliokuwa unatumiwa na Mafisadi. Hivi sasa huoni tender inayopatikana kinyenela, hakuna mwekezaje anayepata kibali kwa njia ya mkato au kibali cha kufanya kazi hupati kwa bahasha ya kaki. Wakuu wa idara na mashirika hakuna trip za ovyo, hakuna kujilipa mishara mara mbili....nk nk
 
Back
Top Bottom