Sio Mungu tu tuliyemkataa

Sio Mungu tu tuliyemkataa

Wao pesa mbele kama mfuko wa shati!ukitaka uheshimiwa na uthaminiwe we kata kobunda ukiingia unapokelewa unaonyeshwa siti za mbele
Hata bible yenyewe imekataza ila nature ya binadamu baadhi.kuheshimu wenye pesa zaidi.
Na sio madehehebu Wala ya upako wote wako hivyo.
Mi nkasema acha Mungu anihukumu maana ye ndio Anajua situation halisi.
Ukikaa mara Kuna tour bagamoyo
Mara kuna trip mikumi
Michango 80,000...70,000
100,000

Hakuna hata trip ya kwenda kutoa msaada Kwa yatima au hospital
 
Hata bible yenyewe imekataza ila nature ya binadamu baadhi.kuheshimu wenye pesa zaidi.
Na sio madehehebu Wala ya upako wote wako hivyo.
Mi nkasema acha Mungu anihukumu maana ye ndio Anajua situation halisi.
Ukikaa mara Kuna tour bagamoyo
Mara kuna trip mikumi
Michango 80,000...70,000
100,000

Hakuna hata trip ya kwenda kutoa msaada Kwa yatima au hospital
Bora ujikalie pembeni aisee Mungu anasikia hata ukiomba sirini!
 
Usipoaamini wewe inatosha Mzee
Mie sijakulazikiaha Yamini kwamba yupo.
Umeniomba mwenyewe nithibishe halafu unaniita mwehu
Uko sawa?
Huo uthibitisho umeuweka wapi nikaacha kuusoma? Wehu ni yule badala ya kujibu hoja anarukia personality, thibitisha uwepo wa Mungu, acha porojo.
 
Kimsingi upo sahihi mkuu,usijali sana maoni ya watu juu ya ulichokiwasilisha,swala la uelewa ni la mtu binafsi,anachagua aelewe au asielewe,contrast ulizoziweka wengine ndo wanaziishi so ni ngumu wao kukupa approval na kukuelewa,bora ya wewe ambaye ushazijua,humu pia watu wanaishi Kwa makundi Mshana Jr anayaita cycle,so Mmoja akipinga hao cycle yake wote watapinga kama mandezi,by the way ni ujumbe mzuri Kwa tafakari ya asubuhi ya jumapili kuliko kuamka tu na kufakamia viporo!!!
Lengo la kuandika makala kwenye majukwaa ya umma ya wazi mfano JF ni kufikisha ujumbe fulani kwa hadhira (wasomaji) yako.
Hivyo lazima uwe na ujuzi wa kutosha wa uandishi. Ujumbe uwafikie wengi waelewe kusudio lako.
Huu ujumbe mahususi kwa matumizi ya watu wengi(public consumption).
Angetaka waelewe watu wachache angewalenga hao moja kwa moja kwa ujumbe binafsi yaani private message (PM).
Angeandika kwa ajili ya manufaa yake binafsi tu angehifadhi kwenye simu, computer au angebandika ukutani chumbani kwake, au angeandika kwenye shajara (diary) yake.
 
ila lengo kuu ni Mungu, kujuliana hali ni ziada tu !
Mungu ni geresha tu la kufanya kanisani paheshimiwe. Ni mhusika wa kufikirika.

Lakini yanayofanyika kule kanisani mfano kuchangisha misaada, kulea watoto, kutoa ushauri, ndo ya muhimu...

Kwahiyo mimi naweza nisimuamini Mungu, lakini nitakua mpuuzi kama nisipoona mazuri yanayofundishwa kwenye dini.

Binadamu alimtengeneza Mungu ili kutanabaisha hitaji lake la kujumuika.
 
Tunafanana mtazamo.
Mimi siendi kanisani miaka mingi Sasa.
Sijinasibishi na dini yeyote.
Naamini Mungu yupo.
Namuomba Mungu kwa wakati wangu kwa faragha.
Siogopi kuzikwa bila ibada ya wafu inayoendeshwa na watu wa kanisa.
Sadaka na zaka zangu natoa kwa mtindo wa kuwasaidia wenye uhitaji pale tu ninapokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Siyo kukamuliwa kilazima kanisani au na watu wa jumuiya ndogo za kikanisa.
Mimi na wewe tuna mtazamo sawa.
Namuamini Mungu ila kanisani siendi ng'oo
 
Back
Top Bottom