Siogopi kushare mume, naogopa HIV

Siogopi kushare mume, naogopa HIV

Shem asante kwa kunisaidia kujibu...

Labda niongeze kidogo,kitendo cha huyo mwanaume kufanya kwa kujiiba maana yake anajua kuwa ni kosa, kwa kuwa huyu bi dada kagundua basi anaweza kutumia mwanya huo japo kutikisa kiberiti.

nalianzisha kwa kweli ajue nimegundua tu hiyo itatosha pengine
 
Inabidi utumie mpira ukikutana kimwili na mumeo.Nakushauri uongee nae kuhusu mahusiano yake na huyo mwanamke mwengine,mwambie kuwa unajua ana mahusiano na mtu na umsikilize atasemaje,mshauri avunje mara moja huo uhusiano kwa manufaa yenu na watoto!!Ukifanya kitendo cha kumuwekea condom au umuombe atumie kinga ataelewa kwamba wewe unaafiki matendo yake maovu anayoyafanya..Itakuwa kama tiketi unampa afanye ayafanyayo kwa uhuru na itashusha heshima kwenye ndoa yenu,hilo sio jambo la busara.Kama amekuoa wewe inabidi wewe ndio mtu wa pekee utakayekidhi mahitaji yake ya kimwili na si vingenevyo.
Unataka kuniambia haikuumi hata kidogo kitendo cha mumeo kuzini nje?Hivi unampenda kweli huyo mumeo?
Nawasihi wote wawili mkacheki afya zenu!
Bila shaka wewe si mwanandoa.
 
we kweli mwanamke wa ajabu!!!!!!!

mbona ningekupata ingekuwa sherehe daily...(but sio kwa kutoka na wadada wengine, nooo!!! but by keeping you happy day to day)

kwanza kabisa, naomba nishauri wewe kwanza, nenda kajijulie hali yako ya afya, jifahamu kama una vvu ama la kwa sababu, muda ambao umegungua mmeo ana kidosho kingine nje, yawezekana alikuwa na mwingine ambaye humfahamu na yawezekana alikuwa akitembea nae bila kutumia kinga!.... zaidi zaidi, akaja tena kwako as a wife, kula tunda la uzima bila kinga.. please kapime kwanza..!
View attachment 113454

thanks dr, ntazingatia
 
Dah ningepata mke kama wewe ningeacha uzinzi siku hiyo hiyo. Ushauri mwambie kuwa unajua ana nyumba ndogo na unamwomba awe anavaa kinga. kama ana akili timamu atamuacha kabisa.

thanx dr, ntamwambia
 
Pole sana, kwa jinsi ulivyojieleza nimepata picha ya ''hekima na busara'' uliyonayo. Siku zote ukweli hutuweka huru, kaa uongee nae juu ya hilo. Katika maongeza usimkataze kutoka nje ya ndoa bali mpe sababu za kutokutoka nje ya ndoa. Mf: maladhi(HIV), Kujivunjia heshima na utu, Kuongeza gharama za maisha n.k. Lakini ni wakati muafaka wa wewe kujitathimini. Angalia kipi kinapungua uongeze au tafuta madoido kama sio majonjo mapya. Mwenyezi Mungu akutangulie.
 
ila tu awe makini, kuna wanaume ukitikisa kibiriti ndio ushamkosa huyo ubaki unahaha. lol

hahaha unanichekesha shost, ndo yale ya kila mtu achukue hamsini zake
 
Unataka ukae kimya kwani mumeo wakati anakuoa mliandikiana mkataba smolo hauzi ni sehemu ya ndoa yenu???

We endelea kucheka cheka na kuweka moyo wa huruma, au umesahau waungwana husema 'mchelea mwana kulia hulia yeye'.

yaani best natamani mimi ningekuwa kwenye position ya bi dada hapa,huyo mwanaume na hawara yake wote wawili wangeipata pata fresh.......hapa anahalalisha kuharibu future ya familia yake kisa small house hehehehehehe kweli upele haujapata mkunaji@
 
from my experience! Suprise pole sana mwanamke mwenzangu usimsikilize mtu anayekuambia usikague simu ya mumeo,mimi hapa kila siku lazima nijue huyu bwana amewasiliana na nani sent items,inbox, na alijibu nini nikishamwandalia maji yakuoga akijimwagia akisha jipaka sabuni machoni mimi nakagua simu mpaka amalize kuoga nimemaliza na hajawahi jua mimi nakaguaga hiyo simu years after years now.ni miaka sasa ,mume wangu si mhisi na sijawahi mkuta na baya ila abiria chunga mzigo wako na anajua kabisa once i suspect something namletea mpaka picha hapo.''KNOWING YOUR ENERMY IS HALF VICTORY '' Suprise
Ushauri wangu.
anza kumpakia kondom za kutosha ,siku ya kwanza ,ya pili,ya tatu akikuuliza mwambie ni mimi nimekuwekea kinga mwenzangu ukatumie na fulani,usije niua bure kuna magonjwa!ohh nani kakuambia mwambie tu najua A-Z ya unayofanya na nimekuvumilia naona sasa baaaaasi nafikiri nikupe sabatical leave uendelee nje ya ndoa ukichoka urudi tupime ukimwi maisha yaendelee.mwambie siwezi acha mtoto wangu /mtaje jina yatima kwa ajili ya tamaa yako.baasii ila tumia kondom japo inauma sana.Jitahidi umjue mwizi wako ndani na nje na imekuwaje akampata!

thans dr, ntaongea nae
 
Pole sana, kwa jinsi ulivyojieleza nimepata picha ya ''hekima na busara'' uliyonayo. Siku zote ukweli hutuweka huru, kaa uongee nae juu ya hilo. Katika maongeza usimkataze kutoka nje ya ndoa bali mpe sababu za kutokutoka nje ya ndoa. Mf: maladhi(HIV), Kujivunjia heshima na utu, Kuongeza gharama za maisha n.k. Lakini ni wakati muafaka wa wewe kujitathimini. Angalia kipi kinapungua uongeze au tafuta madoido kama sio majonjo mapya. Mwenyezi Mungu akutangulie.

Amin ma de, labda nikiongea nae anaweza niambia mapungufu yangu niyaongezee
 
yaani best natamani mimi ningekuwa kwenye position ya bi dada hapa,huyo mwanaume na hawara yake wote wawili wangeipata pata fresh.......hapa anahalalisha kuharibu future ya familia yake kisa small house hehehehehehe kweli upele haujapata mkunaji@

Asnam ma dr, ndio maana nimeleta jamvini lenfo kupata njia ya kusolve, nipe basi maujanja
 
best , na mawazo yako yahitajika pia
Ni vigumu sana kumwambia mumeo mtumie condom kwa kutoa kigezo cha kutomwamini, unless umwambie mnafanya family planning.
anyway, kuna mambo mengine hayashauriki so akili kichwani mwako.
 
Uoga ni donda ambalo muda wote lasubiri kupasuka...ndio dalili ya mwanzo kabisa ya kuonewa na kufanywa mtumwa.

Unless huyu bi dada hajiamini kitandani au ana excuses nyinginezo kiasi kwamba anaona bora tu huyo mumewe apunguze mihemuko yake huko nje...

yaani best natamani mimi ningekuwa kwenye position ya bi dada hapa,huyo mwanaume na hawara yake wote wawili wangeipata pata fresh.......hapa anahalalisha kuharibu future ya familia yake kisa small house hehehehehehe kweli upele haujapata mkunaji
 
Uoga ni donda ambalo muda wote lasubiri kupasuka...ndio dalili ya mwanzo kabisa ya kuonewa na kufanywa mtumwa.

Unless huyu bi dada hajiamini kitandani au ana excuses nyinginezo kiasi kwamba anaona bora tu huyo mumewe apunguze mihemuko yake huko nje...

ndugu unahisi kuna excuse itakayomhalalisha yeye kwenda nje kweli
 
ndugu unahisi kuna excuse itakayomhalalisha yeye kwenda nje kweli
Kilichonisukuma kuomba
msaada hapa ni how to handle the situation coz
sina hofu hata kidogo kushare hilo penzi najua
ipo siku atachoka atarudi.

Wewe tayari nafsi yako imeshakubaliana na hayo afanyayo mumeo...
'Siogopi kushare mume, naogopa HIV' haya ni matamshi ambayo mtu asiyejitambua ndiye pekee anayeweza kutamka.
Jaribu tu kufikiria kama kweli unaogopa HIV kwa nini uwe tayari kushare mume?
Hivi huoni kuwa kitendo cha kushare mume ni moja ya mwanya wa kufanya maambukizi ya VVU?
Ndio maana ninahisi pengine una weakness fulani kwenye suala zima la kungonoka na mumeo kiasi cha kukufanya kufikiria na kuamua uamuzi mgumu kama huo...
 
sina ushauri
Hongera sana kwa kutoogopa kushare

Hivi vikombe vipite mbali aisee

Maana nikigundua baba chanja wangu anagawa utamu wangu itakua balaa,

Uwiiiiiii


Nakutakia busara katika kusolve hilo

Viatu vingine havivaliki aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom