ugumu wa maisha kutokana na sababu mbalimbali kama vile uvivu n.k,
hufanya wengi nyakati hizi kukata tamaa kabisa ya maisha na kuacha hata imani zao za kidini, huku wakidhihirisha ukengeufu wao kwa kujipiga kifua na kujivika usomi ambao pia, kwa mtazamo wa kawaida kabisa hata hauonekani kwenye wanachojaribu kukiamini baada ya kuasi imani zao za awali. Zaidi sana, kinachoonekana ni ujanja ujanja tu usioeleweka kwa wanaohubiriwa.
kwani ukiwa na imani yako kwa Mungu au usipokua na imani kwa Mungu, kuna haja gani ya kuweweseka na kubabaika na wasiohangaika na una choamini au usicho amini? Si ukomae na maisha yako kwa amani na kusonga mbele kimya kimya tu na itapendeza zaidi?