Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,616
- 1,778
Mwanzi1, ishara ya kifo cha vita dhidi ya ufisadi katika awamu hii ambayo ilijinadi kupambana nayo ilionekana mapema tu baada ya uchaguzi 2010 kufuatia matukio mawili makubwa: 1. Kesi ya rushwa dhidi ya wabunge wa ccm kufutwa unceremoniously. 2. Wabunge wa ccm walipogawiwa bahasha za 10m/= kila mmoja na uongozi wa Bunge kukataa swala hilo kutolewa kauli bungeni! Dhamira ya chama cha siasa kupambana na ufisadi inaweza tu kupimwa pale inaposhika dola. Kabla ya hapo ni propaganda tu. Kama kweli tuko serious na suala hili basi tuache kuwaweka kwenye kapu moja watu wenye madaraka ya dola na wale wasiokuwa nayo. Kufanya hivyo ni kutaka tu kuwaaminisha raia kuwa walioko nje ya madaraka nao pia hawawezi!