Zipuwawa
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 3,050
- 657
Hizo mbinu unazotaka kutumia zinaweza kufanya mumeo aendelee kukusaliti na mwisho kuleta magonjwa ndani cha muhimu hakikisha unapata taarifa za kweli na za uhakika za huyo kimada wake. Ukishapata information zote hapo unahaki ya kumwambia ukweli maana kwasasa ukimwambia kuwa umesoma msg anaweza kukudanganya na mkajikuta nmnagomba bila kupata suluhisho na yeye kuamua kutafuta njia nyingine za kuendelea na huyo demu. Sasa anza kazi ya kumfuatilia katika mambo yake ukiona unashindwa basi pambana nae mwambie tu aache ujinga wa kutembea na wanawake wengine na kumpa hasara za vitendo avifanyavyo kisha uone anabadilika au anaendelea. Kumuwekea condom kwa bahati mbaya utaweka ndani bila kujua akazikuta na kutokuamini wewe mkazua mambo mengine. kumwambia atumie kondomu hakika atakuwa huru sana na kuendelea kusherkea na hatimae anaweza kuhama hata hapo nyumbani akijua fika unamruhusu kufanya uzinzi. Daima kemea sana uzinzi mara ugunduapo katika ndoa kwani una madhara mengi .